Kisarawe, Pwani: DC Nikki wa Pili atoa hatimiliki za kimila kwa Ranchi 24

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,149
27,165
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Nikki wa Pili jana amefanya jambo kubwa sana la kutoa hati miliki za kimila kwa ranchi 24 kwa wafugaji katika kijiji cha mafizi kwa ajili ya malisho ya mifugo 17920.

Lengo ni kuondoa migogoro ya ardhi, kuboresha huduma za mifugo, uvunaji wa bidhaa zitokanazo na mifugo,kukusanya kodi,kutunza mazingira na mazao ya wakulima.

Hilo nj Jambo la kuigwa Sana na kupigiwa mifano, hakika kazi inafanyika sana nchi hii.

Mama Samia kanyaga twende, shikilia hapohapo.

Kazi iendelee #kisarawe mpya#

20210626_134047.jpg
 
Hongera kwa jambo zuri hilo, linaweza kupunguza sana migogoro ardhi baina ya wafugaji na wakulima.

ANGALIZO.
Ni vyema DC mpya wa Kisarawe akaachana na hizi promo za mitandaoni, mwisho wake huwa ni mbaya. Ajifunze kwa waliomtangulia. Aache makeke, achape kazi.
 
Kumradhi, mkuu wewe ni chawa wa nikki wa pili ama ni nikki mwenyewe!?
Kwa haraka haraka nimeona si chini ya nyuzi tano umeanzisha za kumhusu niki wa pili.
 
Humu mtandaoni hakuna watu?
 
Kumradhi, mkuu wewe ni chawa wa nikki wa pili ama ni nikki mwenyewe!?
Kwa haraka haraka nimeona si chini ya nyuzi tano umeanzisha za kumhusu niki wa pili.
Kabla sijakujibu hebu sema kwanza wewe ni nani?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom