Kisheria ipoje endapo Shilole atataka talaka watagawana mali walizochuma pamoja? Au hii ipo kwa akina mama tu kudai mali

Naona mtungi wa gesi umelipuka...

Hizi sheria za Ovyo zilitungwa kwa mihemko duniani ndizo zinazosababisha vijana wasioe.
 
Mwanamke anapoachika au kupewa talaka kisheria ipo hivi

(1) Una Haki Na Mali Mlizochuma Pamoja; Hiki ni kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kukifahamu, kuwa kama mkewe una haki ya kila mali mlizochuma pamoja, mali hizi ni zile za kuhamishika na ambazo si zakuhamishika...
Mwanaume kulilia mgao wa mali hasa kujidai umezichuma wewe na mkeo nao ni upumbavu, mwanaume unaweza tafuta hata mali nyingine baada ya kuachana
 
Wakigawana Mali ni aibu sana kwa mwanaume. Pride ya mwanaume itaondoka kabisa.
 
Mwanaume anamrithi awe amemuacha au amekufa, kwetu ilitokea anti alikuwa nesi akaolewa na mwanaume ila akamkuta ameshajenga na ana viwanja, anti kafa mwanaume anadai mali, watoto wakasema hzi mali ni za mama wakaenda mahakaman jamaa akapata urithi, hata kwenye uislam mwanaume anamrith mkewe
 
Mwanaume kulilia mgao wa mali hasa kujidai umezichuma wewe na mkeo nao ni upumbavu, mwanaume unaweza tafuta hata mali nyingine baada ya kuachana

Chief, inategemea kama bado kijana na nguvu unazo unaweza kutafuta mali nyingine ila wakati mwingine mnaachana umri umeenda, halafu pia inategemea na aina ya mali mfano kama mmenunua kitanda na godoro pamoja, mkiachana unaweza kupotezea lakini kama mlifungua mashamba ya mabilioni eti umuachie ukaanze upya, hiyo ni ngumu kwa kweli.
 
Wewe bwana mdogo wacha kupiga makelele mitandaoni!...
Unakifahamu kisa cha mfalume JUHA? Basi Ndio wewe. Sema chochote, kosoa, changia, fafanua etc. Bora yeye kajitahidi kumsaidia mleta mada. Wewe unabwabwaja tu.

Unajua mazingira za sehemu za periphery ambako unaweza kijiji kizima Hamna mtu anayeelewa hayo ma law chambers yenu? What about the legal fees?
 
Unakifahamu kisa cha mfalume JUHA? Basi Ndio wewe. Sema chochote, kosoa, changia, fafanua etc. Bora yeye kajitahidi kumsaidia mleta mada. Wewe unabwabwaja tu. Unajua mazingira za sehemu za periphery ambako unaweza kijiji kizima Hamna mtu anayeelewa hayo ma law chambers yenu? What about the legal fees?
Point, sio kila MTU ana access na professionalz
 
Chief, inategemea kama bado kijana na nguvu unazo unaweza kutafuta mali nyingine ila wakati mwingine mnaachana umri umeenda, halafu pia inategemea na aina ya mali mfano kama mmenunua kitanda na godoro pamoja, mkiachana unaweza kupotezea lakini kama mlifungua mashamba ya mabilioni eti umuachie ukaanze upya, hiyo ni ngumu kwa kweli.
Ni ngumu kwanini iwe ngumu, tusiendekeze sana tamaa ya mali chief, unamuachia tu na isitoshe utafutaji wa mwanaume na mwanamke hutofautiana mwanaume anaweza kuparangana tu, ni vyema unamuachia tu mbona mali tunakufa tunaziacha ni nini kisumbue sasa kichwa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ya kuishi ‘nyumba moja’ kama wanandoa kwa miaka miwili mfululizo, vipi hizi nyumba za kupanga tunaohama kila kukicha!!!
Mimi nauliza kama hawajafunga ndoa na mwanamke aneshapata mimba na haijafika miaka miwili alafu mume amemuacha mke hapo haki ya mke ikoje?
 
Mwanamke anapoachika au kupewa talaka kisheria ipo hivi...
Siku hizi ndoa zote migogoro inaenda ustawi wa jamii ilikupata tiketi ya kwenda mahakamani ili kudai mali,swali hapa ni je mke akiwa muajiliwa na mume sio muajiliwa sasa hapo watagawana pia mshiko uliopo bank kama zao la mke?
 
Mimi nataka kujua hizi Mali ambazo zimepatikana kabla ya ndoa,mfano hai kwangu Mimi kabla ya kuoa nilinunua viwanja vitatu, kimoja katikati ya mji viwili nje kidogo hicho Cha katikati ya mji wife anakijua Ila hivyo viwili havijui hajawahi kufika, kwenye hiki kiwanja Cha karibu nikajenga nyumba na ikafika wenye lenta nikashindwa kuimaliza nikaiacha,nikakaa Kama miaka kiwili nikaoa ndoa ya kanisani kabisa na kwa Sasa ndoa Ina mwaka na nusu na tuna mtoto wa miezi nane.

Sasa kule kwenye kiwanja nilichojenga nyumba ilibaki nafasi kubwa baada ya kuoa nikaona nijenge nyumba ndogo ili tukae tuachane na kero za kupanga,ujenzi ukaanza na Sasa iko hatua ya kuezeka na bati nilipewa Kama zawadi ya wanakamati ya harusi yangu, kimbembe kimekuja wakati huu ndani ya nyumba kumeibuka mgogoro unaohatarisha kuisambalatishia mbali ndoa hii,..

najiuliza endapo tutaachana italazimu kumgawia Mali zangu hizi nilizochuma mwenyewe?

Au Kuna namna nyingine ya kugawana hizi mali?

Msaada tafadhari.
 
Hapana mkuu kisheria kuanza kwa kifupi huyo mwanamnke hana justice wala relief yo-yote hata atakapokwenda mahakaman nikwamba kuna mkataba ambao tunaita(prenature Aggrement)ambao unausika ktk ndoa linapokuja swala la especially Mali mkataba huo unakupa haki ya kubaki nazo Mali zako ambazo ulizichuma wew mwenyewe before marriage na kubaki nazo pekee wew mwenyew kama mmiliki.

Halali wa hizo mali kwaiyo uyo mwanamke hatakuwa na nguvu wala mamlaka yoyote yakutaka mmgawane mali ambazo hajui ulizipata kwa nguvu gan ispokuwa kama mlijenga pamoja ukitoa izo Mali ulizonazo kabla ya kufunga nae ndoa ndio atakuwa na haki ya kudai mahakaman na sio izo Mali ambazo umezitafuta wew mwenyewe,usiogope mkuu,
 
Manaswara mna tamaa na shida sana.Wengi huingia kwenye ndoa kwa lengo la Mali.
 
Basi hawa wafanyakazi wa ndani wanaobebeshwa majukumu ya mke yaani kulea, kusafisha, kufua na Mengineyo naona wepewe option ya kupokea iyo 30,000 kwa mwezi àu kugawana mali.. hahahahaha
 
Hahaa shukrani sana chief nitajitahidi kujizoesha majina hayo japo kibongo bongo majina hayo nimageni sana nani aghalabu kukuta sehemu wanatumia majina hayo naukikuta basi hao ni full mabasi yanjano
Kama kiingereza ni taab bas tumia kiswahili tu.... nephew/niece= MWALIMU
 
Nina swali kidogo hapo kwenye mali ambazo si za wanandoa,umeandika maswala ya mirathi ,je endapo nimerithi fedha taslim ambazo zilikua kwenye account ya mzazi wangu kabla hajafariki nikatumia fedha hizo kujenga kwenye kiwanja changu ambacho nilikinunua kabla ya kuingia kwenye ndoa,je hiyo nyumba itakua ni mali ya wanandoa ?

Kumbuka ninajenga wakati nipo kwenye ndoa kwa fedha za mirathi ila pia kiwanja nilikipata kabla ya kuingia kwenye ndoa,jinsia yangu ni Ke.
 
Back
Top Bottom