Kisa mkwara, baba amposa bintiye bure

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
Kisa mkwara, baba amposa bintiye bure
Kabla sijakuletea kijistori cha baba mkwe aliyelazimika kumposa bure binti yake baada ya kuchimbwa mkwara, nitoe ushauri kwamba ni lazima mtu ujiamini. Unapokuwa muoga, unaweza kujikuta umeondoka kwenye mstari na kuharibu historia na heshima yako.
Usiwe kama Hamdun ambaye alishawahi kumkuta mkewe anavunja amri ya sita na Jimmy Baunsa, badala ya kuchukua hatua eti akaomba msamaha kwa kuwaingilia. Aliwafumania chumbani kwake, tena kwenye kitanda chake mwenyewe.
Jimmy Baunsa alipomaliza shughuli yake chumbani, akatoka kwa kujiamini, akampita Hamdun amekaa sebuleni, akamuaga: “Kaka mimi natoka.” Hamdun akaendeleza ujuha, akajibu: “Shukurani bro, karibu tena.” Yaani Jimmy anakaribishwa tena!
LUQ%20MALOTO.jpg

Ajabu ni kwamba baada ya Jimmy kuondoka ndiyo akaanza kumvaa mkewe kwa maswali. Eti, akamuuliza ni kwa nini amemuingiza mwanaume nyumbani kwake na kufanya naye mapenzi tena chumbani kwenye kitanda chake?
Unajua jinsi mke alijibu? Akampasha mume wake: “Wewe vipi? Katika wanaume na wewe umo? Umeshindwa kumkabili mwanaume mwenzako unakuja kunifuata mimi, hebu ishia zako huko!” Haya sasa!
Wakati nakushauri usiwe kama Hamdun, tatizo la woga lilimfanya baba mkwe ampose mwanaye bure. Unajua kipi hasa kisa na mkasa? Soma mahojiano haya:
MKWE: Yaani unakuja kuposa binti yangu huku unatafuna Big G? Kijana unaleta dharau kwenye nyumba yangu?
MUOAJI: Hapana mzee, sina dharau kabisa. Natafuna Big G kwa sababu mdomo unanuka.
MKWE: Mdomo unanuka? Yaani kijana unanuka mdomo?
MUOAJI: Ndiyo, mdomo unanuka nilivuta sigara.
MKWE: Hee kijana, kumbe wewe ni mvutaji wa sigara?
MUOAJI: Ndiyo mzee, nilivuta jana nilipokunywa pombe wakati nipo klabu.
MKWE: Hii sasa ni kazi, kumbe na pombe unakunywa, wewe ni mlevi?
MUOAJI: Siyo mlevi sana, nilifunza kunywa pombe wakati nipo jela.
MKWE: Mtumee, yaani hata kufungwa ulishafungwa.
MUOAJI: Ndiyo mzee wangu, nilifungwa kwa kosa la kuua.
MKWE: Mungu wangu, kwa maana hiyo wewe ni muuaji!
MUOAJI: Ndiyo, nilimuua mzee mmoja, alikataa posa yangu kwa binti yake, ikabidi nimuulie mbali. Mimi ujinga huwa sipendi.
MKWE: Heeee, basi hakuna shida kijana. Mke nimeshakupa, sasa wewe mwenyewe amua harusi tufanye lini? He he he…!
 
Hii nzuri sana ila topic ilitakiwa isomeke hivi: kisa mkwara, "Baba amuoza bintiye bure." na siyo "amposa"
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom