Kisheria hili la huyu traffic na daladala likoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisheria hili la huyu traffic na daladala likoje?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Soki, Aug 3, 2011.

 1. S

  Soki JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Leo tukio hili lilitokea mahali fulani Dar es salaam.Traffic police anasimamisha daladala. Anachomoa ufunguo wa gari. Anakagua mambo kadhaa kama leseni, bima nk. Gari inakutwa na makosa. Anaambiwa apaki pembeni. Dereva anaambiwa awapandishe abiria wake katika gari nyingine ili wamalizie safari yao. dereva anasema hana hela. Abiria wanamwendea trafiic kumwambia mbona wanapotezewa muda? Anasema 'mmesikia jinsi dreva alivyosema, kwamba hana hela sasa mimi nifanyeje'.

  Hivi kisheria hasa hapa ikoje?
   
 2. Aloysius

  Aloysius Member

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Gari ikiwa na tatizo maana haina uwezo wa kubeba abiria. Kama dereva amepakia watu kwenye gari bovu basi amevunja makubaliano kati yake na abiria wake, hivyo traffic alikuwa sahihi kumnyooshea dereva kidole. Narudia: Trafic akiliona gari linatatizo linakosa uwezo wakukubeba. Mfano hana lesseni; Inatia shaka kama ni dereva kweli, akigonga au akipindua gari nani wakulaumiwa? Tusaidie serikali kutokomeza makosa na sio kumezea makosa mate.
   
Loading...