Kisheria mkataba wa Simba na Mo ulishakufa siku nyingi

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,561
KISHERIA MKATABA WA SIMBA NA MO ULISHAKUFA SIKU NYINGI.

Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Katika kesi ya PHOTO PRODUCTION LTD vs SECURICOR TRANSPORT LTD[1980] 1 ALL ER 556 mahakama ilisema kuwa pale ambapo wahusika katika mkataba watakuwa wamekubaliana aidha kwa maandishi ama mdomo kutekeleza jambo fulani na ikawa jambo hilo halikutekelezwa na mmoja wao, basi mkataba huo unakuwa umevunjika

Kwa mujibu wa kipande cha mkataba ambacho kilitolewa na Mwanachama kindakindaki wa Simba Dr. Hamis Kigwangala, sehemu ya masharti ya uwekezaji(Terms of Investment) sharti la 3 na 4 linamtaka mwekezaji aliyeshinda tenda katika simba kuwa na dhamana ya 10% ya Tshs bilioni 20, na ndani ya mwezi mmoja tokea siku ya kusainiwa mkataba awe amelipa kiasi chote cha tshs Bilioni 20 ambazo ni malipo ya hisa alizochukua.

Kwa mujibu wa hayo maamuzi ya mahakama hapo juu ambayo kwetu ni sheria, kama kiasi hicho cha pesa hakijalipwa mpaka sasa na muda wa mwezi mmoja umeshapita tokea mwekezaji asaini basi maana yake mkataba umeshavunjika na hivyo kisheria hakuna mkataba kati yake na Simba.

Kifungu cha 37(1) cha Sura ya 345 Sheria ya Mikataba kinasema kuwa ni lazima kwa kila muhusika katika mkataba kutekeleza ahadi zake. Limetumika neno ni Lazima(must perform).Hakuna uhiari wa kutekeleza ulichoahidi.

Katika kesi ya Edwin Simon Mamuya vs Adam Jona Mbala [1983]TLR 410uk.414, Jaji Rugakingira amesisitiza kuwa mtu anapotoa hakikisho(assurance) la utekelezaji wa jambo fulani basi anabanwa na hakikisho hilo.

Ifahamike wazi kuwa kama ni kweli Kigwangala alivyosema kuwa MO hajatekeleza majukumu yake ya kimkataba ya kulipa Bilioni 20, basi kwa mujibu wa Sheria huo Mkataba ulishajifia tangu Mwezi mmoja ulipopita bila kulipa hiyo bilioni 20.

Kwa lugha rahisi hakuna mkataba kati ya MO na Simba. Na kama kuna vitu kama usajili, mishahara,matunzo nk. ambavyo MO anatoa ama anaendelea kutoa kwa Simba basi kisheria hizo ni zawadi(gifts) na si majukumu ya kimkataba kwasababu mkataba haupo tena.

Kitu anachotakiwa kufanya MO sasa hivi ama kufanyishwa na wanachama wa Simba ni kuilipa Simba fidia kubwa kwa kuvunja mkataba.

Mahakama ya rufaa katika kesi ya Stanbic Tanzania Ltd vs Abercrombie&Kent(T) Limited, Civil Appeal No. 2/2001 imesema kuwa mvunja mkataba anatakiwa kulipa fidia. Anamlipa yule aliyevunjiwa.

Uongozi wa Simba una mamlaka ya kumtaka alipe fidia. Ama uongozi kama hauna ubavu huo pengine nao unafaidika kwa kinachoendelea basi sheria inamruhusu mwanachama yeyote hai kuhoji mahakamani uhalali wa mkataba na mwekezaji na kuomba fidia ikiwa ni pamoja kujitoa kwa mwekezaji.

Narudia tena kuwa ni mwanachama yeyote hai na halali ana haki hii, hata yule aliyeko Omurushaka huko mbali mpakani mwa Tanzania.

Hii ni kwasababu kila mwanachama hai ana maslahi na Club na sheria inaruhusu kila mwenye maslah(interest) kuchukua hatua ikiwemo kuomba msaada mahakamani au vyombo vingine.

Tuelewane vizuri, hapa tunaongelea sheria sio propaganda kwahiyo mwenye hoja kinzani naye aeleze sheria inasemaje na si vinginevyo.Zile hoja za sisi tunataka matokeo tu,au sijui wanataka kutuvuruga,au sijui hawa yanga nk. hazina nafasi hapa.Njoo na sheria mjomba.

Moja ya athari za kisheria za kutokuwepo mkataba halali ni kuwa klabu haina bodi. Kwasababu uhalali wa mkataba ndio ungezalisha mwenyekiti halali wa bodi.Kama mkataba uliomleta mwenyekiti wa bodi haupo basi na mwenyekiti wa bodi hayupo, na bodi yenyewe haipo.

Kwahiyo klabu inaendeshwa bila bodi bali kikundi cha watu. Kwenye mapinduzi tunasema serikali inaongozwa na baraza la uongozi kama ilivyo Libya.

Kuna mtu akaniambia kwamba huenda ndiyo maana MO hupenda mara kwa mara kutishia kujitoa Simba akikosewa au kuudhiwa, pengine anajua kuwa habanwi kwasababu mkataba haupo. Mi sijui hayo ni mawazo tu ya mdau.

Huyu nae mdau mwingine hapa ananiambia kuwa kuna masharti Simba haijatekeleza ndio maana MO naye hatoi 20b.

Sawa, nini hicho ambacho Simba haijatekeleza?. Mbona hakiko wazi. Mbona akihojiwa kuhusu 20b hakisemi hicho kitu ili lawama zitoke kwake ziende Simba?.

Na je mkataba unasema hivyo kwa uwazi kuwa Simba isipofanya hivi na yeye asiilipe 20b au sharti hilo limekuja baadae(after though).

Na kama ni hivyo kuwa Simba haijafanya na ndio maana MO naye hajafanya basi hoja hii ya Ufu(death) wa mkataba inapata nguvu Zaidi kuwa mkataba ulishakufa tangu zamani kwa pande zote mbili kutotekeleza majukumu ya mkataba.

Anyway,kubwa ni kuwa, kama jamaa hajalipa 20b kama Kingwangala alivosema basi SIMBA haina mkataba na Mo na MO hana mkataba na SIMBA. MO anabaki kuwa mhisani tu ndani ya Simba.
 
Kigwangala ana hoja tuache siasa aisee muda mwingine sisi wabongo sisi tunakwama Sana.
 
Mkataba umewahi kuuona au umesikiliza tu upande wa Kigwangala then ukapenda tujadili kwa upande huo zaidi?

Mimi ninavyoona kuna mambo upande wenye Hisa 51 haujayatekeleza ndiyo maana mengi hayaendi ilivyotakiwa na hata Mo mwenyewe alishasema kuna michakato haijakamilika Bilion 20 ni pesa kidogo kwa yeye kuitoa.Hilo la pesa anazotoa sasa kuwa zawadi analifahamu vema sana
 
Simba haijafanya uhakiki wa wanachama ambao watakuwa wanahisa wa 51% hivyo Mo hawezi shirikiana na watu asie wajua
 
Tatizo washabiki na wanachama wengi wa Simba uelewa wao kuhusu hisa na mikataba ni mdogo ndio maana mo anawapelekesha lakini si tu bodi haina uhalali lakini bodi ilishavunja katiba kwa sababu inaendeshwa bila mwenyekiti wa simba ambaye alijiuzulu muda na hawajaitisha uchaguzi pamoja na kutakiwa kufanya hivyo
 
KISHERIA MKATABA WA SIMBA NA MO ULISHAKUFA SIKU NYINGI.

Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Katika kesi ya PHOTO PRODUCTION LTD vs SECURICOR TRANSPORT LTD[1980] 1 ALL ER 556 mahakama ilisema kuwa pale ambapo wahusika katika mkataba watakuwa wamekubaliana aidha kwa maandishi ama mdomo kutekeleza jambo fulani na ikawa jambo hilo halikutekelezwa na mmoja wao, basi mkataba huo unakuwa umevunjika

Kwa mujibu wa kipande cha mkataba ambacho kilitolewa na Mwanachama kindakindaki wa Simba Dr. Hamis Kigwangala, sehemu ya masharti ya uwekezaji(Terms of Investment) sharti la 3 na 4 linamtaka mwekezaji aliyeshinda tenda katika simba kuwa na dhamana ya 10% ya Tshs bilioni 20, na ndani ya mwezi mmoja tokea siku ya kusainiwa mkataba awe amelipa kiasi chote cha tshs Bilioni 20 ambazo ni malipo ya hisa alizochukua.

Kwa mujibu wa hayo maamuzi ya mahakama hapo juu ambayo kwetu ni sheria, kama kiasi hicho cha pesa hakijalipwa mpaka sasa na muda wa mwezi mmoja umeshapita tokea mwekezaji asaini basi maana yake mkataba umeshavunjika na hivyo kisheria hakuna mkataba kati yake na Simba.

Kifungu cha 37(1) cha Sura ya 345 Sheria ya Mikataba kinasema kuwa ni lazima kwa kila muhusika katika mkataba kutekeleza ahadi zake. Limetumika neno ni Lazima(must perform).Hakuna uhiari wa kutekeleza ulichoahidi.

Katika kesi ya Edwin Simon Mamuya vs Adam Jona Mbala [1983]TLR 410uk.414, Jaji Rugakingira amesisitiza kuwa mtu anapotoa hakikisho(assurance) la utekelezaji wa jambo fulani basi anabanwa na hakikisho hilo.

Ifahamike wazi kuwa kama ni kweli Kigwangala alivyosema kuwa MO hajatekeleza majukumu yake ya kimkataba ya kulipa Bilioni 20, basi kwa mujibu wa Sheria huo Mkataba ulishajifia tangu Mwezi mmoja ulipopita bila kulipa hiyo bilioni 20.

Kwa lugha rahisi hakuna mkataba kati ya MO na Simba. Na kama kuna vitu kama usajili, mishahara,matunzo nk. ambavyo MO anatoa ama anaendelea kutoa kwa Simba basi kisheria hizo ni zawadi(gifts) na si majukumu ya kimkataba kwasababu mkataba haupo tena.

Kitu anachotakiwa kufanya MO sasa hivi ama kufanyishwa na wanachama wa Simba ni kuilipa Simba fidia kubwa kwa kuvunja mkataba.

Mahakama ya rufaa katika kesi ya Stanbic Tanzania Ltd vs Abercrombie&Kent(T) Limited, Civil Appeal No. 2/2001 imesema kuwa mvunja mkataba anatakiwa kulipa fidia. Anamlipa yule aliyevunjiwa.

Uongozi wa Simba una mamlaka ya kumtaka alipe fidia. Ama uongozi kama hauna ubavu huo pengine nao unafaidika kwa kinachoendelea basi sheria inamruhusu mwanachama yeyote hai kuhoji mahakamani uhalali wa mkataba na mwekezaji na kuomba fidia ikiwa ni pamoja kujitoa kwa mwekezaji.

Narudia tena kuwa ni mwanachama yeyote hai na halali ana haki hii, hata yule aliyeko Omurushaka huko mbali mpakani mwa Tanzania.

Hii ni kwasababu kila mwanachama hai ana maslahi na Club na sheria inaruhusu kila mwenye maslah(interest) kuchukua hatua ikiwemo kuomba msaada mahakamani au vyombo vingine.

Tuelewane vizuri, hapa tunaongelea sheria sio propaganda kwahiyo mwenye hoja kinzani naye aeleze sheria inasemaje na si vinginevyo.Zile hoja za sisi tunataka matokeo tu,au sijui wanataka kutuvuruga,au sijui hawa yanga nk. hazina nafasi hapa.Njoo na sheria mjomba.

Moja ya athari za kisheria za kutokuwepo mkataba halali ni kuwa klabu haina bodi. Kwasababu uhalali wa mkataba ndio ungezalisha mwenyekiti halali wa bodi.Kama mkataba uliomleta mwenyekiti wa bodi haupo basi na mwenyekiti wa bodi hayupo, na bodi yenyewe haipo.

Kwahiyo klabu inaendeshwa bila bodi bali kikundi cha watu. Kwenye mapinduzi tunasema serikali inaongozwa na baraza la uongozi kama ilivyo Libya.

Kuna mtu akaniambia kwamba huenda ndiyo maana MO hupenda mara kwa mara kutishia kujitoa Simba akikosewa au kuudhiwa, pengine anajua kuwa habanwi kwasababu mkataba haupo. Mi sijui hayo ni mawazo tu ya mdau.

Huyu nae mdau mwingine hapa ananiambia kuwa kuna masharti Simba haijatekeleza ndio maana MO naye hatoi 20b.

Sawa, nini hicho ambacho Simba haijatekeleza?. Mbona hakiko wazi. Mbona akihojiwa kuhusu 20b hakisemi hicho kitu ili lawama zitoke kwake ziende Simba?.

Na je mkataba unasema hivyo kwa uwazi kuwa Simba isipofanya hivi na yeye asiilipe 20b au sharti hilo limekuja baadae(after though).

Na kama ni hivyo kuwa Simba haijafanya na ndio maana MO naye hajafanya basi hoja hii ya Ufu(death) wa mkataba inapata nguvu Zaidi kuwa mkataba ulishakufa tangu zamani kwa pande zote mbili kutotekeleza majukumu ya mkataba.

Anyway,kubwa ni kuwa, kama jamaa hajalipa 20b kama Kingwangala alivosema basi SIMBA haina mkataba na Mo na MO hana mkataba na SIMBA. MO anabaki kuwa mhisani tu ndani ya Simba.
Usisahau kuwa ili mkataba uidhinishwe na asasi yenye bodi ya wadhanini ni lazima rita watoe kibali,sasa rita hawajatoa kibali hicho,mkataba utakuwa sio kwamba haujaga bali hata haujaanza
 
Wakili kuna tofauti kubwa kati ya direct interest na interest, hakuna shabiki yoyote wa simba ambae ana locus standi ya kumshitaki Mo isipokua bodi ya wazamini ya simba, nikukumbushe swala ilo ni pure civil litigation so sio criminal et kila mwenye interest katika jamii akawa na locus standi.

Sheria ulizozi cite na cases ni irrelevant ktk ilo swala, coz zilikua proposed na ku point watu au makampuni so ni matter of individuality na ndio maana hauja leta kesi ata moja au sheria ata moja ambayo inaendana na ili swala la simba licha ya wewe kufanya juhudi binafsi kuleta hadi reported case za england.

So umekurukupa ukashindwa kujua nature of the problem huku ukisahau iv ni vitu viwili tofauti.

Wakili Soma
 
KISHERIA MKATABA WA SIMBA NA MO ULISHAKUFA SIKU NYINGI.

Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Katika kesi ya PHOTO PRODUCTION LTD vs SECURICOR TRANSPORT LTD[1980] 1 ALL ER 556 mahakama ilisema kuwa pale ambapo wahusika katika mkataba watakuwa wamekubaliana aidha kwa maandishi ama mdomo kutekeleza jambo fulani na ikawa jambo hilo halikutekelezwa na mmoja wao, basi mkataba huo unakuwa umevunjika

Kwa mujibu wa kipande cha mkataba ambacho kilitolewa na Mwanachama kindakindaki wa Simba Dr. Hamis Kigwangala, sehemu ya masharti ya uwekezaji(Terms of Investment) sharti la 3 na 4 linamtaka mwekezaji aliyeshinda tenda katika simba kuwa na dhamana ya 10% ya Tshs bilioni 20, na ndani ya mwezi mmoja tokea siku ya kusainiwa mkataba awe amelipa kiasi chote cha tshs Bilioni 20 ambazo ni malipo ya hisa alizochukua.

Kwa mujibu wa hayo maamuzi ya mahakama hapo juu ambayo kwetu ni sheria, kama kiasi hicho cha pesa hakijalipwa mpaka sasa na muda wa mwezi mmoja umeshapita tokea mwekezaji asaini basi maana yake mkataba umeshavunjika na hivyo kisheria hakuna mkataba kati yake na Simba.

Kifungu cha 37(1) cha Sura ya 345 Sheria ya Mikataba kinasema kuwa ni lazima kwa kila muhusika katika mkataba kutekeleza ahadi zake. Limetumika neno ni Lazima(must perform).Hakuna uhiari wa kutekeleza ulichoahidi.

Katika kesi ya Edwin Simon Mamuya vs Adam Jona Mbala [1983]TLR 410uk.414, Jaji Rugakingira amesisitiza kuwa mtu anapotoa hakikisho(assurance) la utekelezaji wa jambo fulani basi anabanwa na hakikisho hilo.

Ifahamike wazi kuwa kama ni kweli Kigwangala alivyosema kuwa MO hajatekeleza majukumu yake ya kimkataba ya kulipa Bilioni 20, basi kwa mujibu wa Sheria huo Mkataba ulishajifia tangu Mwezi mmoja ulipopita bila kulipa hiyo bilioni 20.

Kwa lugha rahisi hakuna mkataba kati ya MO na Simba. Na kama kuna vitu kama usajili, mishahara,matunzo nk. ambavyo MO anatoa ama anaendelea kutoa kwa Simba basi kisheria hizo ni zawadi(gifts) na si majukumu ya kimkataba kwasababu mkataba haupo tena.

Kitu anachotakiwa kufanya MO sasa hivi ama kufanyishwa na wanachama wa Simba ni kuilipa Simba fidia kubwa kwa kuvunja mkataba.

Mahakama ya rufaa katika kesi ya Stanbic Tanzania Ltd vs Abercrombie&Kent(T) Limited, Civil Appeal No. 2/2001 imesema kuwa mvunja mkataba anatakiwa kulipa fidia. Anamlipa yule aliyevunjiwa.

Uongozi wa Simba una mamlaka ya kumtaka alipe fidia. Ama uongozi kama hauna ubavu huo pengine nao unafaidika kwa kinachoendelea basi sheria inamruhusu mwanachama yeyote hai kuhoji mahakamani uhalali wa mkataba na mwekezaji na kuomba fidia ikiwa ni pamoja kujitoa kwa mwekezaji.

Narudia tena kuwa ni mwanachama yeyote hai na halali ana haki hii, hata yule aliyeko Omurushaka huko mbali mpakani mwa Tanzania.

Hii ni kwasababu kila mwanachama hai ana maslahi na Club na sheria inaruhusu kila mwenye maslah(interest) kuchukua hatua ikiwemo kuomba msaada mahakamani au vyombo vingine.

Tuelewane vizuri, hapa tunaongelea sheria sio propaganda kwahiyo mwenye hoja kinzani naye aeleze sheria inasemaje na si vinginevyo.Zile hoja za sisi tunataka matokeo tu,au sijui wanataka kutuvuruga,au sijui hawa yanga nk. hazina nafasi hapa.Njoo na sheria mjomba.

Moja ya athari za kisheria za kutokuwepo mkataba halali ni kuwa klabu haina bodi. Kwasababu uhalali wa mkataba ndio ungezalisha mwenyekiti halali wa bodi.Kama mkataba uliomleta mwenyekiti wa bodi haupo basi na mwenyekiti wa bodi hayupo, na bodi yenyewe haipo.

Kwahiyo klabu inaendeshwa bila bodi bali kikundi cha watu. Kwenye mapinduzi tunasema serikali inaongozwa na baraza la uongozi kama ilivyo Libya.

Kuna mtu akaniambia kwamba huenda ndiyo maana MO hupenda mara kwa mara kutishia kujitoa Simba akikosewa au kuudhiwa, pengine anajua kuwa habanwi kwasababu mkataba haupo. Mi sijui hayo ni mawazo tu ya mdau.

Huyu nae mdau mwingine hapa ananiambia kuwa kuna masharti Simba haijatekeleza ndio maana MO naye hatoi 20b.

Sawa, nini hicho ambacho Simba haijatekeleza?. Mbona hakiko wazi. Mbona akihojiwa kuhusu 20b hakisemi hicho kitu ili lawama zitoke kwake ziende Simba?.

Na je mkataba unasema hivyo kwa uwazi kuwa Simba isipofanya hivi na yeye asiilipe 20b au sharti hilo limekuja baadae(after though).

Na kama ni hivyo kuwa Simba haijafanya na ndio maana MO naye hajafanya basi hoja hii ya Ufu(death) wa mkataba inapata nguvu Zaidi kuwa mkataba ulishakufa tangu zamani kwa pande zote mbili kutotekeleza majukumu ya mkataba.

Anyway,kubwa ni kuwa, kama jamaa hajalipa 20b kama Kingwangala alivosema basi SIMBA haina mkataba na Mo na MO hana mkataba na SIMBA. MO anabaki kuwa mhisani tu ndani ya Simba.

Ikitokea Mwanachama wa Simba mmoja kwenda Mahakamani.

Mo ataangukia Pua vibaya sana
 
Back
Top Bottom