Kisasi cha Iran kinakuja, Israel wajiandae kisaikolojia

Jamani kuna taarifa imetoka katibu wa cha kikundi cha kigaidi cha hezbollah amehamia Iran baada ya kuuawa mwanasayansi wa Iran amejua na yeye atafuata
 
Iran naikubali iko vizuri sana , lakini swali langu wanafail wapi kuwalinda wanasayansi wao maana huyu atakua kama wa 5 kuuawa je hawawezi kabisa kuwalinda hawa wataalamu, ushauri wangu kama hawawezi kuwalinda wawalete Tanzania tutawapa hata hirizi
 
Kipigo sio kuua watu kipigo ni kitendo cha israel kotolewa lebanon bila kupenda hivi uliuona mji wa haifa ulivyo haribiwa na makombora vifuru vitatu viliharibiwa pia vifar zaidi ya miatatu vilipata uharibifu kidogo pia meli moja ya kijeshi ilizamishwa kilikuwa kipigo hatari kuwahi kutokea kwa kweli
Acha uongo punguza mahaba kuna mimba za ukubwani
 
Mkuu sina shaka Wairan watalipiza kisasi na uwezo huo wanao sana, labda kama Viongozi wa Mataifa ya Ulaya watawaomba Wairan wasitishe mpago wao wa kulipiza kisasi - watawambia kuuwawa kwa mwana sayansi wao ni mpago wa Israel na Pompeo/Trump wenye lengo la kumuwekea wakati mgumu utawala wa Biden ili usifanukiwe kuwa na uelewano mzuri baina ya Iran, mataifa ya Ulaya na Merikani kuhusu suala udhibiti wa vinu vya nuklia vya Iran.

Biden amekwisha sema kwamba at a heshimu makubaliano yaliyo wahi kufikiwa na Iran,Mataifa ya Ulaya na utawala wa Obama (USA) mambo yalikuwa shwari kabisa, aliye kuja kuvuruga kila kitu alikuwa ni Trump na Pompeo kutokana na shinikizo kubwa la waziri mkuu wa Israel (Natenyahu), Trump kaweka kapuni makubaliano baina ya Iran, Obama na wenzake wa Ulaya - Trump aliwadhalilisha kweli kweli, si hilo tu Trum vile vile aliendelea kuiwekea vikwazo vya kiuchumi chungu nzima Iran na kuisema sema vibaya Kimataifa.

Suala la Iran naona Biden ataliweka sawa maanake he knows kwamba kuuwawa kwa mwasayansi wa Iran lilikuwa na lengo draw a wedge between Iran and European leaders and USA ili makubaliano yasifufuliwe tena Biden atakapo ingia white house come January.
Mkuu ni takribani miaka miwili sasa tunakaribia wa tatu vipi Iran wamefanikiwa kulipiza kisasi kwa Israel?!

Na mwaka huu pia wamefanya assassinations huko Tehran na hakuna jibu lolote toka Tehran
 
Kiongozi Muadhamu: Watieni adabu waliofanya na kuamrisha jinai ya kuuliwa kigaidi shahid Fakhrizadeh

Nov 28, 2020 09:42 UTC

[https://media]

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametilia mkazo wajibu wa kutiwa adabu na kupewa adhabu isiyoepukika wote waliofanya na kuamrisha mauaji ya kigaidi ya mwanasayansi wa Kiirani, Dk. Mohsen Fakhrizadeh.

Mapema leo asubuhi, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe wa pongezi na tanzia kufuatia kuuawa shahidi na kumpoteza mwanasayansi bingwa aliyebobea katika masuala ya nyuklia na ulinzi wa Iran, Dk Mohsen Fakhrizadeh na amesisitiza kutolewa adhabu isiyoepukika kwa waliofanya na walioamrisha jinai hiyo na wajibu wa kuendelezwa jitihada za kielimu na kiufundi za shahid Fakhrizadeh.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema katika ujumbe wake huo kwamba: Mwanasayansi huyu bingwa wa nyuklia na masuala ya ulinzi ambaye ameuliwa shahidi na mamluki watenda jinai na wenye nyoyo ngumu, ametoa roho yake azizi na yenye thamani kubwa katika njia ya Allah kupitia jitihada zake kubwa za kielimu na za kubakia milele na hivyo amefanikiwa kupata daraja ya juu ya kuuawa shahidi ikiwa ni zawadi kutoka kwa Mola wake.

Mohsen Fakhrizadeh, Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu la Wizara ya Ulinzi ya Iran aliuawa shahidi jana jioni katika shambulio la kigaidi lililofanywa katika viunga vya jiji la Tehran.

My take:Kitu wanajeshi wa US walifanywa kwenye zile bases za Iraq sasa kwa israel nadhani wajiandae kwa kulengwa kwa watu wao muhimu sana.Wazee wa visasi washaanza kazi waajemi kwa visasi wanajulikana vizuri tu

View attachment 1637597
hata siku moja haitatokea sikio kutikisa kichwa.Muarabu kapewa sheria moja tuu." muheshimu musirael na mmarekani ili upate heri na maisha marefu duniani".
 
Back
Top Bottom