Kishindo cha Mbowe chatikisa bunge, Amtaka Waziri mkuu kutoa ufafanuzi juu ya Corona na Tume huru ya uchaguzi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,496
215,354
Mara nyingi sana tumewaasa watu humu jf na kwingineko kwamba usithubutu kushindana na aliyejaaliwa , utaumia !

Watu wengi wamezungumza kuhusu Corona , lakini namna Mh Mbowe alivyouchambua ugonjwa huu ni namna ya kupigiwa mfano , huyu mtu ameshindikana , huyu Mfungwa si wa kawaida .

Hakuna haja ya watu kuona aibu kumsifia .

====
1586234907727.png

Mhe. Spika nashukuru kwa kunipa nafasi kuwa mchangiaji, na mimi nitazungumza mambo mawili tu ya msingi, Mhe Spika mwaka huu au kwa kipindi hiki tunakabiliwa na mambo mawili makubwa sana katika nchi yetu, janga la maambukizi ya virusi vya corona na baadae mwaka huu uchaguzi mkuu, na hayo ni mambo mawili makubwa sana katika Taifa.

Kwanza nizungumze suala la corona, Mhe. Spika mimi nazungumza kama mtu ambae kwa bahati mbaya nime-experience tatizo hili katika familia yangu kwa hiyo nalizungumza kama mtu ambae na uhakika na kitu ninachozungumza ni nini.

Na sababu nilikuwa katika isolation mpaka leo nilivyotoka rasmi Mhe. Spika namshukuru Mungu kwa hilo napenda ni-share na viongozi na wabunge wenzangu kitu ambacho nafikiri pengine hatujakipa uzito wa kutosha katika kukabiliana na janga la corona.

Hili tatizo ni real wala Watanzania wasifikiri ni tatizo linaweza likazuiwa na mipaka ya nchi yetu, kwa hiyo ni wajibu kabisa wa Serikali na wadau wengine wote kushirikiana katika janga hili kuhakikisha jambo hili linapewa uzito unaostahili kama ambavyo mataifa mengine ambayo yame-experience tatizo hili yanavyopitia.

Mhe. Spika mbali na tahadhari mbalimbali ambazo zimetolewa na Serikali na taarifa mbalimbali ambazo zimetolewa na serikali bado kuna uzembe mkubwa sana miongoni mwetu aidha kwa kujua ama kutokujua au kufikiri tatizo liko mbali na haliko mikononi mwetu.

Sasa kwa upande Serikali ningeomba nishauri kitu kimoja, itakuwa ni dhana ya bahati mbaya sana kufikiri jambo hili ni kazi ya serikali peke yake, suala hili ni lazima lishirikishe wadau wote lakini vyovyote itakavyokuwa lazima serikaki ichukue a leading role na nina uhakika serikali ina wajibu wa ku-take a leading role, lakini hili ni suala ambalo linahusu taasisi binafsi, sekta binafsi, mashirika ya umma, nyumba zetu za ibada tunahitaji effort ya kitaifa, na mimi ushauri mkubwa ambao ningependa kutoa katika bunge langu Mhe Spika ni kuunda a national task force ambayo itasimamia masuala yote yanayohusu corona, serikali iongoze hii task force lakini ishirikishe wadau wengine, shirikisha wanazuoni" Mwenyekiti CHADEMA, Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe

Sasa kwa upande Serikali, ningeomba nishauri kitu kimoja, itakuwa ni dhana ya bahati mbaya sana kufikiri jambo hili ni kazi ya serikali peke yake, suala hili ni lazima lishirikishe wadau wote lakini vyovyote itakavyokuwa lazima serikaki ichukue a leading role na nina uhakika serikali ina wajibu wa ku-take a leading role, lakini hili ni suala ambalo linahusu taasisi binafsi, sekta binafsi, mashirika ya umma, nyumba zetu za ibada tunahitaji effort ya kitaifa, na mimi ushauri mkubwa ambao ningependa kutoa katika bunge langu Mhe Spika ni kuunda a national task force ambayo itasimamia masuala yote yanayohusu corona, serikali iongoze hii task force lakini ishirikishe wadau wengine, shirikisha wanazuoni, shirikisha madaktari, mahospitali binafsi , taasisi mbalimbali za nchi ili jambo hili lipewe uzito wa kitaifa na lisiachiwe serikali peke yake kwa sababu serikali ni sehemu ya uongozi lakini kuna wadau wengine huku nje lakini nao wakielimika wanaweza wakajua na kuisadia serikali katika kufikia malengo yake.

Mhe Spika, ili tatizo la corona virus #COVID19TZ ni kubwa sana, na watu wengine mpaka sasa hivi wanaliona kwetu halijawa kubwa kwa sababu pengine halijaingia watu wengi wakaathirika na wakapata maafa, lakini ukweli maafa ya corona yameshaingia katika uchumi wetu Mhe. Spika, na nilitegemea sana katika bajeti ya mwaka huu serikali ingekuja na mpango maalum kabisa kabisa wa kibajeti na kutoa taarifa katika bunge hili kwamba hivi tuna athari kiasi gani zinazotokana na janga la corona lakini ukiangalia mipango ya serikali mpaka sasa hivi lakini sijui itabadilika baadae bado milango ipo kama business as usual, bajeti zipo pale pale, hatuja-forsee kushuka kwa mapato makubwa sana ya serikali.

Kwa mfano sekta ya utalii ambayo ni sekta inayoingiza mapato makubwa ya fedha za kigeni, hii sekta imeanguka kabisa, hii sekta imeanguka kwa 99%, mahoteli yamefungwa, makampuni ya tours yamefungwa, facilities zote za kitalii zimefungwa , mashirika ya ndege ya kitaifa na kimataifa haya-operate na hali hii Mhe. Spika haita-recover baada ya wiki mbili, hili anguko la kibiashara kwenye upande wa utalii impact yake ni mwaka mzima sababu wageni wame-cancel booking mpaka Desemba mpaka new year, kwa hiyo hili sio jambo la leo au kesho ni lazima serikali iweze ku-forsee haya mambo, tunapojadiliana bajeti hapa mpaka sasa hivi katika bajeti za nchi utaona kwa kiwango kikubwa sana utekelezaji wa mipango mingi ya serikali ulikwama njiani kwa sababu ya mapato kuwa kidogo.

Sasa bado tunakwenda kuangusha mapato zaidi, biashara zinaanguka Mhe Spika, Foreign investment sasa hivinzitakuwa almost suspended for almost kwa mwaka mwingine mmoja, misaada kutoka nchi mbalimbali ambazo zilikuwa zinatusaidia na chakika zitapunguza misaada sababu ya hali yao wenyewe katika nchi zao.

Uwekezaji wa ndani umeingia katika mashaka makubwa uagizaji wa bidhaa kutoka nchi za nje ambao unachangia kwa kiwango kikubwa cha mapato ya serikali inaanguka, mashirika na makampuni mengi yatafunga kazi na wafanyakazi watakuwa retreat lakini sijaona hatua hili jambo likichukuliwa hatua na kupewa uzito kwenye bajeti yetu ya nchi.

Sasa kama tunaendelea na kufanya mipango yetu ya bajeti vile vile kama hakuna tatizo lililotokea wakati tuna-expect mapato ya serikali yataweza kupungua almost by 40% katika miezi sita ijayo, tunawezaje kutekeleza bajeti zetu za kiserikali.

Uwekezaji wa ndani umeingia katika mashaka makubwa uagizaji wa bidhaa kutoka nchi za nje ambao unachangia kwa kiwango kikubwa cha mapato ya serikali inaanguka, mashirika na makampuni mengi yatafunga kazi na wafanyakazi watakuwa retreat lakini sijaona hatua hili jambo likichukuliwa hatua na kupewa uzito kwenye bajeti yetu ya nchi.

Sasa kama tunaendelea na kufanya mipango yetu ya bajeti vile vile kama hakuna tatizo lililotokea wakati tuna-expect mapato ya serikali yataweza kupungua almost by 40% katika miezi sita ijayo, tunawezaje kutekeleza bajeti zetu za kiserikali.

Hili ni jambo ambalo Mhe. Spika nilitamani sana Waziri Mkuu atausaidie, Waziri wa fedha atusaidie tuwe na mipango ya pamoja wala tusione aibu katika kukabiliana na janga la corona ni vyema tukajiandaa mapema measures gani zifanyike ili kujaribu kuounguza hili tatizo, inawezekana Mhe. Spika, tukalazimika kuacha baadhi ya miradi yetu mikubwa ambayo tunaipenda, tunaipenda sana tungetamani ikamilike lakini inawezekana kabisa tukashindwa ku-fund miradi hii kwa sababu mapato y serikali ni lazima yatashuka, na kama tunadanganyana mapato ya serikali hayatashuka sio kosa la mtu yoyote ni kosa la ugonjwa huu na ni lazima tukabiliane na hali hiyo.

Wakati huo huo tukichukua tahadhari hizo Mhe Spika, ni lazima tuongeze fungu kubwa la fedha la kwenda kwenye facility mbalimbali zinazotoa huduma kwa wananchi hasa mambo ya kiafya, kuwaambia watu wanawe mikono, tunaona information ambazo ni contradicted, wakuu wa mikoa wanatoa matamko mbalimbali na maelekezo mbalimbali watu waendelee kukusanyika na kufanya kazi, sasa tunajiuliza sasa Serikali mbona inakuwa na kauli mbili mbili, kuna mikusanyiko tunaona haifai , sio ya lazima kwa utaratibu kwa tafsiri ya serikali lakini kuna mikusanyiko ghafla wakuu wa mikoa wao wanafanya majumuiko ya watu wanakusanya watu na kuhutubia watu, wanawaambia watu corona iko mbali, haya ni mambo ya hatari.

Jambo la pili Mhe. Spika, ningependa nizungumze, ni kuhusiana na uchaguzi, actually process za uchaguzi zimeshaanza, lakini ukiangalia tumekuwa tunadai kwa muda mrefu sana, jamani tutengenezeni maridhiano katika nchi, tutengeneze Tume Huru ya Uchaguzi, uchaguzi ni process na hii process ni ndefu, uandikishaji ni sehemu ya process, upatikanaji vifaa ni sehemu ya process, kurekebisha sheria sehemu ambazo zina matatizo ni sehemu ya process, lakini sisi tumekuwa tunadai minimum reform kwa sababu moja tu, kwamba tunaamini ili nchi iweze kuendelea vizuri lazima ipate viongozi wanaopatikana kwa misingi ya kidemokrasia, tunaimani kwamba wawakilishi wa wanachi lazima wapatikane kwa misingi ya kidemokrasia.

Hili jambo linahitaji political will, wala sio kushindana kupiga kelele, mimi nimemuandikia Rais, tumesema mara nyingi, tumezungumza mara nyingi katika forums mbalimbali kwamba jamani tunaposema tunataka minimum reforms marekebisho machache ya sheria kwa sababu mtakumbuka 2015 wakati mchakato wa katiba mpya unashindikana makubaliano na Rais wakati ule Mhe. Jakaya Kikwete yalikuwa angalau twende kwenye minimum reform mpaka tutakapomaliza mchakato mzima katiba bahati mbaya ile process haijarudia mpaka leo.

Kifungu namba 74 na 75 katika katiba yetu kinahitaji marekebisho machache na haya mambo Mhe Spika kama kuna political will upande wa serikali haya mambo yanawezekana tukaenda kwenye uchaguzi watu tumeridhiana tumekubaliana uchaguzi wa haki, akichaguliwa huyu akichaguliwa yule basi tupate viongozi ambao wamepatikana kwa ridhaa ya wananchi na sio kwa ghiliba ya kifumo za kiuchaguzi.

Kifungu namba 75 katika katiba yetu kinahitaji marekebisho machache na haya mambo Mhe. Spika kama kuna political will upande wa serikali haya mambo yanawezekana tukaenda kwenye uchaguzi watu tumeridhiana tumekubaliana uchaguzi wa haki, akichaguliwa huyu, akichaguliwa yule basi tupate viongozi ambao wamepatikana kwa ridhaa ya wananchi na sio kwa ghiliba ya kifumo za kiuchaguzi.

Sasa katiba ina matatizo yake makubwa ambayo marekebisho yake ya kufanya yanayohitaji minimum reform ni michache, kifungu cha 74 na 75 alafu kuna masuala ya sheria za uchaguzi Mhe. Spika , tumeainisha sheria mbalimbali tushapeleka taarifa hizi serikalini kwa Bwana mkubwa mwenyewe kwamba kuna maeneo mbalimbali yana-criminalize process za uchaguzi, kuna watu wengine wanaenguliwa na process ya uchaguzi kwa sababu tu eti amekosea kuweka nukta hapa, vitu kama hivyo ambavyo vinavuruga ile dhana kupata viongozi bora, kwa hiyo tunachosema sisi Mhe Spika ni kwamba tunahitaji hizi minimum reforms zifanyike na nina hakika huo muda tunao hata bunge hili kabla halijaisha Mhe Spika kama kuna willingness, political will ya kutafuta muafaka katika Taifa, kutafuta amani ya kudumu na maridhiano katika taifa haya mambo bado yanaweza kufanyika, sio mambo magumu ya kuhitaji bajeti maalum hapana, ni mambo ambayo yanawezekana.

Tumeaihirisha mambo chungu mzima katika sheria ya uchaguzi na katika katiba ambayo yanafaa kufanyiwa reform ili kuwezesha jambo hili kufanyika ,Asante sana.
 
Hongera mwamba .Ni bora kuwa na wabunge walau mmoja kila mkoa wenye utashi kama wa Mbowe kuliko wapiga meza 300
Na bado kuna watu hawawezi kuelewa ulichoandika hapa!

Na mimi niongeze la kwangu:

Ni bora kuwa na wachangiaji na wasomaji walau kumi humu JF wenye utashi na kujitambua, kuliko wajaza 'likes' 500 kwenye kila mada!

Hapo sasa, nione msisimko kama upo.
 
Erythrocyte, Mbona hakuna jipya alilosema zaidi ya kujitafutia umaarufu. Tangu Rais alipotoa maagizo jinsi ya kukabiliana na mlipuko, hatua kadhaa zimechukuliwa na zinaonesha matokeo mazuri km maambukizi ya ndani kwa ndani bado hayajatokea.

La msingi ni kila mtu, mmoja mmoja, kuzingatia ushauri wa wataalamu. Pia kuhusu anguko la kiuchumi ambalo si jambo la kukurupukia kutafuta tiba yake bila kufanya utafiti wa kina, na tayari Serikali imeunda kikosi kazi.
 
hii hotuba cvm wataikumbuka majanga yakitupata. bunge linaendelea as if corona ni mafua yameipata familia moja hivi
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom