Kisa chenye mazingatio: Siyo kila mwendawazimu ni mwendawazimu


kwinyo

kwinyo

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2017
Messages
282
Likes
229
Points
60
kwinyo

kwinyo

JF-Expert Member
Joined May 2, 2017
282 229 60
SIYO KILA MWENDAWAZIMU NI MWENDAWAZIMU !!

Palikua na mfalme na mwendawazimu ambao walikutana makaburini.

Mfalme: imekuaje wewe unaishi makaburi siku zote?! Na hutaki kuondoka mahala hapa? Je huna hata chembe ya akili hata ya kukuonesha matatizo ya hapo? Ni swali alouliza mfalme baada ya kumuona chizi amejenga kibanda makaburi.

Mwendawazimu: nadhani itakuwa wewe ndiwe hujielewi! Au huna chembe ya akili!!

Mfalme: kwanini unasema hivyo?!

Mwendawazimu: Mimi nimeona hakuna nyumba ya kubaki ila hizi hapa, nikaamua kusogea karibu hapa! Na wewe
Umeona fahari kujenga kasri ile kubwa na kupakimbia mahala hapa, unasahau kama nawe ipo siku utafika hapa, kwanini usipaimarishe?

Kwani hawa hawakua RAIA zako? Kwani hawataki tena kuishi vizuri? Kwani Hawataki kutembelewa tena?! Pamoja na ufalme wako umeshindwa kuweka waangalizi mahala hapa ambapo kila MTU atarejea? Umejenga kwa gharama nyumba utakayoiacha na kuitupa nyumba utakayoishi milele??!!

Mfalme alibubujikwa na machozi huku akisema sio kila mwendawazimu ni
mwendawazimu, nimekosaje chembe ya akili Mimi????!
Mfalme akamwambia Mwendawazimu omba utakacho nitakupa,

Mwendawazimu akasema naomba mambo matatu?! Naomba uniongezee umri wangu, naomba unipe ulinzi siku atakaponijia malakul-maut, naomba unihakikishie kuingia peponi.. Mfalme akapiga kelele sana!!

Mwendawazimu akamuuliza. Nani kati yetu Mwendawazimu?!

Mfalme akasema. Mimi, Mimi, Mimi.. Mwendawazimu akamuuliza kwanini akasema yote uliyoyaomba sina uwezo nayo, na nilikuwa natembea kwa fahari sana nikidhani Nina uwezo kumbe Mimi si lolote si chochote!! Hata Mimi mwenyewe hayo siwezi kujipatia!!!

Basi Mwendawazimu akamwambia yupo anaeweza nae ni Al-waahidul Qahaar, ndie MFALME wa kila kitu, nami na akili zangu zote zimekwisha kumfikiria yeye!! Mwisho:
jifunze kitu hapo. Wabillahi Tawfiyq.
 

Forum statistics

Threads 1,239,198
Members 476,441
Posts 29,345,452