Kisa nguo ya ndani, bosi ampa kisago kizito msaidizi wa ndani(House girl)

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,436
house-girl-1.jpg
MFANYAKAZI wa ndani (hausigeli) aliyefa-hamika kwa jina la Katalina John anayefanya kazi hizo kwa Lyina John (30) mkazi wa Mhongolo wilayani Kahama, mkoani Shinyanga amejikuta akichezea kichapo kizito kutoka kwa bosi wake huyo kisa kikidaiwa ni sababu mbalimbali ikiwemo ya kutovaa nguo ya ndani.

Akizungumza katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Mhongolo, Maziku Mbusili, binti huyo alisema bosi wake alimshushia kipigo hicho baada ya yeye kufagia vibaya nje na ndani ya nyumba.

Alisema alipokuwa anaanza kumpiga kwa kosa hilo ndipo bosi wake huyo alipogundua kuwa hakuwa amevaa nguo ya ndani ndiyo alipozidi kumshushia kipigo.
“Alianza kunifokea kuwa sijafagia vizuri uwanja, nguo ya ndani, akaanza kunipiga na alipogundua kuwa sijavaa nguo ya ndani, alizidi kunishushia kipigo kikali hadi kunipasua kidole changu cha mkononi,” alisema binti huyo.
house-girl-3.jpg
Akiielezea historia yake kwa binti huyo alisema yeye ni mwenyeji wa Halmashauri ya Segese na kwamba hakuwa na muda mrefu tangu aanze kazi kwa mama huyo.

“Kwetu ni Segese Halmashauri ya Msalala mimi nilikuwa naishi na baba yangu tu mama sijui aliko maana alituacha mimi na wenzangu tukiwa wadogo sana hivyo nilikuja mjini kutafuta kazi nikafikia kwa mama mmoja wa hapa Mhongolo ninayemfahamu kwa jina la mama Samia na mshahara wangu ni shilingi elfu kumi na ndipo huyu mama aliyenipiga akanichukua,” alisema binti huyo.
Aidha, pia binti huyo alisema akiwa nyumbani kwa mama huyo hakuwa ameelezwa mshahara wake ni kiasi gani kwa kuwa alipelekwa na bosi wake wa zamani.

Antony Manyanda ambaye alimsaidia binti huyo, alisema alimkuta binti huyo akilia kwa huzuni huku akiwa amelala chini kashikilia mkono wake kwa maumivu makali na kuamua kumpeleka katika ofisi za Mtendaji wa Kata ya Mhongolo ili apate msaada wa matibabu.

“Nilimwokota akiwa analia kwa maumivu makali, kwa kuwa alikuwa analia kwa sauti ya juu nikamsikia maana mimi nilikuwa nalinda tanki la maji ya Wachina pale Mhongolo Magharibi, baada ya kumsogelea na kuhoji mkasa uliomkuta nikaona nipeleke katika ofisi za mtendaji ili aweze kupatiwa matibabu,” alisema Manyanda.

Hata hivyo, mtuhumiwa wa mkasa huo Lyina Joseph mkazi wa Kata ya Mhongolo alikiri kumpiga binti huyo ambaye ni mfanyakazi wake lakini akasema sababu haikuwa kutovaa nguo ya ndani bali alimpiga baada ya kuona amekosea kutofanya kazi za nyumbani
Mama huyo muomba radhi afisa huyo mtendaji wa kata na kumsihi aachane na kesi hiyo na akaahidi kwenda kumtibu majeraha aliyonayo kwani alimpa adhabu hiyo kama mwanaye wa kumzaa.
house-girl-2.jpg
Afisa Mtendaji, Maziku Mbusili alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa kitendo alichokifanya mama huyo ni cha ukiukwaji wa haki za binadamu na kuongeza kuwa mtoto huyo hastahili kufanya kazi za ndani kulingana na umri wake kuwa mdogo.

“Nimeamuru tuhumiwa afikishwe polisi kwa kuwa kitendo hicho si cha kibinadamu, hili ni tukio la kinyama, kwanza mtoto huyo yupo chini ya umri wa kufanyishwa kazi za ndani, kwa ujibu wa maelezo ya mwanamke huyo hajui mtoto huyo ni wa wapi maana wamepokezana kijiti na mwenzake aliyekuwa akimtumikisha hapo awali na ujira ni shilingi elfu kumi, hii siyo haki polisi wataamua,” alisema Mtendaji Mbusili.
 
Inasikitisha sana kwakweli....
Kwanza kitendo cha kumpiga mtoto hadi kumpasua kidole, hata kama ni wako wa kumzaa..... Tayari kitendo hicho ni zaidi ya adhabu, bali ni unyama uliopita kawaida
 
Pamoja na Usamaria wangu, napendekeza huyo mama apewe adhabu kali iwe fundisho kwa wengine.
Huwezi kutumia shida au matatizo ya watu kuwanyanyasa. Unamlipa elfu kumi na kumtandika hadi kumchana kidole?

Kama alimwadhibu kama mtoto wake mbona asimpeleke hospitali tokea awali alipoona ameshamuumiza? Roho mbaya na ukatili haujifichi
 
Pamoja na Usamaria wangu, napendekeza huyo mama apewe adhabu kali iwe fundisho kwa wengine.
Huwezi kutumia shida au matatizo ya watu kuwanyanyasa. Unamlipa elfu kumi na kumtandika hadi kumchana kidole?

Kama alimwadhibu kama mtoto wake mbona asimpeleke hospitali tokea awali alipoona ameshamuumiza? Roho mbaya na ukatili haujifichi
Kwakweli afungwe tu ata mwezi
 
Inasikitisha jinsi wazazi wanavyowaangusha watoto wao, wewe baba uko hai unaning'iniza makende yako mawili na kijiita mwanaume alafu mwanao mdogo kabisa anahaha kufanya kazi za ndani? Alafu mama ndio katokomea kusikojulikana. Sio lazima kila mtu azae, wengine ishieni tu kufanya mapenzi!
 
Baba mwenye nyumba sio alikuwa wapi, chakula yake kuharibiwa hivyoo..
Hahaha mama mwenye nyumba alijua tayari binti ni chakula ya baba.

May be hakuwa na hizo nguo za ndani ikambidi atembee hivyo au anayo moja amefua anasubiri ikauke

Baba mwenye mji atakuwa yuko job
 
Back
Top Bottom