Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 58,978
- 103,352
Kuudanganya moyo ni kosa kubwa, kwani hata viongozi wa dini, nao ni binadamu kama sisi, wanauamuzi mioyoni mwao, nani wamshabikie na nani wasimshabikie, hivyo, Sena kwamba, inawapasa viongozi wote Wa dini hawapaswi kugawika kuhusu vyama, hawapaswi kuegemea chama chochote zaidi ya kuhubiri haki na amani pia kukemea inapobidi
Kwa sababu, dunuiani kila kitu kinawezekana, Watawala wa Dunia wote si wema, kwa kuwa huangalia mambo yao na si ya Mungu
Wachache mno wenye hofu ya Mungu, na huenda tokea utawala ule wa kifalme uliokuwa ukitumika Israeli uishe, tokea hapo, pengine hakujawahi kuwepo mtawala mwenye kutenda kwa hofu na kukubali kuongozwa na Mungu
Fikiri kwa kina, Embu kiongozi yeyote wa kidini, aegemee upande mmoja wa chama, halafu chama hicho kije kianguke kisishike dola, unadhani atakuwa na amani afanyapo kazi zake??
Kalaga bao....
Ponda amefanya jambo la maana sana, tena anatakiwa azunguke na Lisu kila mahali akihamasisha waislamu wampe kura Lisu. Tumeona wazi vingozi kadhaa wa dini wakitumika na serikali hii kufunika uchafu wake. Chaguzi zote toka Magufuli kaingia madarakani zimekuwa zinanajisiwa, kisha viongozi wa dini wakihoji wanatishiwa. Acha sasa viongozi wa dini wapande majukwaani kumpigia Lisu debe. Liwalo na liwe, tunataka amani ya haki na sio amani ya kutishwa na vya dola.