Kisheria Halima Mdee na wenzake wamepoteza ubunge baada ya kukata Rufaa Chadema badala ya kwenda mahakamani!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,898
141,836
Mzee Mgaya anasema kitendo cha Halima Mdee na wenzake kukata rufaa Baraza kuu la Chadema kinaashiria kuwa kwa sasa wao siyo wanachama wa Chadema na hivyo wanaiomba kamati kuu iwarejeshee uanachama wao. Na kwa mujibu wa sheria mbunge ni lazima awe mwanachama wa chama cha siasa.

Mgaya anasisitiza kuwa mahali sahihi walipostahili kukimbilia akina Bulaya ni mahakamani ambako wangesimamisha maamuzi ya kamati kuu ya Chadema.

Mimi sijamuelewa mzee Mgaya aliyemwelewa ufafanuzi Tafadhali.

Hapa tupo kisheria siyo kiitikadi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mzee Mgaya anasema kitendo cha Halima Mdee na wenzake kukata rufaa Baraza kuu la Chadema kinaashiria kuwa kwa sasa wao siyo wanachama wa Chadema na hivyo wanaiomba kamati kuu iwarejeshee uanachama wao...
Mzee Mgaya aache kuropoka ropoka.

Kwani hao wanaoyafanya haya si ndio hao waliotunga hizi sheria?
Mzee atulie. Watu wapo kazini
 
Huyo mzee wako anataka maamuzi ya Kamati Kuu yasimamishwe kivipi wakati kamati kuu ni chombo halali cha maamuzi ndani ya chama chao?

Hajui hata kama kina Mdee wakikimbilia mahakamanI bado watapoteza uanachama wao kwasababu katiba ya Chadema inazuia mwanachama wao kwenda mahakamani?

Huyo mzee wako sasa atakupoteza.
 
Siku hizi kuna makanjanja wengi kweli kweli. Wengine nao wanajifanya wanasheria (vishoka-uchwara).

Mahakama sio choo kwamba unafika tu na kutapika unachoweza.

Kuna protocal na procedures.

Na procedure muhimu ni kwamba ili kupata Judicial reciew lazima uwe umepitia mchakato wote wa ndani ya chama!

You have internal remedies in the party! Pursue those.
 
Mzee Mgaya anasema kitendo cha Halima Mdee na wenzake kukata rufaa Baraza kuu la Chadema kinaashiria kuwa kwa sasa wao siyo wanachama wa Chadema na hivyo wanaiomba kamati kuu iwarejeshee uanachama wao....
Kama Mwambe alijiunga CCM na hakupoteza ubunge ndio itakuwa hao Covid19? Wanatupotezea muda tu waendelee na kilichowapeleka ikifika 2025 wakapumzike kwa amani.
 
Kwani tangia kamati kuu iwafukuze walikuwa wanaendelea kuwa wanachama? Lakini si wamendelea kuwa wabunge?
 
Mzee Mgaya anasema kitendo cha Halima Mdee na wenzake kukata rufaa Baraza kuu la Chadema kinaashiria kuwa kwa sasa wao siyo wanachama wa Chadema na hivyo wanaiomba kamati kuu iwarejeshee uanachama wao...
Huyo mzee Mgaya ndo nani na ameitendea nini nchi hii? Huyo siyo authority ya kufanyia marejeo.
 
Mzee Mgaya anachemka tu. Hawa wamekata rufaa. Technically uamuzi wa kuwafukuza haujakuwa ratified.

Hata Professeri Lipumba aliwahi kutumia loophole kama hii kujirudisha kundini.
 
Back
Top Bottom