Kisa cha Rais Ali Hassan Mwinyi kipigwa kibao akihutubia

...kwa ujinga kama huu, ipo siku JK naye kwa anavyopenda kujichanganya, atakula kipondo!

...Mjinga kama huyo anayejidai kutumia kivuli cha uislamu kuonyesha ujahili wake kiasi cha kumdhalilisha Mtu mzima kama huyo, achilia mbali urais Mstaafu, ni kitendo kinachofaa kulaaniwa kwa nguvu zote!

Mkuu, nadhani hata hapo alijiachia sana sasa mtu akiamua kutake aim watamkinga vipi? Icadon hebu tusaidie mkuu?
 
Kwasababu zozote zile... ukweli utabaki pale ple, kumpiga kofi mzee Mwinyi tena mbele ya kadamnasi ni kitendo kisichofaa kutetewa hata kidogo, tunapaswa kukikemea kwa nguvu zote.
 
Kwasababu zozote zile... ukweli utabaki pale ple, kumpiga kofi mzee Mwinyi tena mbele ya kadamnasi ni kitendo kisichofaa kutetewa hata kidogo, tunapaswa kukikemea kwa nguvu zote.

Tatizo sio kupigwa Mwinyi peke yake, kupigwa yeyote ni kitendo kisichofaa, kuna namna nyingi za kutoa grievances sio lazima kuamua kuchukua sheria mikononi. Hata hivyo ni lazima tukubaliane katika kutokukubaliana. Siku zote watu wengine tunatend kudhani kuwa tuna haki ya ukweli, ya kwamba mitazamo yetu ni sahihi na wengine wote sio. Hapa ndipo tunapokosea, kila mtu lazima akubali pia wenzake wana haki ya mawazo. Mawazo yetu yasifanywe kuwa Dogma!
 
Wakuu hapa nachanganyikiwa kidogo. Habari zilizopo ni kuwa huyu kijana kaenda high table na kumzaba kibao Mzee kisha naye akavamiwa kama tulivyoona na kupokea kichapo kikali. sasa hizi habari kuwa kachukizwa na kauli ya matumizi ya kondom kwa waislamu zimepatikana kutoka wapi? Kesha hojiwa sababu za kitendo alichofanya? Mimi nadhani hili linaweza kupatiwa ufumbuzi baada ya mahojiano ya kina na kijana yule.
Vilevile ni ujinga kwa kumvamia na kumpa kipigo kijana yule akiwa tayari amezibitiwa. Tofauti iko wapi kati yake na hao wanaompiga?
 
sawa dini lakini ni kweli yeye hapo alipo si kavaa mivao ya western kwa nini na hizo nguo asivue akavaa ma rob kaa ya hao wenye msimamo mkali? ni swali tu.
 
Nadhani hili ni tukio baya kwa nchi yetu hususan katika siku ya sherehe kubwa kwa ndugu zetu waislam. Nimeona kwenye ITV saa mbili usiku huu, Jamaa amekwenda, hakuna aliyemstukia, Mwinyi akamwona na huenda alitambua kuwa jamaa hana dhamira njema... hata hivyo angefanyaje, hakuwa na ushahidi... na sijui angewa alert vipi walinzi au watu wengine. Kwa kawaida mlinzi hukaa nyuma ya kiongozi... jamaa akajifanya kama anainamia kushoto... Mwinyi akaendelea na hotuba... kufumba na kufumbua akampiga kibao cha Kelbu, ambacho kilimpata barabara mzee yule. Walinzi kustuka, wanaanza kusukumana na yule mhuni.

Hakika watu walitaharuki pale.. hususan Mzee Bob Makani ambaye alionyesha dhahiri kuogopeshwa na kitendo kile.
 
...Kibaka tu huyu, kweli kijana kama huyu ambaye Mzee Mwinyi anaweza kumjukuu anadiriki kunyanyua mkono wake kumchapa kofi? ...*%$"+@:^%$**&&$$zake huyu!!!!

...picha kwa hisani ya blogu ya drfaustine!

Wakuu hapa nachanganyikiwa kidogo. Habari zilizopo ni kuwa huyu kijana kaenda high table na kumzaba kibao Mzee kisha naye akavamiwa kama tulivyoona na kupokea kichapo kikali. sasa hizi habari kuwa kachukizwa na kauli ya matumizi ya kondom kwa waislamu zimepatikana kutoka wapi? Kesha hojiwa sababu za kitendo alichofanya? Mimi nadhani hili linaweza kupatiwa ufumbuzi baada ya mahojiano ya kina na kijana yule.
Vilevile ni ujinga kwa kumvamia na kumpa kipigo kijana yule akiwa tayari amezibitiwa. Tofauti iko wapi kati yake na hao wanaompiga?

supported;

sometime kuongea sana unaweza onekana mjinga, Mwinyi kaongea mbele ya waislamu, aliepiga kofi Mwinyi anaweza akawa mwislamu au sio! kinachoonekana ni kuwa waislamu ndio wanaompiga huyu jamaa! sasa Mwinyi hakuongea utumbo, kuna jambo lingine nyuma ya haya!

Kwa namna yeyote hakuna na haitatokea kutenganisha siasa, dini, maisha na asili ya kila siku ya mwanadamu. Kama Mwinyi aliongelea ukimwi, basi aliongelea kama Kiongozi anayejua ni kwa kiasi gani gonjwa hili linatumaliza.

Kama dini zingekuwa zinasaidia basi tangu mwaka 1981 waliopatikana na wanaothirika kwa ukimwi si wapagani!

Ya kaisari mpeni kaisari, Diamond sio msikitini though.
 
Ni kweli katika dini zetu matumizi ya kondom yanakwenda kinyume na maagizo ya Mungu, lakini hapa wamemwalika public figure ndio tatizo!. Ingawa Mzee Mwinyi ni Muislam na pengine anajua kuwa maagizo ya dini hayakubaliani na matumizi ya kondom, majukumu aliyonayo katika jamii yanamtaka ayatazame mambo katika upeo wa kiutawala wa kijamii. Kama angekuwa ni kiongozi wa kidini ambaye ameamua kuitumia hadhara ile iwe na kuwashawishi watu watumie kondom katika mapambano dhidi ya ukimwi, hapa ningeliona kuwa ni tatizo. VIongozi wa dini wanatakiwa kuongoza mapambano dhidi ya ukimwi, lakini kwa silaha waliyopewa nayo ni acha kufanya ngono nje ya ndoa. Tukumbuke Mzee Mwinyi ni mlezi sijui au cheo kinachofanana na hicho ktk mapambano dhidi ya ukimwi, kwa hiyo sio rahisi kutoa hutuba bila kuongelea eneo hilo. La msingi ni huyu ndugu na wengine wote wanaokerwa na hutuba za namna hii sehemu ya ibada wawe na moyo wa uvumilivu, na hekima pia inahitajika.
Binafsi nalaani sana kitendo kilichofanya na kijana huyu, ni udhalilishaji mkubwa kwa mzee wetu na ukosefu wa adabu!
 
Hujui kitu wewe na ni mgumu wa kuelewa....issue ni ngono haramu na sio uvaaji wa kondomu!! Unaweza kumdungua mke wako halal tena wa ndoa kwa kondomu.....tulia na acha kukurupuka!! Na zaidi ni kuwa kondomu zilikuwepo hata kabla ya ngoma haijaingia.......ukielewa hapa then utakuwa umeelewa tofauti ya binadamu na ng'ombe!!

Misimamo kama yako na huyu mpuuzi aliyemchapa kelbu Mwinyi ndio inafanya uislamu unaonekana ni dini ya kifedhuli. Again, kupigia debe kondomu sio sawa na kuhalalisha matendo ya ndoa nje ya ndoa.....kwanza ni waislamu wangapi ambao hawakuwahi/hawajawahi kufanya ngono kabla ya kuoa/kuolewa?? Wewe unavimada wangapi? Anza kuvaa kondomu, la sivyo utaiachi udhuni familia yako....

Acha unafiki.......

Wewe ulichikielewa ni nini? naona unanipinga na unaniunga mkono at the same time, hueleweki.

Halafu tafadhali chunga lugha yako.

Kuhusu waIslam wangapi ambao wanafanya dhambi hayo ni yao na si mafundisho ya uIslam. Usichanganye uIslam na makosa wanayofanya watu.
Taadab.

Sitovaa kondom kwa sababu sifanyi upuuzi na maisha yangu, sifanyi ngono haramu kama unavyofikiria. Na inabidi uelewe kuwa kutumia kondom sio dawa ya kuzuwia ukimwi. Labda mtengenezewe kondom za kuvaa mwili mzima, wazinifu.
 
Mkuu Icadon,

.........ukishamiliza kupiga box..........tunaomba uje utuwekee mavitus hapa........
 
Nimekasirishwa sana na tukio hili, nimekasirishwa sana na wanafurahia na kuchekelea tukio hili. Ali Hassan Mwinyi bado ni symbol ya taifa anastahili ulinzi, anastahili heshima na anastahili pongezi kutokana na kuhudhuria kwake mkutano kama huo na kusema ukweli kuhusu condom.

Walinzi wake ndio wanaotakiwa kuadhibiwa kwanza, na baadaye kumwadhibu aliyenda tukio hilo.
 
Kama kweli tunamheshimu mzee wetu huyu basi kichwa cha habari nacho hakimtendei haki " Mzee Mwinyi ALA KICHAPO"!! Hii ni haki kweli ?Hii ni issue kubwa kidogo kuandika heading kama hii hapa jamvini.
 
Ni kitendo kibaya na cha huruma kwa rais mstaafu wa Tanzania Ndugu Ally Hassani Mwinyi kupigwa kofi jukwaani wakati akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu leo. Je! ndio tuseme walinzi walikuwa wapi? Hainiingii akilini kusikia mtu tu kutoka katikati ya waumini kujifanya anarekebisha vipasa sauti na kumpiga Raisi wetu mstaafu kofi. Ndio tuseme angekuwa na cha moto angeweza kumuumiza au hata kumuua mstaafu wetu huyo tunayemtegemea kwa amani na ushauri wa nchi yetu. Walinzi wa viongozi kuweni makini. Hivi ni vitendo tunavyovisikia kwa nchi nyingine tusikubali vitokee kwenye kisiwa hiki cha amani yaani TANZANIA. Mungu ibariki Tanzania amani iendelee kuwepo.
 
Hii ni dalili kwamba nchi yetu inaelekea pabaya. Je angekuwa na cha moto ingekuwaje? Si ajabu sasa tungekuwa tunaongea mengine. Walinzi inawezekana walichapa usingizi.
 
......kwani mwinyi alikuwa anategemea nini kutetea condom mbele ya Taleban,ana bahati kapata kibao tuu maana ingekuwa kule kabul angechinjwa kwenye Stadium,naheshimu sana dini za watu lakini taleban nawaogopa sana maana unaweza kuhukumiwa kifo kwa kula kiti moto tuu au kunyoa ndevu tuu!
 
Sitovaa kondom kwa sababu sifanyi upuuzi na maisha yangu, sifanyi ngono haramu kama unavyofikiria. Na inabidi uelewe kuwa kutumia kondom sio dawa ya kuzuwia ukimwi. Labda mtengenezewe kondom za kuvaa mwili mzima, wazinifu.

Mkuu nakuheshimu kutokana na posts zako ila kwa hili umepotoka... kondom sio kinga ya VVU pekee na sidhani kama wewe ni mkamilifu...

Dunia duara baba
 
......kwani mwinyi alikuwa anategemea nini kutetea condom mbele ya Taleban,ana bahati kapata kibao tuu maana ingekuwa kule kabul angechinjwa kwenye Stadium,naheshimu sana dini za watu lakini taleban nawaogopa sana maana unaweza kuhukumiwa kifo kwa kula kiti moto tuu au kunyoa ndevu tuu!

Acha unafiki wewe clown Koba wewe, kusema unaheshimu dini za watu halafu unawaita Taliban. Mule ndani Mwinyi alienda kuongea na Taliban mule?

Kama wale ni Taliban kwa nini sasa walimgombania Taliban mwenzao anaepinga condom? Dullard!
 
Hiki kitendo kibaya sana. Ila wanasiasa wamezidi mno ku hang out na watu wa dini. Haya ni matokeo ya wanasiasa kuingilia majukwaa ya kidini.
 
......kwani mwinyi alikuwa anategemea nini kutetea condom mbele ya Taleban,ana bahati kapata kibao tuu maana ingekuwa kule kabul angechinjwa kwenye Stadium,naheshimu sana dini za watu lakini taleban nawaogopa sana maana unaweza kuhukumiwa kifo kwa kula kiti moto tuu au kunyoa ndevu tuu!

Talebani machoko tu mimi siwaogopi wala nini. Nenda kawaambie Ngabu kawatukana...
 
sifikilii kama sababu ya mzee wetu kupigwa kibao ilikuwa ni kutamka neno la condom, nahisi kuna zaidi ya hilo,labda wasitueleze ukweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom