Kisheria, kifo cha Rais hutakiwa kuombolezwa siku 21 na sio siku 14

Makosa sio ya Rais wetu mteule bali wale walioandaa ile taarifa. Hapa ndio tujue wapo wapotosha katiba kwa maslahi yao nyuma ya pazia.
R.I.P JPM
... wachukuliwe hatua kali mara moja iwe fundisho kwa wajinga wengine waliokalia ofisi za umma bila kujua wajibu wao! Ona sasa, hotuba ya kwanza tu tangu awe de facto President tayari wamempotosha!

Mama Samia awe makini sana na hawa watu ikiwezekana kwenye issue muhimu za kitaifa has to seek different opinion hata kwa upinzani badala ya haya MATAGA.
 
NYIE WENYEW KISHERIA mlitakiwa muwe jela mnatulimia mashamba wanaume wapambanaji, umehitimu chuo unazurura mtaani unakaa kwa ndug unajaza choo, then unakuja kusema ilitakiwa ziwe siku 21 sio 14. Mngekua na kaz za kufanya msingekaa kuona vitu vidogo ni big deal. Vijana jishughurishen otherwise mtaolewa
 
Aliyoandika hapo siyo Katiba bali Ni Sheria ya Mazishi ya Viongozi wa Kitaifa Sura ya 419 ndiyo inayoeleza hivyo katika kifungu cha 8 kama kilivyooneshwa post #1.

View attachment 1728474

RE: 2010 mjasiriamali sio mtu mzuri.

Mkuu kasome ammendments za hii Act then tuendelee, hii Revised Edition 2010 ni yakubumba imejumlisha ammendments kurahisisha maisha ya wasomi ila sio official kiivyo.
 
RE: 2010 mjasiriamali sio mtu mzuri.

Mkuu kasome ammendments za hii Act then tuendelee, hii Revised Edition 2010 ni yakubumba imejumlisha ammendments kurahisisha maisha ya wasomi ila sio official kiivyo.
Imejumlisha Ammendments za uongo?
 
Nawaza mama Samia alivyopata hii taarifa atakuwa alistuka sana. Akili yake itakuwa ilisimama kwa muda dah.
watakuwa walimficha hali halisi ya mgonjwa.... kwa hiyo yeye kama sisi tu wakamshtukiza Mzee kaondoka duniani - ndiyo maana kwenye tangazo hakuwa sawa !!
 
watakuwa walimficha hali halisi ya mgonjwa.... kwa hiyo yeye kama sisi tu wakamshtukiza Mzee kaondoka duniani - ndiyo maana kwenye tangazo haku sawa !!
Ila ikumbukwe sasa anakwenda kuwa Rais, anatakiwa ku-act ki-rais
 
Uko sahihi kabisa aliyetangaza kifo cha Rais Magufuli amemchukulia kama kwamba alikuwa Makamu wa Rais hili ni kosa kubwa sana kisheria, ni dharau iliyokithiri.
The Tanzanian Leaders Funeral Acts, 2006 stipulate as follows:

7. The President shall, as soon as possible after receiving official
infonnation and confinnation from an authorized medical officer ofthe
death of a national leader -
(a) deliver official announcement on the death of the national
leader, date and time ofdeath and cause of death;
(b) convene a meeting ofthe Cabinet; and
(c) announce-
(i) in the case of a retired President, a period of 7 days for
state mourning and the flags to fly half mast;
ii) in the case of a serving Vice-President the period of 14
days for state mourning and the flags to fly half mast;
(iii) in the case of retired Vice-President a period of 7 days
for state mourning and the flags to fly half mast; and
(iv) in the case of -
(aa) a serving Prime Minister, a period of 7 days;
(bb) a retired Prime Minister, a period of 5 days, for
state mourning and the flag to fly half mast.
8. -(1) Where the President who is in office dies, the Vice President
shall, after receiving official infonnation and confinnation ofthe death,
deliver death announcement in the manner stipulated under section 7.
(2) The Vice President shall, in respect of the late President,

announce a period of21 days for mourning and the flag to fly halfmast.

NB: Kama makosa yameanza kufanyika mapema hivi kuna hatari huko tuendako yakatenedeka mambo mengi yaliyo kinyume na sheria

Katiba (Article 37 subart 5 na kuendelea hadi subart 10 pamoja na sheria ya mazishi ya viongozi wa kitaifa, wastaafu na wengine wenye heshima serikalini, umma vimetoa mwongozo vizuri sana kuhusiana na masuala haya sijui kwanini taratibu zinakiukwa?
Shukrani kwa Elimu nzuri.
 
Imejumlisha Ammendments za uongo?

Hapana ila hauwezi cite kama RE: 2010 sio proper. Pia inawezekana ikajumlisha ammendments sizo sababu zipo CPC na MCA za kubumba zenye ammendments za uongo hasa hii ya RE 2019 ina toleo la Mjasiriamali.

Ngumu kuelewa ila kama ni wakili au mwana LST utanielewa.
 
Tuchapeni kazi kumuenzi. Alisema "hapa kazi tu" sasa mwezi mzima watu wakae waomboleze? Tena wafanye wamzike haraka maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom