Kisa cha Vidkun Quisling jina lake likawa msamiati mpya wa usaliti

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,912
30,254
KISA CHA VIDKUN QUISLING

Naamini itawashangaza wengi nikiwaeleza kuwa jina la Jecha na jinsi Wazanzibari walivyoliingiza katika msamiati wao ni sawa na jina la Vidkun Quisling nalo pia lilivyoingia katika msamiati wa dunia nzima kwa vitendo sawa na alivyofanya Jecha Salum Jecha.

Mfano mwingine ni jina la Kihiyo kumithilishwa na mtu ambae hana elimu lakini akajifanya na kuwaaminisha watu kuwa kaelimika vizuri.

Leo mtu akikwambia mathalan, ‘’Asikushughulishe huyo ni Kihiyo,’’ mara moja unajua kuwa anakuambia usipoteze muda na yeye hana alijualo.

Mifano hiyo hapo juu nikianza na neno, ''Jecha'' maana yake ni mtu aliyebadili au kufuta matokeo halali ya kitu chochote kile ama iwe matokeo ya uchaguzi au hata ya mtihani.

Neno, ''Kihiyo,'' maana yake ni mtu asiye na elimu inayoeleweka.
Na kama vile ni sharia maalum watu hawa wote hujulikana kwa jina moja tu.

Sasa tuje kwa baba wa mababa labda kwa msamiati mpya utasema baba lao na hii ‘’lao’’ hapa imetumika kwa kutuniza.

Huyu ni Quisling.
Nani huyu Quisling?

Quisling alikuwa mwanajeshi katika jeshi la Norway wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 – 1945).

Quisling alishirikiana na Adolf Hitler kumwezesha kuingiza jeshi lake nchini kwake na kuikalia nchi yake Norway.

Kwa ajili ya usaliti huu wa taifa lake ndipo dunia ilipopata msamiati huu wa neno hili, ‘’Quisling,’’ ikawa mtu yeyote awaye yule atakaeshirikiana na adui wa nchi yake kwenda kinyume na kile ambacho nduguze wanakipigania kukipata akimtia nguvu adui anaitwa, ‘’Quisling.’’

Manazi waliikalia Norway mwaka wa 1940 kwa msaada wa Quisling na yeye kama ahsante yake akatunukiwa uongozi wa Norway.

Hakuna asiyejua ufisadi wa Wajerumani katika nchi walizozikalia wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia.

Mwaka wa 2011 nilialikwa Zentrum Moderner Orient, Berlin hii ni moja ya taasisi mashuhuri duniani ya utafiti.

Nilimuuliza mwenyeji wangu wanajisikia vipi historia hii ovu ya nchi yao inapofanyiwa rejea tena na tena.

Jibu alilonipa ni kuwa wao kama kizazi kipya historia hii inachoma nyoyo zao kwa fedheha lakini wanaithamini sana na inasomeshwa ili isipotee nia ikiwa historia ya wazee wao ibaki kama funzo kwa vizazi vijavyo.

Afrika ina mengi ya kujifunza katika historia ya dunia.
 
KISA CHA VIDKUN QUISLING

Naamini itawashangaza wengi nikiwaeleza kuwa jina la Jecha na jinsi Wazanzibari walivyoliingiza katika msamiati wao ni sawa na jina la Vidkun Quisling nalo pia lilivyoingia katika msamiati wa dunia nzima kwa vitendo sawa na alivyofanya Jecha Salum Jecha.

Mfano mwingine ni jina la Kihiyo kumithilishwa na mtu ambae hana elimu lakini akajifanya na kuwaaminisha watu kuwa kaelimika vizuri.

Leo mtu akikwambia mathalan, ‘’Asikushughulishe huyo ni Kihiyo,’’
mara moja unajua kuwa anakuambia usipoteze muda na yeye hana alijualo.

Mifano hiyo hapo juu nikianza na neno, ''Jecha'' maana yake ni mtu aliyebadili au kufuta matokeo halali ya kitu chochote kile ama iwe matokeo ya uchaguzi au hata ya mtihani.

Neno, ''Kihiyo,'' maana yake ni mtu asiye na elimu inayoeleweka.

Na kama vile ni sharia maalum watu hawa wote hujulikana kwa jina moja tu.

Sasa tuje kwa baba wa mababa labda kwa msamiati mpya utasema baba lao na hii ‘’lao’’ hapa imetumika kwa kutuniza.

Huyu ni Quisling.

Nani huyu Quisling?

Quisling alikuwa mwanajeshi katika jeshi la Norway wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 – 1945).

Quisling alishirikiana na Adolf Hitler kumwezesha kuingiza jeshi lake nchi kwake na kuikalia nchi yake Norway.

Kwa ajili ya usaliti huu wa taifa lake ndipo dunia ilipopata msamiati huu wa neno hili, ‘’Quisling,’’ ikawa mtu yeyote awaye yule atakaeshirikiana na adui wa nchi yake kwenda kinyume na kile ambacho nduguze wanakipigania kukipata akimtia nguvu adui anaitwa, ‘’Quisling.’’

Manazi waliikalia Norway mwaka wa 1940 kwa msaada wa Quisling na yeye kama ahsante yake akatunukiwa uongozi wa Norway.

Lakini Quisling hakuwa mjinga wa kukosa kutambua kuwa yeye hakuwa na madaraka yoyote.

Madaraka walikuwanayo wale waliomuweka kukalia kiti kile.

Hakuna asiyejua ufisadi wa Wajerumani katika nchi walizozikalia wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia.

Mwaka wa 2011 nilialikwa Zentrum Moderner Orient, Berlin hii ni moja ya taasisi mashuhuri duniani ya utafiti.

Nilimuuliza mwenyeji wangu wanajisikia vipi historia hii ovu ya nchi yao inapofanyiwa rejea tena na tena.

Jibu alilonipa ni kuwa wao kama kizazi kipya historia hii inachoma nyoyo zao kwa fedheha lakini wanaithamini sana na inasomeshwa ili isipotee nia ikiwa historia ya wazee wao ibaki kama funzo kwa vizazi vijavyo.

Afrika ina mengi ya kujifunza katika historia ya dunia.

[/QUOTE]Vidkun Quisling
Screenshot_20201114-132747.jpg
 
Sheikh Mohamed ulipotaja ZMO Umenikumbusha Prof.Kai Kresse katika kitabu cha "Swahili Muslim Publics and Postcolonial experience"
 
Brade...
Kai ni rafiki yangu kila akija Dar es Salaam tunakutana kubadilishana fikra.

Hii picha hapo chini nilimpiga New Africa Hotel mwaka jana ndiyo kwanza alikuwa kachapa hicho kitabu chake.

1605384368278.png
 
Hongera sana. Prof yuko vizuri sana.

Nimeona pia Prof Hamza njozi alitoa comments zake juu ya kitabu hicho
 
Back
Top Bottom