Kisa cha Rais Ali Hassan Mwinyi kipigwa kibao akihutubia

Wajameni hata uwe dini gani, sijawahi sikia maandiko au mafunzo yanayoongoza kukosoa wakubwa kwa vibao au bakora. kila andiko linasema mkubwa ahifadhiwe na kosa lake kuonekana kama kughafirika.

Hili la kibao hata iweje ni utovu wa nidhamu na laana kwa watu wanaobeba baadhi ya mistari bila comprehensive understanding of the bible or quran's context

i hope wisdom itasaidia ndani ya mafundisho kwani hata manabii wangekuwa wanaamua au ku-support physical encounters kila sehemu [except jihad] basi ingekuwa manundu tu
 
Nasikia hii hotuba alipewa tu ilikuwa tayari imeandaliwa na timu ya JK! Nadhani hili kofi lilikuwa maalumu kama zawaidi ya maulidi kwa JK! Lakini hata hivyo JK nadhani angelikwepa kama Bush alivyofanya Iraq! Au lilikuwa ghafla sana? Tuwekeeni yutube wakubwa! (this is with a light touch!)
 
Huyo kijana ni mzima kiakili lakini? Maana hili jambo si la kawaida kwa kweli. Uislam nao wahubiri subira. Kama ni mzima basi ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu na aadhibiwe vikali. Na hao walinzi kweli wanachekesha, wanakuwa kazini au wamelala!
 
sifikilii kama sababu ya mzee wetu kupigwa kibao ilikuwa ni kutamka neno la condom, nahisi kuna zaidi ya hilo,labda wasitueleze ukweli.
====

Au ndiyo maana mgeni rasmi, Rais Kikwete hakwenda?
Nchi hii ina mengi sasa hivi hata mtu huwezi kujua mtu yupi yuko kundi lipi. Ndiyo maana mtu anaamua kumpiga anayesema condom kuliko kumpiga anayezini!
 
Kwa mbinu alizotumia huyu jamaa sidhani hata jk kama angepona, labda kama walinzi wangemstukia mapema. Kipande kilichoonyeshwa kwenye taarifa ya habari jamaa alijifanya kama anataka kurekebisha microphone, kwanza ilionekana kama mzee Mwinyi alijiuliza huu ujio ni wa nini. Lakini jamaa aliposhika microphone mzee akaendelea na hotuba yake, ndipo alipopata nafasi nzuri ya kutekeleza azma yake. Na kweli lilimuingia maana hakuwa amejitayarisha, ila ukweli bwana mdogo kajichukulia laana. Ni sawa kama kampiga babu yake, mbali ya adhabu atakazozipata kwenye mkono wa sheria amejichukulia laana.
 
Hata kama hukubaliani na msimamo wake, lakini ni vema kuuheshimu. Personally sikubaliani na vitu kama abortion lakini I always strive to respect other people`s point of views. Right to make a choice. No body is a sole custodian of the truth.

Thats why nakataa vitu kama kadhi`s court kuviweka kwenye katiba inayotuhusu WATANZANIA wote..maana ni issues ambazo wengi hatuwezi kukubaliana mpaka mwisho wa dunia. Hivyo ni bora tuu kila mtu akaachiwa uhuru wa kuamua. Ya dini yawe ya dini. Ya kisecular yawe hivyo hivyo. Hapo tutaishi kwa amani na upendo.

Pole sana Alhaji.

Mahakama ya kazi na suala hili lina uhusiano gani? Usipojua neno ni bora ukanyamaza kwani utachanganya mambo bure. Suala la mtu binafsi kujichukulia sheria mikononi mwake ni suala la mtu binafsi na hatuvihususi vyombo ambavyo wahusika wake wanachukua sheria mikononi mwao na ndio maana hata jeshi la Polisi bado tunalitambua na kuliamini juu ya vitendo mbali mbali vya watendaji wake kama mauwaji, rushwa na kadhalika. Si vizuri kuzungumza mambo ya dini ya mwenzio kwa ubaya eti muumini wake katenda jambo fulani.
 
Kwa mbinu alizotumia huyu jamaa sidhani hata jk kama angepona, labda kama walinzi wangemstukia mapema. Kipande kilichoonyeshwa kwenye taarifa ya habari jamaa alijifanya kama anataka kurekebisha microphone, kwanza ilionekana kama mzee Mwinyi alijiuliza huu ujio ni wa nini. Lakini jamaa aliposhika microphone mzee akaendelea na hotuba yake, ndipo alipopata nafasi nzuri ya kutekeleza azma yake. Na kweli lilimuingia maana hakuwa amejitayarisha, ila ukweli bwana mdogo kajichukulia laana. Ni sawa kama kampiga babu yake, mbali ya adhabu atakazozipata kwenye mkono wa sheria amejichukulia laana.

Bwanawe, hata JK ingelimpata mbona kule Mwanza jamaa alimuingia na kumwangusha? Hizi nyingine ni nguvu za giza. Ona sasa nami naanza kuota mchana!
 
Sifikiri alifanikiwa kwa ajili ya nguvu za giza, ila alijiweka katika hali ya kutotiliwa mashaka. Na huu wingi wa vyombo vyetu vya habari kuna haja ya kuwa na utaratibu wa kuwa na mtu/watu maalum wa kurekebisha mic au taperecoder inaweza kusaidia tukio kama hili lisitokee tena.
 
Mhh!!!, hii hatari, kumpiga mtu, tena aliyekuzidi umri. Lakini nitajizuia kulaumu zaidi mpaka itakapotolewa ripoti kwa nini alifanya hivyo. Manake naweza kumlaumu moja kwa moja kumbe ni majnuni (kichaa).
 
Walinzi, angalau mmoja inatakiwa awe karibu sana na mlindwa, ama pembeni yake au nyuma yake na anapohisi mtu yoyote anaweza kuleta zali basi huyo mlinzi inabidi awe tayari tayari. Sasa huyo dogo anaenda hapo mbele na hakuna mtu amtambuaye na walinzi hawakukaa ktk attention stance? What ze hell? Usikute hao walinzi wenyewe wana vitambi na hawazidi hata 5 '4!
 
Mhh!!!, hii hatari, kumpiga mtu, tena aliyekuzidi umri. Lakini nitajizuia kulaumu zaidi mpaka itakapotolewa ripoti kwa nini alifanya hivyo. Manake naweza kumlaumu moja kwa moja kumbe ni majnuni (kichaa).

Kichaa gani anaenda kumfuata na kumpiga raisi mstaafu? Kwa nini kamchagua yeye na si wengine ukumbini? Ni wazi alikuwa anajua na kutambua Mwinyi ni nani. Hakuna cha insanity wala nini. Wanipe mimi tu huyo mtu kwa dakika mbili. Dakika mbili tu...no more than that.
 
Shughuli itaandaliwa na BAKWATA? lakini thats what you get if you get involved with that lot

halafu mwinyi huyu huyu wakati wa utawala wake alikuwa kimya wakati wa MABUCHA YA NGURUWE na vurugu zake

Ohh walimpa Mengi tuzo as if hakukuwa na waislam ambao wangepewa tuzo na BAKWATA
 
Kichaa gani anaenda kumfuata na kumpiga raisi mstaafu? Kwa nini kamchagua yeye na si wengine ukumbini? Ni wazi alikuwa anajua na kutambua Mwinyi ni nani. Hakuna cha insanity wala nini. Wanipe mimi tu huyo mtu kwa dakika mbili. Dakika mbili tu...no more than that.

Mkuu NN, nimesema nitajizuia kulaumu zaidi mpaka nipate ushahidi wa yaliyomfanya alifanye hilo. Kama kichaa angempiga mtu mwingine ukumbini hiyo isingekuwa habari kubwa hapa JF na huenda wala isingeletwa.
 
Nadhani kuna haja ya viongozi wetu kuiga mfano wa "General" Colonel Ghadafi... Body guards woote wa kike...

Hao wanawake watasaidia nini? Huyo Kadafi usikute anawadinya tu hao....hawana lolote. Hivi wale walinzi wake waliozipiga kule Uganda walikuwa hao wanawake? I don't think sooooooo....
 
Sitaki kabisa kuwa drawn katika alichokuwa anakizungumzia Mwinyi!! Hata rais kuna mengi anayoyazungumzia ambayo si wote tunayakubali. Sasa ikiwa rais anazungumzia jambo nisilolikubali, nipande jukwaani nimzabe?? Au nimzuie kuzungumza kwa kuwa mimi sikubaliani na anachosema?

Vipi Kiongozi mwingine? inabidi ajue kuwa haya nitakayoongea inabidi woote waliopo wawe wanakubliana nayo, vinginevyo naweza pigwa?

Hii ni failure ya security installations. Ni failure kubwa. Watu wameshajua kuwa ulinzi huwa ni dhaifu.

Naungana na wewe kuwa hapa la kutizamwa ni kitendo kibaya kilichofanywa na huyo jamaa na namna alivyoweza kutekeleza hilo.
Nashangaa na wale wanaohalalisha kitendo hicho kwani kama ulivyosema huwezi kujua nani atafurahishwa na nini kwenye hutuba.
Nashangazwa zaidi na wale wanaolivalia njuga suala hili kidini. Ni tabia yetu Watanzania jambo lolote linalowahusu Waislamu linapewa udini na kwa hili tayari mengi yamesemwa kuhusu uislamu kuhusiana na kitendo cha muumini mmoja. Suala la kuulizana hapa ni kuwa Mzee Mwinyi alikuwa katikati ya waumini wa dini ya Kiislamu na kama tendo lililofanywa lilikuwa la kidini basi hilo valangata lingekuwaje? halisemeki. Alichokisema Mwinyi kweli hakikubaliki na uislamu lakini uislamu hauelekezi hayo aliyofanya jamaa. Hiyo ni jazba yake binafsi na si ajabu pengine hata nyumbani ni mtu ovyoovyo.
Sasa kupachika tendo hili na uislamu nini maana yake kama si kitendo cha makusudi cha kuwatoa akili Waislamu wote? Nawaomba wale wenye tofauti za kidini kujizuia na tujadili kitendo cha utovu wa nidhamu kilichofanywa zidi ya Mzee wetu.
 
GT,
You have an issue with BAKWATA? Mengi alipewa tuzo kwa sababu alistahili. Au ulitaka atafutwe Mengi Muislamu?
 
Hata kama hukubaliani na msimamo wake, lakini ni vema kuuheshimu. Personally sikubaliani na vitu kama abortion lakini I always strive to respect other people`s point of views. Right to make a choice. No body is a sole custodian of the truth.

Thats why nakataa vitu kama kadhi`s court kuviweka kwenye katiba inayotuhusu WATANZANIA wote..maana ni issues ambazo wengi hatuwezi kukubaliana mpaka mwisho wa dunia. Hivyo ni bora tuu kila mtu akaachiwa uhuru wa kuamua. Ya dini yawe ya dini. Ya kisecular yawe hivyo hivyo. Hapo tutaishi kwa amani na upendo.

Pole sana Alhaji.

Sure, kumpiga kiongozi sijambo zuri hatakama hukubaliani na hoja zake. Ndio maana tupo hapa jamvini kupinga hoja na sio kurusha viatu au kuwachapa makofi viongozi wetu. Pole Alhaji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom