Kisheria, Spika wa Bunge anaweza kuondolewa. Je, Job Ndugai aondolewe?

Spika hata aondolewe bado tatizo litakuwa palepale. Tatizo sio Spika tatizo ni hizo sheria za Bunge zinazompa Spika mamlaka ya kufanya hivo. Huyu hata mkimwondoa atakuja mwingine atafanya hivohivo maana ndio mwongozo wake.

My intake. Tusikomae tu na Spika Wabunge nao wajirekebishe, unajua kuongoza watu wazima ni kazi sana, imagine kila siku wabunge wengine wafanye kama ilivyokuwa kwa Mdee na Bulaya na Spika akae kimya si tutasema Bunge limemshinda? Hebu tuweni neutral tuone mengi

Tatizo si SHERIA za BUNGE tatizo ni Upendeleo unaofanywa na viongozi wa Bunge.
 
Hakuna sababu ya kumuondoa spika kwa sasa. Acheni uchochezi

Sababu ni ikithibitika kanuni , taratibu na sheria zinakiukwa (mtu anaendesha bunge kwa moody, mathalani unanuniana na mwenza hasiraunaleta ofisini, mtoto anafanya vibaya darasani hasira unaleta ofisini!! Sasa ni kifanyike kama sio impeachment!!!!
 
Naona leo bandugu umekuja na hasira.Bunge letu hili sidhani kama ni Bunge kwa mantiki ya chombo cha kuwawakilisha wananchi watanzania.

Sidhani kama ni Bunge maana limeshindwa kuidhibiti Serikali badala yake Serikali imeidhibiti Bunge kwa 100%.Wabunge wamekuwa ni YES sir,wakisubiri wa waponde wapinzani ili wapate teuzi za Uwaziri (unaibu/full).

Wako pale kupiga kelele za kuipongeza serikali ili waweze kesho kupenyeza jamaa,ndugu na marafiki kwenye system ili waweze kupewa nafasi mbalimbali.

In short Shemeji hatuna Bunge ,tuna kitu kinaitwa Bunge lakini si Bunge labda NEC ya CCM au Mkutano Mkuu wa CCM uliobadilishwa jina kuitwa Bunge
Nazingatia hoja zako hizi!.

P
 
Nimeanza homework ya maandalizi ya
Dodoma.

P
Usiogope. Pengine huo ndio utakuwa mwanzo wa mabadiliko makubwa ya Bunge letu kama tulivyokuwa tunapiga kelele hapa jf siku zote.
Twanga bila woga ukijua idadi kubwa ya hao wabunge wanakuunga mkono kwa sababu wao midomo yao imezibwa
 
Wanabodi,
Leo ninazungumzia Kuondolewa kwa Spika wa Bunge la JMT. Kuna watu wanadhani mtu akiishachaguliwa kuwa Spika wa Bunge, basi anageuka mungu mtu, anaweza kufanya lolote na asiguswe!. No!. Nafasi ya Spika ipo kwa mujibu wa Katiba, na atatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni, akikiuka na ikathibitishwa amekiuka, Spika anaondolewa!. Swali ni Jee Spika Mhe. Ndugai amekiuka Katiba, sheria, taratibu na kanuni kustahili Kuondolewa?.
Hili swali kwenye bandiko hili japo ni swali la zamani, lakini sasa liko very valid. Wanasheria tuelimisheni, ili Spika aondolewe madarakani, inambidi mpaka afanye kosa gani?.
P.
 
Mayala Bado ana Kovu La Kukimbiwa Na Mwanamke Aliekuwa anampenda Sana Joyce, Na Joyce Kwa Sasa Anaishi Marekani
Wanabodi,

Niliposema Rais wa JMT anaweza Kuondolewa madarakani na Bunge, wengi walibeza kuwa nilikuwa nazungumzia hypothetical situation, yaani kitu ambacho hakipo, nikauliza hakipo vipi wakati kipo kwenye Katiba yetu?, sema haijatokea tukapata rais wa kulazimika Kuondolewa.

Leo ninazungumzia Kuondolewa kwa Spika wa Bunge la JMT. Kuna watu wanadhani mtu akiishachaguliwa kuwa Spika wa Bunge, basi anageuka mungu mtu, anaweza kufanya lolote na asiguswe!. No!. Nafasi ya Spika ipo kwa mujibu wa Katiba, na atatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni, akikiuka na ikathibitishwa amekiuka, Spika anaondolewa!. Swali ni Jee Spika Mhe. Ndugai amekiuka Katiba, sheria, taratibu na kanuni kustahili Kuondolewa? .

Declaration of interest.

Mimi ni muumini wa Katiba, unauhusisha uendeshaji wa nchi kwa mujibu wa Katiba kwa kutumia sheria, taratibu na kanuni.

Naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kufuatia bandiko hili

Tundu Lissu apinga vikali adhabu ya Mdee na Bulaya,


Tanzania ni nchi inayofuata Katiba kwa kuzingatia misingi ya haki, kuwa "no one is above the law" kumaanisha Katiba ndio the supreme law, hakuna yoyote aliye juu ya Katiba na sheria.

Chini ya Katiba hiyo, tunayo mihimili mitatu, ya Serikali, Bunge na Mahakama ambayo yote inapaswa kuwa huru kwa kutenda bila kuingiliwa na mihimili mingine (independently) lakini wakati huo huo kila mihimili ukiwa na majukumu ya kutenda kwa mujibu wa Katiba, ikitokea mihimili mmoja umekiuka mamlaka yake, then hii mihimili mingine ina jukumu la kuufanyia checks and balance.

Hii inaitwa "the doctrine of separation of powers".

Bunge lina jukumu la kutunga sheria, Mahakama inatafsiri sheria na Serikali inatekeleza sheria.

Serikali inatakiwa kuliwezesha Bunge na Mahakama ikiwemo kulidhibiti Bunge kupitia mamlaka ya rais kuteua mtendaji mkuu wa Bunge ambaye ni katibu wa Bunge.

Serikali inaidhibiti Bunge kwa kuridhia sheria zinazotungwa na Bunge haziwi sheria hadi mkuu wa serikali aridhie, na asiporidhia rais ana mamlaka ya kulivunja Bunge.

Serikali pia inawajibu wa kuihudumia Mahakama kwa kuiwezesha ila pia kulidhibiti kwa kuteua Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Jaji Mkuu lakini haiwezi kumuondoa, ila pia serikali inaidhibiti Mahakama kwa kusaini hati za capital punishment.

Bunge kwa upande wake lina jukumu la kuisimamia Serikali na Mahakama kwanza kwa kuitungia sheria, kupitisha bajeti zao, na kuisimamia matumizi yake.

Serikali inapokosea kwa kukiuka mamlaka yake, inashitakiwa Mahakamani au bungeni, na mkuu wa mihimili huu wa Serikali akienda kinyume cha Katiba, anashitakiwa na Bunge na kufukuzwa kazi kupitia "impeachment process"

Kama serikali inaweza kushitakiwa Mahakamani, Mahakama inashitakiwa Bungeni na Serikalini, Jee Bunge haliwezi kushitakiwa Mahakamani?.

Serikali imewahi kushitakiwa mahakamani mara kibao tuu na ikashindwa. Sina kumbukumbu ya Mahakama kushitakiwa nje ya Mahakama, nakumbuka zile kesi za Mtikila, lakini Bunge la Tanzania halijawahi kushitakiwa mahakamani.

Hii ya Bunge kutokushitakiwa kumemfanya Mkuu wa Mhimili huu Bunge, kujisahau, kujiiunua na kujiona kama mungu mtu hivyo kutaka kuabudiwa, kuigopwa na kunyenyekewa hadi kujiona anaweza kufanya chochote, kusema chochote na kutoa maamuzi yoyote hata yaliyo kinyume cha sheria, taratibu na kanuni na asiguswe!.

Adhabu kwa Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya now goes down to history books za Bunge letu kwa mara ya kwanza kushitakiwa mahakamani if at all kesi itafunguliwa kweli.

Kwa kumbukumbu zangu mtu pekee mwenye kinga ya kisheria ya kutokushitakiwa mahakamani ni Rais wa JMT pekee, hivyo serikali Inashitakika, Mahakama Inashitakika swali ni Jee Bunge nalo pia Linashitakika?!.

Mihimili hii ya dola inaongozwa na binadamu ambao sio malaika na wanaweza kukosea, ikitokea wakuu wa mihimili hii kukosea, sheria imeweka utaratibu wa jinsi ya kumuondoa rais, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge. Swali ni Jee Spika wa Bunge Job Ndugai aondolewe?.

Kwa vile utaratibu wa kumuondoa spika ni kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, kwa vile mimi sio mwanasheria, naomba niwakabidhi kwa mmoja wa wanasheria wetu humu jf,
Mkuu The Learned Brother
Petro E. Mselewa
ili muweze kupata vifungu vya sheria, kanuni na utaratibu was kumuondoa spika .
Spika anaondolewa hivi...


Paskali
Rejea
Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika!

Vurugu za Jana Bungeni: Chanzo ni Mhe. Job Ndugai!- Ni Dikteta Hatari Kuliko Spika Anne Makinda!.

Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of Separation of Powers is it Nothing, Just a Myth? ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki ...
Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi? | Page 15 ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom