Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 14,501
- 26,997
Nimewaza tu, wala msinipuuze!
Pengine ni hizi changamoto za ajira, au pengine ni katika kuwaza uwekezaji ‘nje ya boksi’ kama tunavyohubiriwa. Basi nimepata kuwaza hii kama fursa, tupeane taratibu na miongozo ya kisheria.
Kama ilivyo kwenye huduma zingine za kijamii, mfano Afya, Elimu, Usafirishaji, Mawasiliano n.k kuna mashirika ya serikali na binafsi.
Na hata kwenye ulinzi kuna majeshi ya serikali na vikosi vya kampuni binafsi, lengo ni lile lile kutoa huduma katika ubora unaokidhi viwango tarajiwa.
Basi nimewaza upande wa magereza (jela), tunaweza kuwa na uwekezaji katika sekta hii (Private Prisons). Lengo ni kuleta ushindani na kuboresha huduma, mradi tupate miongozo kuhusu vigezo vya kuzingatia.
Kuhusu i namna kwa gani tutanufaika, hili linabaki siri kwa sasa. Itoshe tu kusema tutajiendesha kama asasi zingine zisizo za kiserikali, hivyo tutajipatia ujiko kutoka kwa wahisani!
Tutapokea wafungwa kutokana na hukumu halali za kimahakama zetu, pia tutakuwa na wanasheria ili kutoa msaada kwa wahitaji, wateja wetu pamoja na wengine.
Hii itasaidia kujenga ufahamu juu uraia, na kujiepusha na uvunjifu wa sheria.
Gereza ni kwa ajili ya kurekebisha tabia, hivyo pamoja na huduma bora kwa wafungwa ni lazima tuzingatie lengo mahsusi la uwepo wake.
Wafungwa watafundishwa kazi za uzalishaji kipindi watumikiapo vifungo vyao, hii itasaidia kuwapatia kipato cha kuendesha maisha na familia zao zisizo na hatia wakati na hata baada ya kifungo.
Wasalaamu,
Ncha Kali.