MH. KISHOA AJITOSA KATIKA HARAKATI ZA KUMNASUA ISAAC EMILY.
Na Kilawa the Iron
Ule usemi usemao "akufaae kwa dhiki ndiye rafiki" leo umejidhihirisha wazi kwa kamanda J. Kishoa, Mbunge wa CHADEMA toka mkoa wa Singida, baada ya kuguswa na adhabu aliyopewa Isaac Emily kama hukumu kwa kile kilichoitwa makosa ya mtandao yaani cybercrime.
Mh Kishoa kwa Moyo wa upendo akatimiza wajibu wake wa kuheshimu usemi unaosema "undugu ni kufaana si kufanana" kwa kuchangia ths 505,000/=..
Kwa mjibu wa mkusanyaji wa michango hiyo kamanda Godlisten Malisa alisema amefurahishwa sana na upendo aliouonesha Mh. Kishoa na akatoa wito kwa wabunge wengine wa ukawa waige mfano huo.
"J. Kishoa anafaa kuwa mbunge wa kudumu kwani si mara yake ya kwanza kusaidia jamii na vijana wanaonyanyasika.... "Malisa alisema
Pia alieleza kuwa makamande wengine wanampongeza kwa dhati Mh J. Kishoa, na aliwashukuru wote wanaojitoa kwani Vijana wa CHADEMA ni watu wenye umoja sana katika shida na raha.
" Sisi CHADEMA ni familia na tunaishi kama ndugu wa baba mmoja... "Alisikaka kamanda Kwinyara na wenzake ambao majina yao hayakufahamika kwa haraka
Kwa mjibu wa mkusanyaji wa michango hiyo kamanda Godlisten Malisa alisema wabunge wengine walioweza kumtumia michango ni Mh Grace Kiwelu, Mh Lucy Owenya, Mh Yosepher Komba, Mh Cecilia Paresso na Mh Joshua Nassari. Aliwamwagia Pongezi zao na kuwaomba waendelee na upendo huu wa kujitolea
Isaac Emily alikutwa na hatia na kuhukumiwa miaka mitatu jera au kulipa faini ya milion saba (7). Inasemekana pale aliposema ".... Huwezi kumfananisha huyu bwege na Nyerere" kupitia account yake ya Facebook akakamatwa na polisi na ndipo jana hukumu yake ilitolewa.
Mungu Bariki Tanzania