Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 7,697
- 12,878
Habari wana JF
Leo naomba kuongelea au kuliwekea ufafanuzi jambo moja ambalo limekuwa likielezwa vibaya au kimakosa na watu wengi wengine wakiwa ni viongozi hadi wa kiserikali.
Suala hilo ni swala la je, ni ndoa kiserikali baada ya kuishi na mwanamke au mwanaume nyumba moja kama wapenzi?
Hili suala hata huku sio geni wapo waliolielezea ama kwenye uzi kamili au komenti katika uzi.
Jibu kwa swali hili ni kuwa HAKUNA NDOA kisa mmeishi nyumba moja na mwanaume au mwanamke kwa miezi sita au zaidi. Ndio HAKUNA NDOA.
Hili linaweza likakushitua kwani umeshawahi kusikia na hata kuaminishwa na viongozi wa kiserikali kama ustawi au dawati la jinsia na hata baadhi ya wabunge bungeni kwa nyakati tofauti (inashangaza sana).
Jambo ambalo huwa lipo baada ya kuishi kimahusiano katika nyumba moja kwa miezi sita au zaidi ni UWEPO WA FIKIRIO LA NDOA hii sio ndoa bali ni fikirio tu na fikirio hili halina nguvu ya ndoa.
Kwanini ni FIKIRIO LA NDOA na sio NDOA?, jibu ni rahisi kabisa. Swala hili ni fikirio kwani sio ndoa na kwavile watu hao wanaishi pamoja basi hujengeka fikra kuwa pengine wataoana.
Fikirio hili limewekwa mahususi kwa ajili ya kumlinda hasa mwanamke kwani mwanamke akiishi na mwanaume kwa muda huu kisha mwanaume akaoa mwanamke mwingine basi mwanamke huyu anao uwezo wa kushitaki na kudai fidia kwa kupotezewa muda (japo wote wanaweza kuwa wamepotezeana muda)
Fikiro hili la ndoa kamwe haliwezi kufanya kazi kama ndoa na mwanamke au mwanaume aliyepo kwenye hadhi ya FIKIRIO LA NDOA hawezi kudai maslahi ya ndoa hata mara moja akafanikiwa Mahakamani.
Sasa tupate ufahamu juu ya jambo ambalo huonesha uwepo wa ndoa halali.
Ndoa yoyote ili iwe ndoa halali Tanzania ni sharti.iwe imesajiliwa kwa msajili wa ndoa na kupewa cheti cha ndoa cha serikali, hapa nisisitize sio cheti cha kanisa lako au msikiti wako ni cheti cha serikali. Upo mtindo wa sasa unakuta taasisi ya kidini ina cheti chao hasa makanisa ya kiroho, rafiki hapa kuwa makini sana hakikisha unapata cheti cha serikali.
Ndoa ili iwe halali ni sharti ifungishwe na mtu aliyepewa mamlaka ya kufungisha ndoa. Hapa tufahamu kuwa sio kila kiongozo wa kidini anao uwezo wa kufungisha ndoa halali, hakikisha anayefungisha ndoa yenu anayo hayo mamlaka.
Kwa vile uzi huu sio kwa ajili ya kupima uhalali wa ndoa kisheria basi itoshe kuishia hapo juu ya swala hili.
Turudi kwenye jambo litakalokuonesha kuwa hapa kuna ndoa.
Kitu kitakachokuonesha na kuthibitisha uwepo wa ndoa kama nilivyosema ni cheti halali cha ndoa cha serikali.
Hivyo hata ndoa za kimila zinapaswa kusajiliwa kwa msajili wa ndoa mara baada ya kufungwa.
Kuna kasumba imejitokeza watu waliosogezana wakaanza kuishi pamoja kujiita wapo kwenye ndoa ya kimila, hakuna ndoa ya kimila ya hivyo na watu hao sio wana ndoa hata wakiishi miaka 20 pamoja.
Mwisho kabisa ndoa haiwi ndoa kwa muda mlioishi pamoja bali ndoa huwa ndoa baada ya kusajiliwa kwa msajili wa ndoa.
Ahsanteni na mafikirio mema ya hali zenu.