Mother Confessor
JF-Expert Member
- Jan 7, 2016
- 18,596
- 45,225
- Thread starter
- #121
Em weka picha basii...kha!!
Em weka picha basii...kha!!
Mmh...
Kama upo mjini kanunue super market,kwenye kupika fuatisha maelekezo niliyoyatoa,.Nakitamani sana sa sijui nakipataje
kinaitwaje kwa lugha ya malkia.Kama upo mjini kanunue super market,kwenye kupika fuatisha maelekezo niliyoyatoa,.
Kweli,...wamama wamepumzika kuumia makwapa kwa kutwanga,.
Neno gani mkuu??
Ngoja huyu anisaidie Mshana Jr
Sio vibaya lakini ukipata muda ukakitwanga mwenyewe fresh,.ili kuepuka kula kilichopoteza uhalisia wake,.Tatizo sio kuumia mkuu. Tatizo ni muda. Maisha yamekua kasi sana usipoangalia unakosa Musa wa kutosha kufanya maisha kuwa bora. Kama kuna kitu kinafupisha process bila kuathiri quality ni kheri tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Unajihisije??
Apa wengine hawali kisamvu ujue.. njoo kimya kimya uone bwanaaaMmh...
Sasa nikupe mbinu ya Vitamins.. , huwa unasukumia na Kahawa (coffee changu) 3 cups !! Weeeenakinai mapema sana nikila kitu chenye sukari au mafuta mengi hata hiyo haluwa inanishindaga mafuta
watu wa zenji ndo mafundi wa hiyo kitu
hapa nikianza kusema vitu nisivyopenda kula mwisho utaniuliza nakulaga nini, ok kiufupi sipendi vitu vinavyonikaraisha mdomoni kahawa ya uchungu sipendi pia labda zile tamu tamuSasa nikupe mbinu ya Vitamins.. , huwa unasukumia na Kahawa (coffee changu) 3 cups !! Weeee
Wakurya mna hasira hadi na vyakula..lol,....ungepita tuu kimyakimya
Mamboo wapenzi wa mahanjam,mambo matam matam ya jikoni,mambo ya chakula kizuuuri chenye ladha isiyo chosha.....Asalam Alaykhum,.
Leo nataka tujifunze mboga hii jinsi ya kuitengeneza na kuipika,.kisamvu ni moja ya mboga za majani na ni maarufu sana kwa nchi zetu za Africa na hata baadhi ya nchi za ulaya hutumia pia kama mboga ya majani,.YES kisamvu kina utam wake waliowahi kula mboga hii wanaelewa hasa kikiwa kimepikika kwelikweli kikapikika,.aisee ni kitam sanaaa
Basi tupike mboga yetu hii ya kisamvu; kwanza utachuma kisamvu chako kitekekiteke (mimi nimekipanda kwangu)utakichambua kwa kutenganisha jani la kisamvu na kikonyo,utaweka kwenye kinu chako kisafi, kisha utamenya kitunguu saumu na utakiweka kwenye kinu pamoja na kisamvu (wengine huweka na tangawizi)japo si lazima sana,.ukitwangia kitunguu saumu kinafanya kisamvu chako kinukie vizuri.
Twanga kisamvu na kitunguu saumu mpaka kilainike sana,tumia kinu kikubwa na kipana kwa sababu kisamvu kikianza kulainika huruka-ruka na kumwagika....kikisha lainika kitoe kwenye kinu kiweke kwenye sufuria pana,weka maji kwenye kinu kisuuze vizuri hayo maji yaweke kwenye sufuria lenye kisamvu chako tayari kwa kuweka jikoni kichemke,.wakati huu unaweza kuchanganya na kunde mbichi vikachemka pamoja,..
Kisamvu chako kikishaiva pamoja na kunde (kama utatumia,sio lazima sana kuweka kunde japo huvutia zaidi)epua hakikisha kimeiva na hakina majimaji mengi(kiwe kimekauka kidogo)weka sufuria nyingine kavu jikoni,ikipata moto weka mafuta ya kupikia kiasi na wakati huu unakuwa umekuna nazi yako iliyokomaa vizuri na kuichuja matui mawili jepesi na zito (tui bubu)au utatumia tui la karanga..
Mafuta yakipata moto weka kitunguu maji kikaange mpaka kiwe cha rangi ya brown,weka kisamvu chako kikaange pamoja na kitunguu mpaka viingiliane,halafu weka tui lako jepesi acha vichemke kwa dk 5-6 ukiwa umefunika,baada ya hapo punguza moto kidogo halafu weka karoti iliyokatwa katwa vipande vya wastani pamoja na chumvi na pilipili mbuzi kama utapenda,geuza kwa pamoja halafu weka tui zito na uache kichemke taratibu kwa dk 4-5...
Epua kisamvu chako na kitakuwa tayari kwa kuliwa,mboga hii unaweza kula kwa ugali,wali,ndizi,makande na hata chapati ukipenda,.
Mpaka wakati mwingine babaaiina weekend njema!!!
Ewaaaaah,.kisamvu kitamm jomonii hasa kikilala😋Hiki kisamvu ukikipatia na wali wa nazi daku daaah