Kisheria, hata asiye na Cheti cha Ndoa anaweza kufumania

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,561
Sio kweli kama Waziri Simbachewene alivyosema kuwa asiye na cheti cha ndoa hawezi kufumania.

Yeyote mwenye ndoa halali anaweza kufumania. Na ndoa halali imetajwa Kifungu cha 9 cha Sheria ya Ndoa na hapo cheti hakikutajwa.

Kuwa na mahusiano nje ya ndoa ni kosa kwa mujibu wa Kifungu cha 72 Sheria ya Ndoa na hivyo kufumania ni Haki aliyonayo Mwanandoa ili kupata ushahidi wa kosa hilo.

Kwahiyo yeyote mwenye ndoa awe na cheti au bila cheti anaweza kufumania. Suala la msingi ni awe na ndoa tu.

Na ndoa zenyewe tulizonazo ni ndoa za kidini, ndoa za kimila(Customary Marriage), ndoa za serikali(Civil Marriage), na ndoa inayotokana na kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili(Presumed Martiage) Kifungu 160.

Hawa wote katika ndoa hizi wana ndoa halali na wana haki ya kufumania.

Kama kweli uhalali wa ndoa ingekuwa cheti basi asilimia 80 ya Watanzania tungesema hawana ndoa.

Cheti kwa mujibu wa Sheria ni ithibati tu lakini hakitengenezi wala kuharibu uwepo wa ndoa halali na haki zake. Kwa hiyo tusipotoshane.
 
Ngoja awadanganye kipindi mtu anapakwa Vaseline waziri yeye atakuwa kwenye liV8 anaelekea ziarani makao makuu,yaani mtu apate fumanio la mke/mume akakimbilie cheti kwanza home.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom