Kisa cha Waziri Ngeleja na Mlinzi kwenye ATM

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
Ngeleja azua tafrani ATM

  • NI BAADA YA KUTAKIWA AWAPISHE WATEJA
Sadick Mtulya

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, juzi alizua tafrani kwenye mashine ya kuchukulia fedha (ATM) ya benki ya Standard Chartered, jijini Dar es Salaam baada ya kutaka kumchapa makonde mlinzi wa mashine hiyo, Pascal Mnaku.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na mlinzi huyo wa kampuni ya Ultimate Security, zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 asubuhi kwenye jengo la Habour View, maarufu kama JMall.

Mnaku aliliambia gazeti hili kuwa alinusurika kupigwa na waziri huyo kijana aliyekuwa akizungumza na simu ndani ya kibanda hicho, baada ya kumtaka atoke kuwapisha wateja wengine kupata huduma hiyo.

Mnaku alisema waziri huyo alikuwa anatumia muda mwingi kuzungumza na simu ndani ya mashine hiyo badala ya kuchukua fedha wakati msururu mrefu wa watu ukiwa unamsubiri atoke.

"Kwanza mimi sikujua kwamba mtu niliyemwambia awapishe wateja wengine ni waziri. Ni kweli nilimfuata na kumwambia awapishe kwa sababu alikuwa anatumia muda mwingi kuzungumza na simu, wala sikuwa na nia nyingine yoyote mbaya dhidi yake," alisema Mnaku na kuongeza:

"Lakini, waziri huyo ghafla aligeuka na kuanza kunifokea akiniambia wewe unanijua mimi nani?... hunijui mimi! na kunitusi, (matusi yasiyoweza kuandikika)."

Mnaku aliendelea kueleza kuwa; "Kutokana na hali hiyo nilipomjibu kwamba, mimi sikuwa na nia mbaya na nilifanya vile ili wateja wengine wapate huduma".

Aliongeza: "Baada ya kumwambia hivyo akazidisha ukali, lakini watu walipoanza kukusanyika, huku wengine wakimwomba radhi kwa kumtaja jina, alianza kupunguza hasira na kuondoka".

Kwa mujibu wa mlinzi huyo, baada ya tafrani hiyo iliyodumu kwa takribani dakika nane, Waziri Ngeleja aliondoka na baadaye kunako majira ya saa 7:00 mchana uongozi wa kampuni yake ya ulinzi ulimwondoa katika kituo hicho cha kazi na kurudishwa makao makuu.

Alisema saa 9:30 jioni, alichukuliwa na uongozi wa kampuni hiyo na kupelekwa ofisini kwa Ngeleja kwa ajili ya mazungumzo zaidi.

"Baada ya kutokea kwa tukio saa 9:30 jioni wakuu wangu walinipeleka ofisini kwa Ngeleja na kisha akazungumza mengi ambayo siwezi kukuambia na baada ya hapo wakuu wangu wakamuomba msamaha kwa niaba ya kampuni," alisema Mnaku.

"Na kwa sasa maelekezo niliyopata kutoka kwa waajiri wangu ni kwamba, wanalifanyia upelelezi suala hili hivyo hatima ya kibarua changu kinategemeana na majibu ya upelelezi huo," alisema Mnaku

Mashuhuda wa tukio hilo walilieleza gazeti hili kuwa hali hiyo ilijitokeza baada ya Mnaku kuwahamishia wateja kutoka katika mashine ya ATM ya Barclays iliyoko katika jengo hilo ambayo wakati huo ilikuwa imeishiwa fedha.

"Baada ya Mnaku kuona mashine ya ATM ya Barclays kuwa haina fedha, ndipo akalazimika kuwaambia wateja wakatumie ATM ya Standard Chartered ambayo wakati huo Waziri Ngeleja alikuwa anaitumia na huku akizungumza na simu," alisema shuhuda mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe.

Shuhuda huyo alisema baada ya Mnaku kumtaka waziri kuwapisha wengine, ghafla na huku akiwa na hasira, Waziri Ngeleja alisema: "Ina maana hunijui mimi, hujui nafasi yangu, halafu...tusi," alisema shuhuda huyo.

Shuhuda huyo aliongeza: "Kutokana na maneno hayo, Mnaku akamjibu kwa kujitetea kwamba, mimi nimekuomba uwapishe wateja wengine, sikuwa na lingine".

Habari zaidi zinadai kwamba, katika kikao na waajiri wa Mnaku, Ngeleja alisema: "Siwezi kumsamehe (Mnaku) mpaka atakapopewe adhabu kali."


kazi ipo
 

Attachments

  • ngeleja.jpg
    ngeleja.jpg
    19.2 KB · Views: 132
Ochu,

Hii habari umeikopi vibaya, haitiririki. Tafadhali irekebishe.
 
huyu waziri ana mapepo sana;anatumia madaraka yake vibaya
Siku moja nikiwa mwanza usiku wa manane na ATCL tumeshapanda muda
umefika wa kuondoka;ndege aiondoki ukiuliza wafanyakazi awajibu
akatokea dada mmoja wa airco akaingia ndani nikamuuliza nini tatizo
akadai ngeleja alipiga simu nusu saa sasa ndege imsubirir anakuja
ikabidi tuwaabarishe wenzetu ndipo kelele zikaanza rubani akaona haya
akaamua kuondoka;
tulipofika dar nikapiga kwa mmoja wa marafikizangu mfanyakazi wa ATC
kwa nini wametutenda vile tunakaa nusu saa na mwisho hata huyo ngeleja akuonekana???akaanza kaka we acha kwanza nina msala nimepigiwa hapa simu na Bosi wangu nitoe maelezo;jamaa kachelewa kajaa kaanza kutoa maneno ya dharau;mara anantutishia tutajuta kumwacha;akaanza kuwapigia wAKUBWA WA atc ovyo;...alipandisha zaidi alipoambiwa na mmoja wa wafanyakazi airport aliachwa edward lowassa akiwa waziri mkuu ije kuwa wewe;so
ni katabia fulani anaitajika kukabadilisha ama kukiondoa kabisa kama anaweza;else ataishi na watu kwa matatizo;hawa wakubwa wa ultimate awatakiwi kumwadhibu kabisa waulize hali halisi wajibiwe;
 
Jamaa atafukuzwa kazi bila kosa,alikuwa akitekeleza majukumu yake lakini itaonekana kama alimkosea waziri heshima.
 
Tunalalamika nini si ndio wawakilishi wetu tuliwachagua huko majimboni na kuchinja ng'ombe walipopata uwaziri??? Leo ndio tunaumia? na kura tutampa kedekede mwezi october

Kikwete is right...
 
Wengi tunadhani mawaziri wazee ndio wenye matatizo, sasa kama na vijana kama ngereja anafanya aliyoyafanaya basi kuna kazi nchi hii. Kwa ufupi Ngeleja hana nidhamu, amekidhalilisha cheo na madaraka aliyokabidhiwa kuwahudumia hao anaowaita kwamba 'hawajui nafasi yake'. Sasa wakiijua so what???????????????????????????
 
Ndio itakavyokua mkuu,matatizo ya nchi zetu haya......

...Kibaya zaidi ni kuwa Vyombo vyetu havina utamaduni wa kufuatilia story kama hii, kwa mfano miezi mitatu baadaye, kujua kilichoendelea kuhusu huyo askari. ndio maana tutaendelea kunyanyaswa tu.
 
Mnaku aliliambia gazeti hili kuwa alinusurika kupigwa na waziri huyo kijana aliyekuwa akizungumza na simu ndani ya kibanda hicho, baada ya kumtaka atoke kuwapisha wateja wengine kupata huduma hiyo.

Mnaku alisema waziri huyo alikuwa anatumia muda mwingi kuzungumza na simu ndani ya mashine hiyo badala ya kuchukua fedha wakati msururu mrefu wa watu ukiwa unamsubiri atoke.

"Kwanza mimi sikujua kwamba mtu niliyemwambia awapishe wateja wengine ni waziri. Ni kweli nilimfuata na kumwambia awapishe kwa sababu alikuwa anatumia muda mwingi kuzungumza na simu, wala sikuwa na nia nyingine yoyote mbaya dhidi yake," alisema Mnaku na kuongeza:

"Lakini, waziri huyo ghafla aligeuka na kuanza kunifokea akiniambia wewe unanijua mimi nani?... hunijui mimi! na kunitusi, (matusi yasiyoweza kuandikika)."

Huyu ndie waziri, kiwango cha busara kidogo kuliko bawabu! Kikwete an kazi kubwa sana ya kufanya! Yaani ni 'hovyo hovyo' tu!
 
Kifupi huyu askari kibarua hana.Kitendo cha mabosi wake kumburuza mpaka kwa Ngeleja sio sahihi hata kidogo kiutawala.Mbaya zaidi viongozi wetu ni kama Miungu...hawakosei hata siku moja.All they do must be accepted by all as correct.Hao waliokuwa kwenye hiyo queue nao wana matatizo kwa vile walimjua yeye ni waziri basi wakatulia...hata askari yule angalijua huyu ni waziri angetulia vilevile....naona mabebenki yawawekee wakubwa wetu ATMs majumbani kwao ili tuwe mabli nao
 
Aaah, kaboa kweli mheshimiwa, unaongeaje na simu ATM machine? Halafu hawa watu hawajui kuwa kesho tu wanaweza kuwa barabarani. Akifukuzwa kazi huyo mlinzi vilio vyote vya wanawe watakaokosa ada na chakula vitamfuata. Halafu why would a Minister argue with a guard? he went too low...
 
Duh japokuwa sijui upande wa pili, yaani Mh Ngeleja hadithi yake ni vipi, lakini kama hii habari jinsi ilivyoandikwa ni sawa basi huyo Waziri kwa kweli hafai kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi. Hivi hawa watu huwa wanasahau kuwa wao wanatakiwa kuwatumikia wananchi na sio wao kuwa wafalme na sisi kuwa ni watumwa wao. Hao waliomwomba msamaha nao ndio wanaowapa kichwa hao mabwanyenye. Kazi ipo nashukuru hili gazeti kuandika hili kwani linatufungua macho wengi.
 
Humu jamvini kuna waandishi wengi,kwa nini wasifuatilie tukio hili na likatoka magazetini ili wananchi wa kawaida ambao hawana muda wa kusoma mtandaoni wakawajua viongozi wao waliowachagua wakoje? Kisa cha Meya wa Moshi kumpiga mlinzi makofi kama kisingetoka magazetini kingeisha kimya kimya lakini kusambaa kwa habari ile kumefanya haki itendeke. Wajibikeni waandishi.
 

hi kali - ila nachojua mimi ukiwa waziri unakuwa exempted kwenye public services kwamba hutatakiwa kupanga foleni na unatakiwa kupata huduma muda uleule na kuondoka ili uwahi majukumu ya kiserikali ya kufanya.

Kwa hiyo hata kama Ngereja angekaa mule saa nzima anaongea na simu hakuna ubaya, may be alikuwa anaongea na Bosi wake (Rais) kwa hiyo hawezi kum hold bosi wake na lazima akae sehemu kuna privacy. (Hii inafanya kazi kama simu ilikuwa muhimu sana na asingeweza kui hold)

Kingine yule mlinzi kutomjua huyu ni ngereja kama ni waziri si kosa, kwa hiyo cha msingi Ngereja asipeleke mambo haya yawe makubwa, amsamehe ili jamaa aendelee kutafuta mkate wa watoto wake.

Lakini na we Ngereja kama call haikuwa ni emergency kwa nini usimwambie yule mtu aliyekupigia kwamba huko kwenye postion ya kupokea simu yake then umpigie baadaye?
 
Jamaa atafukuzwa kazi bila kosa,alikuwa akitekeleza majukumu yake lakini itaonekana kama alimkosea waziri heshima.
..Ni kweli na kama jamaa atafukuzwa kazi lawama zote kwa Ngeleja, kwani kwa jinsi nilivyoielewa hii story mlinzi alimshauri kitu cha maana sana na sioni kosa lake hata kama anadai kuwa hatamsamehe.Huwezi kuingia kwenye ATM ukaendelea kuongea na simu as if uko kwenye telephone booth badala ya kuchua pesa utoke na kupisha wengine. Hata huyo Ngeleja ana ulimbukeni fulani na kwa nini akimbilie kumuuliza mlinza mlinzi kuwa kwani yeye hamjui ni nani? Mambo mengine ni kutumia akili na busara tu. Angejaribu kunitusi mimi nisingejali ni waziri au nini Ningemuangushia kosovo tu habari nyingine tutajuana mbele ya safari. Haya mambo ndio Nyerere alikuwa anakemea viongozi kuishi kihuni huni...
 
Back
Top Bottom