Uchaguzi 2020 Kishindo: Sheikh Ponda atoa neno kwenye mkutano wa Lissu Dodoma, Uwanja walipuka kwa shangwe

Sheikh Ponda kweli amesema kama Lissu hakuchaguliwa, basi Mungu hatapokea Dua za watanzania? Kama ni kweli basi sheikh amekufuru sana, shekh ponda hana uwezo wa kumsemea mungu, na hajui uamuzi wa mungu utakuwaje.
Wasioelewa dini wanashangilia, pia ameongea uongo kusema waislam wamekubaliana, lini na wapi Waislam walikubaliana?
 
Mwili umenisisimka kwa furaha kubwa na isiyoweza kuelezeka,ccm wameshindwa kumnunua Shekh Ponda. Hakika huyu ni Shekh anayesimamia miiko na maadili ya Uislam na kuyaishi!

Kura zote kwa Lissu!
Fuatilia historia ya huyu Sheikh utaelewa kwa nini anamuunga mkono Lissu.

Mpinzani mkubwa wa BAKWATA mwanaharakati wa kupigania haki, ndie sheikh anayeongoza kwa kukamatwa na kufunguliwa kesi na zote kashinda pia aliwahi kupigwa risasi na polisi katika moja ya pilika za kumkamata.
 
Huyu ndio amekuja kuharibu kabisa, maana huwa ana itikadi za kutokupenda amani ya nchi yetu, kwa ujumla Chadema tumebugi sana.
Kuwa mkweli Ponda ni mtu mkweli asiyetishwa na yeyote awaye kwenye masuala ya kudai haki.
Ni jinamizi kubwa kwa ccm Ponda kumu endorse Lisu na majibu utayapata Ponda akienda Zanzibar na Lisu
 
Huyu ndio amekuja kuharibu kabisa, maana huwa ana itikadi za kutokupenda amani ya nchi yetu, kwa ujumla Chadema tumebugi sana.

Hii amani iliyopo ilikuwepo tangu mkoloni alipokuja Tanzania m
Jambo la kwanza alilofanya mkoloni ni kuwaondoa watu aina ya Mkwawa. Na kuwanyongelea mbili wapigania uhuru wote.

Watawala wote wanana awe mloloni mzungu au mweusi.
Hivi unafikiri wakati Mwingereza anatawala walukua wanavuruga amani ?
Ili mtawala apate raha ya kutawala ni lazima pawe na amani.
Amani inayodumu ni ile inayotokana na Haki.
Kukosekana kwa haki kunawaumiza Watu wasio na kitu. Wenye mali na madaraka siku zote hawana shida sana na haki hasa wale walioko laribu na watawala.
Lakini kukosekana kwa amani anayepata shida zaidi ni mwenye mali nyingi.
Leo hii Somalia hakuna Serikali lakini watu wanaendelea na maisha yao . Waliokimbia nchi ni matajiri na watawala .Maskini kwao kila siku ni kama wapo kwenye vita.
Mtu anajangaika na maisha miaka 60 anashindwa kununua hata pikipiki halafu Waziri anakaa kwenye uwaziri kwa mwaka mmoja kwa Kodi ya wananchi halafu anamiliki maghorofa mashamba ,malori,magari ya kutembelea, watoto wanasoma Nje na bima ya afya ya kimataifa na kila aina ya maisha mazuri na familia yake.
Bila Shaka anayehitaji amani ni Mtawala na familia zao zenye maisha mazuri sana na starehe za kila aina.
Lakini maskini anahitaji Haki ili asionewe na kufungwa kwa kuitwa halifu wakati sio. Asionewe kwa kunyimwa uhuru na haki ya kulalamika na kupinga dhulma.

Amani zipo za aina mbili :
Amani inayopatikana kutokana na ncha ya Upanga na Amani inayotokana na Haki.

Amani ya CCM ni amani inayotokana na ncha ya upanga. Hii ni ya kupiga watu risasi na kuwatisha ili wasifurukute hata kama wanadhulumiwa. Amani hii ni kama zile za nchi za Kidikteta. Hii Amani inawanufaisha watawala zaidi na watoto wao huku watoto wa watawaliwa wakiwa wanaishi kwa hofu na unyonge mkubwa na vilio vikubwa . Amani hii ni amani ya watawala kujiuna wao ndio wenye haki ya kuamua na kufanya chochote. Amani hii inafikia kikomo mana kundi kubwa linakuwa halunufaiki na amani hii hasa kiuchumi na kisiasa Mana ni rahisi watu wakavunjiwa nyumba au wakanyanganywa ardhi bila fidia na wakijaribu kudai fidia wanapigwa mabomu na risasi na kukaa kimya. Wafanyakazi wanalipwa mshahara kiduchu ukilinganisha na watwala halafu wakidai kuwa na sisi ni binadamu kama nyie ,wanapigwa risasi na kukaa kimya pawe amani na utulivu. Wananchi wakijaribu kuwaambia basi kama mmeshindwa kutupa Haki zetu pisheni waje wengine wenye uwezo wa kutusililiza , wanapigwa risasi na mabomu.
Mwisho wale maskini wanachoka na kuona hawana cha kupoteza wanaamua kufanya vurugu ili kila mtu aumie na familia yake ipate adha ili litimie lile neno la wahenga ,"Amani haiji ila kwa ncha ya upanga.

Amani inayotokana na Haki inadumu mana ni amani ya Kimungu. Mungu anajiita ni Mungu wa Haki.

Miaka mitano Siprian Musiba ameruhusiwa kuhamasisha chuki, mauaji,uzushi , matusi, ukabila, uhasama na kila aina ya rafu za kisiasa kwa sababu tu ameona fursa ya kulinda biashara yake kupitia amani ya risasi.

Serikali za zenye kusimamia Katiba na Haki za Kila mtu kamwe hawapigani wenyewe kwa wenyewe mana kila mtu anafurahia amani na kupata haki yake.

Mamuunga mkono Shekhe Ponda. Waathirika zaidi wakubwa wa dhulma tangu ukoloni ni Waislam isipokuwa wale tu wenye maslahi ninafsi ndani ya amani ya risasi.
Kukosekana kwa Haki hakuwezi kumuumiza Huseni mwinyi wala Ridhiwani mana wao wana Kila kitu na wanaweza kuhonga na kununua haki yao.

Wote tuhamasishe amani lakini haki ni lazima itendeke. Kwenye uchaguzi.

CCM oneni aibu. Miaka mitano mnapiga kampeni, mmejenga madaraja,mmejilimbikizia mahela na mali chungu nzima, mmesaidiwa na watu wasiojulikana kwa miaka mitano kuwapiga wapinzani ,kuwateka ,kuwaua na kuwajeruhi lakini bado tena mnataka kuiba kura na kupindua matokeo.
Hapo amani kwa kweli itakua sio amani bali ni ubinafsi ambao jata wajukuu wenu watawashangaa watanzania kuwa ilikua ni amani ama ni woga.
 
Na safari hii wakijaribu kuiba kura watakoma, Lissu hataki ujinga, wafadhili/mabeberu nao hawataki ujinga, na wanaomuunga mkono Lissu wote nao hawataki ujinga, CCM itabidi wajue wataibaje hizo kura kwa akili vinginevyo kazi wanayo.
Usisahau kuna vyombo vya dola ambavyo vinalinda maslahi ya Serikali lkn pia kwa kujua au wengine kutokujua, wanalinda pia maslahi ya chama kilichopo madarakani. Nadhani hofu yao ni kutokana na ukweli kuwa hatujawahi kuwa na utawala wa Chama kingine tangu uhuru hivyo majeshi hayaamini wasiyemjua na wengine wanahofu ya kupoteza ugali! Otherwise, majeshi (JWTZ & POLISI) yakiamua kuwaacha wananchi waamue bila kuruhusu uchafu (unajisi) wowote katika tukio zima la upigaji, kuhesabu kura na kutangazwa, basi ndoto ya wananchi wengi ingetimia! Inshaalah!
 
Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo Wanaomuunga Mkono Tundu Lissu wanavyojitokeza na kuzidi kuongezeka.

Mwangalie Sheikh Ponda Issa Ponda alivyotikisa Dodoma leo.

Video hii hapa

====

SHEIKH PONDA: WAISLAMU TUMEKUBALIANA TUTAMPIGIA KURA LISSU

Sheikh Ponda Issa Ponda amesema Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu kushinda kura za urais katika Uchaguzi Mkuu 2020 sio tatizo

Amesema waislamu wote wamekubaliana kumchagua Lissu. Hivyo atashinda tatizo linaweza kuja kwenye suala la kutangazwa

Pia Sheikh Ponda amesema Mungu atashindwa kusikia maombi na sala za watanzania kama hawatamchagua Tundu Lissu kuwa Rais

#JFLeo #JamiiForums #Uchaguzi2020 #TZ2020

View attachment 1603479View attachment 1603480View attachment 1603481

View attachment 1603231
Tufungeni kwa tatu kabla mchanguzi ili Mungu awashulikie wote wenye nia ya kutudhulumu watanzania tukaye mpingia kura Lisu
 
Mwili umenisisimka kwa furaha kubwa na isiyoweza kuelezeka,ccm wameshindwa kumnunua Shekh Ponda. Hakika huyu ni Shekh anayesimamia miiko na maadili ya Uislam na kuyaishi!

Kura zote kwa Lissu!
Acha udini. Huyo Ponda siku zote ni udini tu. Ni siku gani atakubali kuwa Mungu ni wa wote na habagui watoto wake. Kwani Ponda ana hatimiliki ya Waislamu?
 
Huyu ndiye Shehe pekee aliyebaki hapa Tanzania. Ponda ni kiongozi, Ponda ni mtu, Ponda ni mtu jasiri na hana unafiki kama wale walamba viatu vya binadamu.

Sheikh pekee kwako. Kuna wengine pia wanamuona siyo Sheikh pekee. Yaani maelfu ya masheikh TZ unamuona mwanaharakati Ponda, ndiyo Sheikh pekee. Tuliwaona wengi, hata wapiga ramli, lakini ndiyo hivyo!
 
Huyu ndiye Shehe pekee aliyebaki hapa Tanzania. Ponda ni kiongozi, Ponda ni mtu, Ponda ni mtu jasiri na hana unafiki kama wale walamba viatu vya binadamu.
Yule sheikh Mkuu wa Mkoa wa DSM, Bwana ubwabwa Musa, anaswali siku hizi kupitia Yesu na Mohammed. Njaa mbaya sana.
 
Kiujumla waislamu swami hii wamepigwa sana, masheikh wao wengi wako ndani.

Unaweza kuthibitisha hao masheikh waliyo ndani ni wake nani. Au unataka kupandikiza chuki zako za kidini! Toa majina yao kama unasema ukweli! Najua hutatoa kwa sababu hakuna masheikh waliowekwa ndani.
 
Yule sheikh Mkuu wa Mkoa wa DSM, Bwana ubwabwa Musa, anaswali siku hizi kupitia Yesu na Mohammed. Njaa mbaya sana.

Si afadhali anayeswali kupitia Mtume Muhammadi na Yesu kuliko wewe unayeswali kupitia Mtume Muhammadi na Shetani. Shetani haendani na Yesu wala mtume Muhammadi.
 
Kuudanganya moyo ni kosa kubwa, kwani hata viongozi wa dini, nao ni binadamu kama sisi, wanauamuzi mioyoni mwao, nani wamshabikie na nani wasimshabikie, hivyo, Sena kwamba, inawapasa viongozi wote Wa dini hawapaswi kugawika kuhusu vyama, hawapaswi kuegemea chama chochote zaidi ya kuhubiri haki na amani pia kukemea inapobidi

Kwa sababu, dunuiani kila kitu kinawezekana, Watawala wa Dunia wote si wema, kwa kuwa huangalia mambo yao na si ya Mungu

Wachache mno wenye hofu ya Mungu, na huenda tokea utawala ule wa kifalme uliokuwa ukitumika Israeli uishe, tokea hapo, pengine hakujawahi kuwepo mtawala mwenye kutenda kwa hofu na kukubali kuongozwa na Mungu

Fikiri kwa kina, Embu kiongozi yeyote wa kidini, aegemee upande mmoja wa chama, halafu chama hicho kije kianguke kisishike dola, unadhani atakuwa na amani afanyapo kazi zake??

Kalaga bao....
Ponda has always been anti CCM, so him campaigning for Lissu is expected. It is his right to choose who to support and try to convice all Tanzanians to support his candidate of choice. What I do not support or agree with is him calling Muslims to support Lissu. Why Muslims in particular. How about nonMuslims? Should they support Magufuli or Lissu. The best is to leave religion out of this. At the end of the day we want to remain Tanzanians of different beliefs, tribes, regions, gender, age groups etc. That is what matters to us. We do not want Kenyan style politics. Certainly not Middle East style of politics. We do not want that, because we know how costly, in terms of human suffering that type of politics is.
 
Sheikh Ponda kweli amesema kama Lissu hakuchaguliwa, basi Mungu hatapokea Dua za watanzania? Kama ni kweli basi sheikh amekufuru sana, shekh ponda hana uwezo wa kumsemea mungu, na hajui uamuzi wa mungu utakuwaje.

Sijawahi kuona Sheikh mkweli kama Ponda.
 
Back
Top Bottom