Kisa na Mkasa ipi kali kupita zote hapo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa na Mkasa ipi kali kupita zote hapo?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, May 6, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [h=2]AMSHTAKI MWANAMKE ALIYEMN'GAN'GANIA[/h]Bwana mmoja nchini Ujerumani amesema atafungua mashtaka dhidi ya mwanamke aliyemfungia ndani kwa muda wa saa tano mfululizo na kumalimisha kufanya naye mapenzi.
  Bwana huyo anayefahamika kwa jina la Dieter, ameliambia gazeti la TZ la huko kuwa alilazimika kupiga simu plisi waje kumuokoa kutoka nyumbani kwa mwanamke aliyemfungia ndani.
  "Yaani ana wazimu wakufanya ngono" amesema bwana huyo. Akizungumza na gazeti hilo bwana huyo amesema awali walikubaliana na mwanamama huyo kuwa na uhusiano baada ya kukutana katika baa moja.
  Amesema baadaye waliodoka na kuelekea nyumbani kwa mwanamama huyo. Hata hivyo bwana huyo amedai kuwa alipotaka kuondoka alikuta mlango umefungwa na ufunguo umefichwa. Amesema alipotaka kutokea dirishani alishindwa kwa sababu nyumba ya mwanamama huyo ipo katika ghorofa ya juu.
  Amesema mwanamke huyo alimlazimisha kuendelea na mapenzi licha ya kwamba alikuwa hataki tena. Hatimaye mwanamama huyo alipitiwa na usingizi, na bwana huyo kupata upenyo wa kuita polisi. Taarifa zinasema polisi walipowasili, mwanamama huyo alitaka kuwashawishi kwa ngono, lakini polisi walikataa na kumpeleka kituoni, na kumshtaki kwa kumzuilia mtu na kumlazimisha kufanye tendo.
  [h=2]KUKU BILA YAI[/h]Kuku mmoja nchini Si Lanka amezaa kifaranga bila ya kutaga yai. Kwa kawaida kuku hutaga yai na kulitamia kwa muda wa wiki tatu. Hata hivyo kuku huyo hakutaga yai, na badala yake yai lilisalia ndani ya kuku huyo hadi likapasuka na kufaranga kuzaliwa.
  Taarifa zinasema kifaranga hicho kipo katika hali nzuri ya kiafya, ingawa kuku mwenyewe alikufa kutokana na majeraha ya ndani. Afisa mifugo wa huko amekiambia kituo cha habari cha AFP kuwa alikuwa akisikia tu matukio kama haya, lakini safari hii amepata nafasi ya kushuhudia mwenyewe.
  "Kuku huyo alichanika sehemu za uzazi na kusababisha kifo chake" amesema afisa huyo. "Mtoto anaendelea vizuri" ameongeza afisa huyo. Habari hizo zimegongwa vichwa vya habari na huku watu wengine wakisema kitendawili cha kipi kilitangulia kati ya kuku na yai huenda kimeteguliwa.
  Kuku mwingine huko Montana aligonga vichwa vya habari wiki hii baada ya kutaga yai dogo zaidi duniani. Yai hilo lina ukubwa wa sarafu.
  [h=2]TV YA MBWA[/h]Kituo kipya cha Televisheni kinazidi kupata umaarufu nchini Marekani.
  Kituo hicho ni maalum kwa ajili ya mbwa. Kituo hicho kiitwacho DogTV kimepata umaarufu mkubwa mjini San Diego na sasa kitasambaa nchi nzima.
  Vipindi katika televisheni hiyo vimetengenezwa mahsusi kwa ajili ya kuwaliwaza na kuwatumbuiza mbwa, wakati wenye mbwa wakiwa wamekwenda kazini.
  Picha za televishyeni hiyo hupigwa kwa mtazamo wa kimbwa, na hata sauti na muziki umetengenezwa maalum kwa ajili ya mbwa. Mkazi mmoja wa huko Mary Catania amesema mbwa wake ni mshabiki mkubwa wa TV hiyo.
  "Huwa najihisi vibaya ninapomuacha nyumbani na upweke" amesema Bi Mary, "Lakini sasa ana kitu cha kumliwaza" amesema msichana huyo.
  Hata hivyo amesema mara kadhaa mbwa wake hujaribu kuingia ndani ya TV ili aungane na mbwa anaowaona kwenye kioo cha TV.
  [h=2]MLOWESHA VITI AKAMATWA[/h]Bwana mmoja nchini Marekani amejikuta matatani baada ya kupatwa na hatia ya kulowesha viti vya wenzake kazini.
  Bwana huyo mwenye umri wa miaka hamsini na tisa anashikiliwa na vyombo vya dola baada ya wenzake kazini kulalamika kuwa viti vyao ofisini vimekuwa na madoa yasiyoeleweka yanatokea wapi.
  Aidha wamesema wamekuwa wakikuta viti vibichi kila asubuhi wanapofika kazini.
  Mameneja ofisini hapo waliamua kuweka mtego kwa kupachika kamera za video. Baada ya kuzikagua picha za video zilizorekodiwa kwa siri walimuona bwana huyo akijisaidia haja ndogo juu ya viti vya wafanyakazi wenzake, wakati wakiwa wamemaliza kazi na kwenda majumbani kwao.
  Hatma ya bwana huyo bado haijafahamika, lakini amesababisha hasara ya karibu dola elfu nne na mia tano.
  [h=2]DANSI KATIKA MLO[/h]Nchini Uswisi wafanyakazi wamepata njia nyigine ya kujiburudisha wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana.
  Wafanyakazi hao huenda katika vilabu vya kucheza dansi na disco kabla au baada ya kupata lo wao wa mchana.
  Mtindo huo, unaojulikana kama Lunch Beat - yaani mdundo wakati wa maakuli - umeanza kuenea katika miji mingine ya Ulaya. Baada ya kusakata dansi lao wafanyakazi hao hurejea kazini kama kawaida.
  Mtindo huu ulianza kwa wafanyakazi wachache waliokuwa wakicheza muziki katika maeneo ya wazi ya kuegeshea magari. Dansi hilo husakatwa kwa muda wa saa moja, halafu hurejea kazini, ingawa hawatakiwi kunywa vinywaji vyenye ulevi.
  [h=2]ATISHA KWA UFAGIO[/h]Bwana Mmoja anayejulikana kama Lawrence Deptola kutoka mji wa New York huko Marikani ametiwa kizibani baada ya kujaribu kuiba pesa kwa nguvu kwenye benki tatu akitumia ufagio wa chooni kuwatisha wafanyakazi kwenye benki.
  Bwana huyo aliwatisha wafanyakazi wa benki na ufagio huo akisema ni bunduki.
  Polisi waliitwa baada ya Bwana Deptola kuingia katika benki mmoja na ufagio mkononi na kuanza kuwatukana na kuwatisha wafanyakazi wa benki na kuwaamuru wamtilie pesa kwenye mfuko aliyobeba.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [h=2]MTOTO NDANI YA POCHI[/h][​IMG]Pochi ni ya kuwekea hela..


  Polisi nchini Marekani wanamshikilia mama mmoja baada ya kukuta ameficha mtoto mchanga ndani ya pochi yake.
  Polisi katika visiwa vya Virgin wamesema walikuwa katika ukaguzi wa kawaida barabarani na kumsimamisha mwanamama huyo majira ya saa tatu na robo asubuhi siku ya Jumanne.
  Mtandao wa cnews.com umesema afisa wa polisi alimsimamisha mwanamke mmoja na kutaka kuona leseni yake lakini mara akasikia sauti ya mtoto akilia.
  Polisi huyo hakuweza kumuona mtoto lakini akawa akiendelea kusikia sauti ya mtoto, na hivyo kumuuliza mama huyo yuko wapi mtoto anayelia.
  Polisi wamesema mama huyo alifungua zipu ya pochi yake na kumtoa mtoto mchanga wa kike.
  Mwanamama huyo amesema alijifungua mtoto huyo wiki moja iliyopita akiwa nyumbani kwake.
  Mtoto huyo amepelekwa hospitali na mama huyo huenda akakabiliwa na mashtaka ya uhalifu kwa kutompeleka hospitali mwanaye, baada ya kujifungua.
  [h=2]WAZAZI WASUSA MTOTO WA KIKE[/h][​IMG]Mji wa Jodphur kulikotokea sakata hilo


  Wazazi nchini India waliosusa kumchukua mtoto wao wa kike, kwa madai kuwa mtoto wao aliozaliwa ni wa kiume, hatimaye wamerejea kumchukua, baada ya vipimo vya DNA kuonesha mtoto huyo wa kike ni wa kwao.
  Wazazi hao walidai kuwa mtoto wao ni wa kiume na wamebadilishiwa na kupewa wa kike. Taarifa ya BBC imesema watoto wawili walizaliwa katika muda unaofanana katika hospitali moja mjini Jodphur wiki moja iliyopita.
  Habari zinasema mchanganyiko wa watoto ulitokea na sakata la kugombea mtoto wa kuime likaanza kati ya familia mbili. Suala hilo lilipelekwa mahakamani na amri ya vipimo vya DNA kutakiwa kuchukuliwa ili kutatua utata huo.
  Katika kipindi chote hicho mtoto wa kike alikuwa amesalia hospitali, huku wa kiume akiwa anagombewa na familia hizo mbili. Wazazi hao Bwana na Bibi Chain Singh, hatimaye walikubali matokeo ya vipimo na kurejea hospitali kwenda kumchukua kichanga wao wa kike.
  [h=2]MKATA NYWELE ABAMBWA[/h][​IMG]Marufuku kutembea na mkasi


  Bwana mmoja hapa Uingereza amepigwa marufuku kupita mitaani huku akiwa amebeba mkasi.
  Polisi wamesema bwana huyo Darren Dixon wa mjini Salford, Manchester alikutwa na hatia ya kukata nywele wasichana wawili. Mtandao wa habari wa MSN umesema Bwana huyo alikuwa akinyatia wasichana mitaani na kuwakata nywele kimyakimya.
  Mahakama imempa bwana huyo hukumu ya kutumikia jamii kwa miaka mitatu na pia kupigwa marufuku kubeba mkasi na vifaa vyovyote vinavyotumiwa na vinyozi mitaani. Polisi wamesema katika tukio moja msichana mmoja aligundua kuwa alikuwa akifuatwa kwa karibu na bwana Dixon, na alipoongeza mwendo na Dixon naye akamfuata, na mara alisikia mlio kwa mkasi ukikata.
  Msichana huyo amesema alipogeuka, aliomuona mtu akiokota nyewele zake na kukimbia. Kachero wa polisi Konstebo Lawrence Gallagher amesema bwana Dixon hakusema kwa nini alikuwa akikata nywele za wasichana hao.
  [h=2]WASICHANA WAGEUKA WAVULANA[/h][​IMG]Mapacha wabadili jinsia (sio pichani)


  Wasichana wawili mapacha wa kichina wamefanikiwa kuwa mapacha wa kwanza kubadili jinsia na kuwa wanaume.
  Kinadada hao kutoka jimbo la kusinimagharibi mwa uchina la Yunnan walifanyia ubadilishwaji wa jinsia zao katika hospitali ya kijeshi ya mjini Shanghai. "Shughuli ya kuwabadili kutoka wanawake kuwa wanaume imekwenda vizuri" amesema Daktari Zhao Yede Daktari aliyewafanyia mabadiliko hayo.
  Gazeti la Shanghai Daily limesema pacha mmoja ameruhusiwa kurejea nyumbani wakati mwingine bado anapata matibabu hospitalini.
  Madaktari wamesema kinadada hao mapacha walikuwa wakipenda kuvaa nguo za kiume, na waliweka ahadi ya kutofunga ndoa hadi watakapo kuwa wanaume.
  Gazeti la Sun limewakariri wakisema mapacha hao wamekamilisha ndoto yao ya muda mrefu. Mmoja wa mapacha hao amesema hawakutaka habari zao zijulikane kwa sababu wanaweza kufukuzwa kazi.

  [h=2]KUKU KATAMIA BATA[/h][​IMG]Kasheshe kwenye maji


  Kuku mmoja nchini Marekani ametotoa vitoto vya bata baada ya kutamia mayai ya bata kimakosa.
  Kuku huyo aitwaye Hilda, alitamia mayai hayo akidhani ni ya kwake. Gazeti la Daily Mail limesema kuku huyo aliyatamia mayai hayo matano kwa muda wa mwezi mzima, bila kufahamu kama sio ya kuku.
  Mmiliki wa kuku huyo, mfugaji Philip Palmer amesema hata kifaranga cha kwanza cha bata kilipotoka, kuku huyohakukata tamaa na aliendelea kutamia na sasa ni kama mama yao.
  Mahala pekee kuku huyo anahisi kuna musheli ni wakati vifaranga vya bata vikiingia ndani ya maji na kuku huyo kushinda kuwafuata. Bwana Phillip amesema kuku huyo ameonesha kutojali na vifaranga vya bata hao humfuata kila mahali.
  Mfugaji huyo amesema huenda kuku huyo bado hajafahamu kama vifaranga vyake ni bata, na hata vifaranga vyenyewe havijui kama mama yao ni kuku.
  [​IMG]Mitindo mingine ya nywele sio mchezo


  Bwana mmoja nchini Marekani ametupwa gerezani kwa miaka mitano baada ya kumpiga risasi msichana mmoja akidhani ni ndege.
  Gazeti la Daily Sentinel limesema Bwana huyo Derrill Rockwell alidhani ni ndege aliyekuwa akiwasumbua sana paka wake.
  Msichana huyo alikuwa amepaka rangi nyekundu nyewele zake na kufanana na ndege wenye vibwenzi vyekundu.
  Bwana Rockwell amewaambia polisi kuwa baada ya kusikia paka wake wakikimbia alichukua bunduki yake na kwenda kumsaka ndege huyo, na kwa umbali wa kama futi tisini alimuona msichana huyo akipita na nywele zake nyekudu, na akadhani ni ndege.
  Lakini baada ya kufyatua bunduki yake,bwana huyo amesema akaona ndege huyo hajaruka na badala yake alisikia mayowe ya msichana.
  Kaimu hakimu Jason Conley amesema bwana huyo hakuwa na nia ya kumpiga risasi dada huyo, bali kweli alikuwa akitaka kutisha tu ndege.
  Taarifa zinasema baada ya kusikia ukelele huo bwana Rokwell aligundua kuwa amempiga risasi binaadam na sio ndege. Gazeti limesema msichana huyo mwenye umri wa miaka ishirini na tatu alinusurika, lakini ameuhama mji wa Colorado.
  Na kwa taarifa yako........... Mchwa hujinyoosha wanapoamka asubuhi.
   
 3. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Duh!zote kali aisee dunia ina maajabu but iliyonishangaza zaidi ni ya kuku kuzaa kifaranga bila yai..
   
 4. Endangered

  Endangered JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 929
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  na wale wa lady gaga style, wajihadhari, tutapata kesi za bure tukidhani ni ndege.
  Mkuu thenkyu kwa stori!
   
 5. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,208
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  zote zimetisha but imenipa majonzi pia huyo mama kuku alotamia vijibata pale anaposhindwa la kufanya akiviona vijibata vikiingia kwenye maji.
   
 6. Dachr

  Dachr Senior Member

  #6
  May 6, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mhhh....
  Mhh....mhhh
   
Loading...