Kisheria, Mdee na wenzake bado ni wabunge halali kwa tiketi ya CHADEMA

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Chama kikishamvua uanachama mbunge hatua inayofuata ni kulitaarifu bunge juu ya uamuzi huo na Spika akisharidhika anaiandikia tume kuwa nafasi husika iwazi ili tume ya uchaguzi ifanye utaratibu wa kujaza.

Lakini hebu tujiulize utaratibu upoje? CHADEMA iliwavua ubunge akina Mdee na wenzake na ikawapa muda wa wao kukata rufaa,

Je, katika muda huo wa kukata rufaa je CHADEMA ilitakiwa/ilishalitaarifu bunge? Kisheria si sahihi kulitaarifu bunge kwa sababu chama hakijamalizana nao bali lazima kisubiri mpaka muda kiliowapa kukata rufaa upite Kama hawajakata rufaa ndiyo kimtaarifu Spika juu ya uamuzi wao.

Baadaye Mdee na wenzake walikata rufaa kupinga uamuzi huo wa chama Baraza kuu la chama.

Swali: je, wamepoteza ubunge baada ya kukata rufaa na rufaa yao haijasikilizwa? Kisheria ni hapana, chama hakipaswi kimtaarifu Spika kabla hakijasikiliza rufaa yao maana wakimtaarifu Spika akina Mdeee watapoteza ubunge sasa kutakuwa na haja gani ya kusikiliza rufaa ya uanachama wa mtu ambaye mshatekeleza hukumu yake?

Je, mkishamtaarifu Spika akamvua ubunge halafu Baraza kuuu likabaini hawana kosa na waliapishwa bungeni kihalali mtakuwa na uwezo wa kuwarudishia ubunge?

Hivyo kisheria mpaka sasa akina Mdee ni wabunge halali wa Bunge la JMT kwa tiketi ya chama cha CHADEMA, na hii ngoma ninavyoiona ikitoka Baraza kuu break ya kwanza ni mahakamani kuchukua ubunge wa Mahakama.
 
Tulia we bibi; watu wanakufa ni balaa!! Jikite kuokoa maisha ya watanzania acha siasa njaa...!! Usipochukua hatua ngonjwa hili linakwenda kukuumbua vibaya saaana!!
 
Hata Lowasa hakusikilizwa na kamati ya Mwakyembe aisee.
Hiyo kamati haikumvua ubunge wake wala uanachama wake wa ccm. Uwaziri mkuu ni cheo tu unachopewa na rais ambaye anaweza kukunyang'anya wakati wo wote kwa sababu yo yote au hata bila sababu ye yote na kumteua mtanzania mwingine ye yote wakati wo wote. Hata wewe anaweza kukuteua kuwa waziri mkuu hata kama wewe ni mwanachadema.

Kamati ya Mwakyembe ilichofanya ni kumshauri rais, Kikwete wakati huo, amtoe Lowassa kwenye nafasi hiyo ya uwaziri mkuu. Kabla hata ushauri huo haujamfikia rais Lowassa aliamua kujiuzuru uwaziri mkuu. Aliendelea kuwa mbunge wa Monduli na mwanachama wa ccm.
 
Hiyo kamati haikumvua ubunge wake wala uanachama wake wa ccm. Uwaziri mkuu ni cheo tu unachopewa na rais ambaye anaweza kukunyang'anya wakati wo wote kwa sababu yo yote au hata bila sababu ye yote na kumteua mtanzania mwingine ye yote wakati wo wote. Hata wewe anaweza kukuteua kuwa waziri mkuu hata kama wewe ni mwanachadema. Kamati ya Mwakyembe ilichofanya ni kumshauri rais, Kikwete wakati huo, amtoe Lowassa kwenye nafasi hiyo ya uwaziri mkuu. Kabla hata ushauri huo haujamfikia rais Lowassa aliamua kujiuzuru uwaziri mkuu. Aliendelea kuwa mbunge wa Longido na mwanachama wa ccm.
longindo ipi ?
 
Chama kikishamvua uanachama mbunge hatua inayofuata ni kulitaarifu bunge juu ya uamuzi huo na Spika akisharidhika anaiandikia tume kuwa nafasi husika iwazi ili tume ya uchaguzi ifanye utaratibu wa kujaza.

Lakini hebu tujiulize utaratibu upoje? CHADEMA iliwavua ubunge akina Mdee na wenzake na ikawapa muda wa wao kukata rufaa,

Je, katika muda huo wa kukata rufaa je CHADEMA ilitakiwa/ilishalitaarifu bunge? Kisheria si sahihi kulitaarifu bunge kwa sababu chama hakijamalizana nao bali lazima kisubiri mpaka muda kiliowapa kukata rufaa upite Kama hawajakata rufaa ndiyo kimtaarifu Spika juu ya uamuzi wao.

Baadaye Mdee na wenzake walikata rufaa kupinga uamuzi huo wa chama Baraza kuu la chama.

Swali: je, wamepoteza ubunge baada ya kukata rufaa na rufaa yao haijasikilizwa? Kisheria ni hapana, chama hakipaswi kimtaarifu Spika kabla hakijasikiliza rufaa yao maana wakimtaarifu Spika akina Mdeee watapoteza ubunge sasa kutakuwa na haja gani ya kusikiliza rufaa ya uanachama wa mtu ambaye mshatekeleza hukumu yake?

Je, mkishamtaarifu Spika akamvua ubunge halafu Baraza kuuu likabaini hawana kosa na waliapishwa bungeni kihalali mtakuwa na uwezo wa kuwarudishia ubunge?

Hivyo kisheria mpaka sasa akina Mdee ni wabunge halali wa Bunge la JMT kwa tiketi ya chama cha CHADEMA, na hii ngoma ninavyoiona ikitoka Baraza kuu break ya kwanza ni mahakamani kuchukua ubunge wa Mahakama.
Aya yako ya kwanza tu inakinzana na kichwa cha mada. Lini Chadema iliwahi kuwateua uliowataja kuwa wawakilishi wa chama chao bungeni? Kama haikuwahi kuwateua kama chama kinavyodai kinawezaje kufanya hayo mengiiiiiii iliyoelezwa???!!!!
 
Makamanda bhana, mwenzao kasema anajenga arguments zake kisheria, wao badala ya kuja na zao za kisheria pia, wanakuja na povu, porojo na matusi. Maskini chadema!
 
Back
Top Bottom