Kisa kilichosababisha moyo wangu kupata maumivu makali ya ndani kwa ndani

DUMU

JF-Expert Member
Sep 23, 2019
431
577
Ndugu za poleni kwa mapambano ya nyumonia mpya ila natumai Mungu atatufanyekuwa washindi kwa hili.

Mimi ni kati ya kijana aliyepitia changamoto nyingi za kimaisha katika harakati zangu za kimaisha nikajikuta nimetumia miaka mingi kumaliza elimu yangu yaani kuanzia darasa la saba mpaka chuo kikuu. Sio kwamba nilikuwa nafeli hapana ila tu kipato cha wazazi wangu hakikukaa sawa.

Baada ya kumaliza darasa la saba nilikaa mtaani muda kidogo nikisubiri wazazi wapate hela ya kunipeleka shule ya sekondari pia kipindi nilipomaliza darasa la saba licha ya kufaulu kwenda fomuwani sikuweza kwenda kwani kipindi hichohicho mmoja ya mzazi wangu alipatwa na ugonjwa wa ajabu tiba za hospitali ziligonga mwamba na badala yake muda mwingi tukatumia kuhangaika kwenye tiba asili nashuku Mungu hatimaye mzazi wangu aliweza kupata nafuu na kupona tatizo lilokuwa likimsumbua kwa muda mrefu yapata kama miaka minne mfululizo.

Baada ya matatizo ya mzazi wangu harakati za mimi kwenda shule zikaanza. Nilifanya mawasiliano na jamaangu mmoja kipindi hicho huyo jamaa alikuwa akiishi mbeya anafanya shughulizake binafsi za kujiingizia kipato, akanitafutia shule ya sekondari iliyopo mbeya mjini ambayo gharama zake zilikuwa ni kubwa ila kwa kipato cha wazazi wangu wangeweza kuzimudu.

Muda ukafika nikajiunga na shule baada ya muda mfupi mitihani ilifanyika nashukuru nilionekana ninauwezo mzuri tu licha ya kukaa nje ya mfumo wa kielimu muda mrefu.

Bila kupoteza muda sana habari ili iko hivi: Siku hiyo nilienda shule kujisomea maana mimi nilikuwa nimepanga gheto na huwa kila siku za juma mosi na juma pili asubuhi naenda shule kujisomea kwakuwa mazingira ya gheto siopoa kwa kujisomea hakuna kiti hakukuwa na meza hakukuwa na kitanda ila nilinunua godoro la 2.5 ft kwa 6ft, pamaoja na ndoo ndogo moja , sufuria mbili za kupikia mfuniko mmoja hapo gheto limekamilika nilijiambia wazazi wangu choka mbaya na huku nimekuja kusoma nikawa na soma kwa nidii licha ya changamoto za hapa na pale.

Siku ya tukio nilienda shule kama ada nikafika shule nikajisomea ila baada kama lisaa kupita kuna mwalimu wangu mmoja akaniita maana namuheshimu sana naye ananiheshimu sana . Akaniomba nikachukue funguo za ofisi kwa mwalimu mwingine ambaye alikuwa anaishi mita kama hasini (50m) kutoka shule ilipo ambapo amepanga chumba pamoja na wananchi wengine.

Nilikubali wito wa mwalimu nikaelekea kula anakoishi mwalimu kuifuata funguo. Nikafika kwenye ile nyumba pake nje nikakutana na binti alikuwa anafagia uwanja nikamsalimu akakubali salamu yangu. Nikamuomba anioneshe nyumba na chumba anachoishi mwalimu X ambaye nilitumwafunguo kwake. Yule binti akanambia pita mlango ule ingia ndani ukaulize nikaingia nikaelekea uelekeo alosema yule binti karibu na mlango alonielekeza kulikuwa na mama wa makamo tu kabla ya kuingia nikamuuliza tena kwa uhakika zaidi akanionesha chumba cha yule mwalimu.

Nikaingia mle ndani nikasimama nje ya chumba nikagonga mlango huku nikilitaja jina la mwalimu nikasikia sauti toka upande mwingine wa nyumba ukinijibu huyo mwalimu ameshatoka. Nikamshukuru nikatoka nje nikamshukuru tena yule binti kiumri yule binti aalikuwa ni 18+ ivi.

Nikaondoka kufikisha ujumbe kwa mwalimu aliyenituma kuwa yule mwalimu sijamkuta nimeambiwa ametoka. Mwalimu akaniruhusu nikaendelee na shugulizangu za kujisomea .

Mara baada ya kupita kama dakika 15 hivi kuna jamaa naye ni mwanafunzi wa pale shule nayosoma ila yeye anasoma darasa la juu ila hatujuani ila mimi huwa namwona mara kadhaa pale shule ila nikuwa sijui anaishi wapi akanifuata kuwa naitwa nikamuuliza naitwa wapi pia naitwa na nani akanambia pale ulipofuata funguo ila nifuate twende nikasema twende.

Huku nikiwaza nikajisemea itakuwa mwalimu atakuwaashurudi labda anataka anipefunguo nizilete kwa mwalimu aliyezihitaji. Nikafika pale kwenye ile nyumba nje kuna wapangaji kadhaa wasiopungua kama nane hivi yule kijana tuloongozana akawambia wale
wapangaji jamaa mwenyewe mwizi ndio huyu.

Nikastaajabu mmoja kati ya wale wapangaji kawaanambia leo lazima tukuchome moto nikamwambia umezoa wizi enhee juzi umetoka kutuibia umeona haitoshi leo umeona ngoja uje ukague tena vitu vya kuiba

Nikamwambia kaka naomba nijitambulishe nisikilize kabla hauja nihukumu kwa chochote nikusimulie jinsi ilivyo ama ukionaje nakuomba piga simu wa jeshi la polisi hayo maelezo hata polisi nikayatoe.
Nikajitambulisha nakuwasimulia kama jinsi nilivyofika nakuingia ndani.

Pia nimwambia mimi nilipofika hapa nilimkuta huyu dada hapa nikamuuliza na yule mama pale sikuamini macho yangu na masikio yangu yule dada na yule mama alikana katukatu kuwa siawauliza kuhusu mwalimu niliyemfuata pale.

Wote wakawa wanasema ameingia mlango ambao hautumiki huyu atakuwa mwizi tu hata vile vitu vya juzi atakuwa ameiba huyu huyu
Bahati nzuri kuna mpangaji mmoja alikuwa ni wa kike akawambia wale wapangaji wenzake tumwite mwalimu aliye mtuma kweli

wakakubali mwalimu akaitwa kufika pale ameshangaa mimi kuwekwa mtu kati akauliza ninitatizo maana huyu ni mwanafunzi wangu nilimtuma hapa muda si mrefu sana , wakaanza kumwambia ooh sisi juzi tuliibiwa kwahiyo huyo naye alipofika hapa hajasalimia mtu yoyote yeye akaingia ndani na akatoka akaondoka bila kusema chochote.

Mimi nikamwambia mwalimu hali halisi jinsi ilivyo hivyo mwalimu akawaomba wanisamehe pale nilipowakwaza na akawambia labda kama hizo tabia anazifanya akiwa kwake ila kwa hapa shuleni kwetu ni kijana mwenye nidhamu nzuri na hatujawahi kupata malalamiko aidha toka kwa wanafunzi wenzake ama mtaani anakoishi.

Baada ya maelezo ya mwalimu wakaniruhusu kuondoka ila kwakweli ile siku imechafua sana taswira ya moyo wangu hivo ninapokumbuka liletukio huwa naumia moyo sana . Tabia ya wizi sijawahi ifanya wala udokozi wala dhuluma ya aina yoyote.

Najua stori ni ndefu na muda wa wanajf kusoma ni mdogo sana . Mnisamehe kwa kupoteza muda wako kwa kusoma tukio hili labda lingewezakuwa mwisho wa maisha yangu. Asante
 
Pole sana Ni maisha tu.Ninachojitahid kila siku kabla sijaanza siku ni kujiombea binafsi na kuwaombea wanangu kwa kuwataja majina wote.ktika mambo menngi nitakayoomba huwa siachi kusema Mungu atuepusha na HATARI MAJANGA ,MIKOSI NA MABALAA.
NB
haimaanishi hii ndio dawa tosha ila atleast huwa napata feeling kwamba we r in safe hands.yakitokea mengie namuachia Mungu
 
Nimeumia kaka!! Ila usijali, Kikubwa haukudhurika, binadamu wabaya sana. Watu wawili wanakuruka foot 100, uliamini wao ndo watetezi wako. Kaka hata jela wengi ni wenye mikasa kama yako wanyonge, waliokosa watetezi.
 
Pole sana ,huyo binti na huyo bimkubwa ulishawahi kutanà nao? Nina wasiwasi itakauwa wao ndiyio walikuwa vibaka wa hapo!
 
Duh umemaliza au maana kama ndiyo ilikuwa inaanza vile, ila pole leo ungekuwa marehemu alikuwa mtu wa watu mpole.
Kweli kuna muda tusiwetunakimbilia kuhukumu kabla ya kusikiliza upande wa pili
 
Pole sana ,huyo binti na huyo bimkubwa ulishawahi kutanà nao? Nina wasiwasi itakauwa wao ndiyio walikuwa vibaka wa hapo!
Wote sijawi kukutana nao kabla ya siku ya tukio.
 
Mimi sio mtaalamu wa haya mambo, lakini sio vizuri kupita bila kusema chochote, Ila kama nilivosema hapo mwanzo mimi sio expert wa haya mambo, kwahiyo ngoja nikae kimya.

BTW, Mitano tena.
 
Kuna mtu huku alisakiziwa mwizi wa chupi za mtaani


Sasa wewe unaumia moyo nini?
 
Pole na nibdhahir una mikosi ila kama hukusalimia bas na mwiz ni uyo jamaa aliekuita akishirikiana na hao wawili
Mitano +
 
Umelizungumzia hili tukio, bila shaka itakuwa ni njia ya kukuondolea maumivu yanayokusumbua. Daima kuwa mkweli, na ukweli utakuweka huru, haijalishi wanadamu wana nia gani mbaya juu yako.
 
Umelizungumzia hili tukio, bila shaka itakuwa ni njia ya kukuondolea maumivu yanayokusumbua. Daima kuwa mkweli, na ukweli utakuweka huru, haijalishi wanadamu wana nia gani mbaya juu yako.
Roho yangu inaamani sasa baada ya kuweka hili dukuduku kwenye maandishi.
 
Back
Top Bottom