Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,483
- 30,155
It is very true.Jamaa anatamani hata ateue mabalozi wa nyumba kumi.
Jamaa ameamua kuendesha nchi kwa staili ya ONE MAN SHOW.
Katiba ya nchi na sheria mbalimbali za nchi zishawekwa kapuni.
Hebu nitoe mifano michache tu ili tupate picha namna gani nchi ambavyo haiendeshwi tena kwa misingi ya sheria.
Jamaa alimpendekeza yule mdada kada mkubwa wa Chama chake akakalie kigoda kule jumba la kutunga sheria kule Dom na kesho yake akapita kwa kishindo kukalia kigoda kule Dom!
Matokeo yake hiko chombo kimeondokana kabisa na kuwa chombo cha kuwakilisha wananchi na badala yake kimegeuka kuwa vikao vya NEC.......
Jamaa akatangaza hadharani kuvipiga marufuku vyama vyote vya siasa vya upinzani visifanye shughuli zozote za siasa hadi 2020,lakini akatoa 'ruksa' kwa chama chake kuendelea kufanya shughuli za kisiasa na Jeshi la Polisi lisiwabughuzi na Jeshi la Polisi limeitii amri hiyo bila kujali kuwa insisigina Katiba ya nchi..........
Tusije shangaa before 2020 jamaa akawa tayari keshairejesha hii nchi kwenye single party system...
Let us wait and see. Kwa Magu anything can happen.