Kisheria, kifo cha Rais hutakiwa kuombolezwa siku 21 na sio siku 14

Nov 28, 2020
12
45
Muacheni huyu mama amechanganyikiwa atarekebisha baadae maana hapo najua kichwa kimejam, kuongoza nchi sio mchezo bora uwe msaidizi, ila sasa maamuzi yatakuwa juu yake🙏🏿🙏🏿
 

Mpandisha mishahara

JF-Expert Member
Mar 1, 2014
1,541
2,000
Poleni TAIFA LETU kwa kupoteza kiongozi wetu! MUNGU ampe pumziko la milele, niende kwenye mada! Ni kwanini tuomboleze siku 14 badala ya siku 21? Katiba imezungumziaje hili?
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,400
2,000
Huu msiba umenigusa kupita maelezo
Ni jambo la kawaida kutegeana na namna ulivyokuwa karibu na marehemu. Na wakati umeguswa kupita maelezo na huo msiba, kuna Watanzania wenzako baadhi wamekesha bar jana usiku kufurahia hilo tukio la kuhuzunisha.

Hayo ndiyo maisha.
 

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
1,563
2,000
Sheria ya mazishi ya viongozi inasema, endapo Rais aliyekuwa madarakani akifariki dunia, na baada ya Makamu wa Rais kupata taarifa rasmi zilizothibishwa atatakiwa kutangaza kifo kwa mujibu wa taratibu.

Sheria inamtaka Makamu wa Rais atangaze maombolezo ya siku 21 ambapo bendera itapepea nusu mlingoti kuonesha heshima kwa Rais aliyeaga dunia.

Uko sahihi kabisa aliyetangaza kifo cha Rais Magufuli amemchukulia kama kwamba alikuwa Makamu wa Rais hili ni kosa kubwa sana kisheria, ni dharau iliyokithiri.
The Tanzanian Leaders Funeral Acts, 2006 stipulate as follows:

7. The President shall, as soon as possible after receiving official
infonnation and confinnation from an authorized medical officer ofthe
death of a national leader -
(a) deliver official announcement on the death of the national
leader, date and time ofdeath and cause of death;
(b) convene a meeting ofthe Cabinet; and
(c) announce-
(i) in the case of a retired President, a period of 7 days for
state mourning and the flags to fly half mast;
ii) in the case of a serving Vice-President the period of 14
days for state mourning and the flags to fly half mast;
(iii) in the case of retired Vice-President a period of 7 days
for state mourning and the flags to fly half mast; and
(iv) in the case of -
(aa) a serving Prime Minister, a period of 7 days;
(bb) a retired Prime Minister, a period of 5 days, for
state mourning and the flag to fly half mast.
8. -(1) Where the President who is in office dies, the Vice President
shall, after receiving official infonnation and confinnation ofthe death,
deliver death announcement in the manner stipulated under section 7.
(2) The Vice President shall, in respect of the late President,

announce a period of21 days for mourning and the flag to fly halfmast.

NB: Kama makosa yameanza kufanyika mapema hivi kuna hatari huko tuendako yakatenedeka mambo mengi yaliyo kinyume na sheria

Katiba (Article 37 subart 5 na kuendelea hadi subart 10 pamoja na sheria ya mazishi ya viongozi wa kitaifa, wastaafu na wengine wenye heshima serikalini, umma vimetoa mwongozo vizuri sana kuhusiana na masuala haya sijui kwanini taratibu zinakiukwa?
 

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,730
2,000
Watarekebisha tu. Human error.
Na hili wanapaswa kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo, Samia, atangaze kuongeza siku za maombolezo vinginevyo Watanzania watanza kuhoji uwezo wake wa ku-react inapotokea maswala ya kufanyia kazi kwa haraka kama haya.
 

nkumbison

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
1,931
2,000
Siku saba za mwanzo walishaomboleza waliokua nae hizi 14 ndio zetu wananchi.... kwani taharifa za uwezekano wa kuwa hatunae tumeanza kuzipata lini? Siku 7 hazifiki?

Binafsi naona sawa tuu!! Kwani katiba inafuatwa vizuri awamu hii?
 

Albaab

JF-Expert Member
Jun 6, 2015
1,009
2,000
Sheria ya mazishi ya viongozi inasema, endapo Rais aliyekuwa madarakani akifariki dunia, na baada ya Makamu wa Rais kupata taarifa rasmi zilizothibishwa atatakiwa kutangaza kifo kwa mujibu wa taratibu.

Sheria inamtaka Makamu wa Rais atangaze maombolezo ya siku 21 ambapo bendera itapepea nusu mlingoti kuonesha heshima kwa Rais aliyeaga dunia.

Huu utamaduni wa kutokufuata sheria ameanzisha nani?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom