Kisa cha saccos kudidimia na kufa


Novatus

Novatus

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2007
Messages
331
Likes
2
Points
0
Novatus

Novatus

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2007
331 2 0
Saccos ni njia sahihi ya kumwokoa mjasiriamali wa kawaida. Mpango huu wa kuweka na kukopa unasaidia sana sana watu walio wengi.

saccos zilianzishwa nyingi lakini siku hadi siku zinakufa. Wanahisa walio wengi hawaelewi ni kwa nini zife wakati zinapoanzishwa zinakuwa na gawio linakuwa kubwa.

utafiti niliofanya katika Saccos zaidi ya tatu ni kuwa kifo cha ushirika huu kinaanza ambabo Benki zinaingilia SAccos hizi kama wadhamini au kuwaongezea mtaji. Kwanza kwakuwa Benki zinawekeza pesa nyingi kuliko ya wanachama wanalazimisha Saccos ziendeashwe na Wataalamu waliosomea Ushirika/uhasibu. Sina pingamizi na hili. ILA sasa Benki ndio wanaoajiri wafanyakazi hawa ambao wanajifanya ni waelewa waliobobea na zaidi ajira zinaenda kiundugu wala sio sifa halisi. matokeo yake wanaongeza mzigo wa gharama za uendeshaji, wengine wanakiuka misingi na kanuni zilizowekwa katika kukopesha na kurejesha. Wengine wananakiuka taratibu wanajikopesha mikopo mikubwa kama taasisi nyingine eti watakatwa kwenye mishahara.

Matokeo yake unakuta wanahisa baada ya mwaka wanaambiwa hakuna gawio. Iweje taasisi ikae na fedha yako millioni kumi isizae wakati imekuwa ikopeshwa? Jambo hili linawakatisha tamaa watu na kukosesha imani kwenye saccos

Ni wakati muafaka serikali iingilie kati kutatua jambohili au wanahisa wategemee pesa yao wakopeshane wasimamie wenyewe wataona faida ya ushirika huu

WanaJF tafadhali changia mada hii kwa faida ya watanzania
 
Elia

Elia

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Messages
3,442
Likes
5
Points
135
Elia

Elia

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2009
3,442 5 135
Una zungumzia hela na hilo ndio tatizo, sina utaalam na mambo ya pesa ila nitapenda nione wataaram watavyo changia. Ahsante kwa post
 

Forum statistics

Threads 1,236,572
Members 475,187
Posts 29,262,642