Kisa cha Prof. Khigoma Malima na Sheikh Mavumbi, Uchaguzi wa 1995

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,054
2,000
KUMBUKUMBU ZA PROF. KIGHOMA MALIMA NA SHEIKH IBRAHIM MAVUMBI WA TABORA UCHAGUZI WA 1995

Radio ya gari yangu siku zote wakati wote ninapokuwa naendesha kituo changu ninachosikiliza ni TBC Taifa.

Leo ile kuwasha gari tu namsikia mtangazaji TBC Taifa anatangaza mkutano wa Kampeni ya CCM Tabora Viwanja Vya Ali Hassan Mwinyi na anasema kuwa Sheikh wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi atapanda jukwaani kusoma dua.

Mashaallah kama kuna kitu masheikh wetu wanakiweza kwa ufanisi wa hali ya juu ni kusoma dua katika shughuli za kitaifa.

Kwa hakika katika eneo hili wanastahili pongezi kutoka kwetu sote.

Mtangazaji anamtaja Sheikh Ibrahim Mavumbi Sheikh wa Mkoa wa Tabora kuwa anapanda jukwaani kusoma dua kabla ya mkutano wa kampeni ya CCM.

Jina hili la Sheikh Mavumbi kwangu ni maarufu.

Ghafla na kwa kasi kubwa jina la Sheikh Ibraim Mavumbi likanirudisha miaka 25 nyuma wakati kama huu wa uchaguzi mkuu wa vyama vingi mwaka wa 1995 ndani ya msikiti mkuu wa Ijumaa Tabora magazeti yalipoandika kuwa Prof. Malima atajitoa CCM ndani ya msikiti wa Tabora baada ya sala ya Ijumaa.

Wahariri wa magazeti takriban yote ukilitoa Annuur gazeti la Waislam, walikuwa wanachuki kubwa na Prof. Malima na kila wakinyanyua kalamu zao ilikuwa ni kumwandika vibaya Prof. Malima.

Magazeti ya siku hiyo yote yalikuwa yametawaliwa na habari za Prof. Malima kujitoa CCM Msikiti wa Ijumaa Tabora.

Waingereza wanamsemo wanasema, ‘’They had a field day,’’ hii maana yake ni kunufaika bila kutoa jasho na kuhangaika.

Magazeti walikuwa wamekipata walichokuwa wanakitafuta tena wamekipata kwa bei hafifu sana.

Kufika saa tano msikiti umejaa pomoni na nje watu wametandika misala Waislam wameitika taarifa za magazeti wamejitokeza kwa wingi kuja kumsikiliza Prof. Malima akijitoa CCM ndani ya msikiti wao wa Gongoni.

Haukupita muda gari ya polisi ikasimama mbele ya msikiti akashuka Sheikh Ibrahim Mavumbi na kuingia ndani ya msikiti.

Sheikh Ibrahim Mavumbi alikuwa Sheikh wa BAKWATA.

Siku ile nje ya msikiti askari wenye unifomu na wengine makachero walikuwa wametanda kuzunguka msikiti na wengine wakiranda mitaa ya jirani achilia mbali makachero waliokuwa ndani ya msikiti wenyewe.

Sheikh Mavumbi akaenda mbele kibla akachukua kipaza sauti akawatangazia Waislam kuwa Prof. Malima asiruhusiwe kuzungumza siasa ndani ya msikiti.

Waswahili tuna msemo, ‘’Hukuweko lakini malaika wako alikuwako.’’

Sheikh Mavumbi ile kulitaja tu jina la Prof. Malima msikiti wote ulilipuka kwa hamaki.

Kila mtu akisema lake.

Kwa kipindi kifupi pakawa na fujo na vurugu kubwa Waislam wameghadhibika pasi na kiasi.

Katikati ya kelele zile ikasikika sauti ya upole na sauti maarufu kwa wengi na hakuna asiyeijua sauti ile.

Ilikuwa sauti ya wito ikisema kwa upole, ‘’Salaa Nabi,’’ ‘’Msalieni Mtume.’’

Hakuna Muislama asiyejua maana ya wito huu kila aliyesikia maneno yale aliitika kwa Sala ya Mtume wakijibu, ‘’Allahu Maswali Wasalimaale.’’

Ghafla utulivu ukarejea msikitini ikawa ukiangisha pini utasikia kishindo cha kuanguka kwake.

Sauti ile ilikuwa sauti ya Mzee Bilal Rehani Waikela.

Muasisiwa TANU, mpigania uhuru wa Tanganyika na mtumishi wa Waislam toka ujana wake hadi pale sasa kawa mtu mzima.

Mzee Waikela akachukua kipaza sauti kutoka mikononi mwa Sheikh Mavumbi huku kamwelekea Sheikh Mavumbi akamuuliza, ’’Sheikh Mavumbi wewe nani kakuambia kuwa Prof. Malima atakuja hapa msikitini kufanya siasa?

Hebu angalia hapa.

Unamuona Prof. Malima humu msikitini?’’

Sheikh Ibrahim Mavumbi kinywa kikawa kimemjaa mate.

Anaangaza kote hamuoni Prof. Malima.

Hana la kusema.

Hakuweza kumtaja aliyemtuma kuja msikitini wala hakumuona Prof. Malima ndani ya msikiti.

Taratibu kwa unyonge akageuka kuelekea mlango wa msikiti na kutoka nje kwenda kupanda gari ya polisi iliyomleta pale msikitini kwa vishindo vya kumwaga vumbi.

Nimefurahi sana kuona kuwa Sheikh Ibrahim Mavumbi baada ya robo karne bado kashikilia nafasi yake ile ya Sheikh wa BAKWATA Tabora.

Hakika hii inaonyesha na ushahidi wa kuaminiwa kwake katika kutekeleza majukumu yake.

Kwa kweli Sheikh Ibrahim Mavumbi ni kiongozi wa kuigwa katika kuweza kuwatumikia Waislam wa Tabora kwa miaka yote hii na bila shaka kwa ufanisi mkubwa.
 
platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
8,700
2,000
Sheikh Mavumbi alishafariki miaka mingi. Fanya utafiti utagubdua kwamba huyu uliyemtaja ni mwanaye.
1600790022114.png

Mzee MS,
Huyu anayeonekana pichani anaweza kuwa makamo ya Sheikh Mavumbi unayemzungumzia?

Tatizo la Mzee wetu ni 'haraka' ya kuonyesha ubaya wa wengine au kuelezea jambo ili kutimiza matakwa yake.

Sasa umesikia jina la Mtu unayemshuku kwamba ndiye yule 'mbaya' wa kipindi kile zaidi ya miaka 25 iliyopita, tena kwenye redio hata picha hujaiona. Ingekugharimu nini kupiga simu mbili tatu tena kwa Watu unaowafahamu Tabora kabla ya kuandika ili kujiridhisha kuwa ndiye. Halafu jingine, hapa kuna Ally Mavumbi na Ibrahim Mavumbi, hata majina hayakukupa tahadhari kuwa huyu siye!

Angalia sasa umemfanyia dhihaka marehemu ambaye yupo udongoni miaka kumi sasa.

Kwa ambao tuliokuwa nao hapa JF kama miaka mitatu iliyopita Mzee MS alileta kisa cha bwana mmoja aliyekuwa anasema aliteswa na kudhalilishwa na jeshi la Polisi tena ndani ya vituo kwa kisingizio kuwa ni gaidi, ikaja kubainika kuwa ni tapeli anatumia hizo stori kupata huruma ya Waislamu ili apate pesa. Mzee MS aliipamba sana 'stori' ya huyo bwana tena akielezea madhila aliyoyapata kwa mbwembwe. Ni dhahiri waliompa hiyo taarifa wameshamjua,'ukishampelekea Mzee MS haraka ataruka nayo'.

Tuache hayo, nimekumbuka sana gazeti la Annuur. Kwa habari za gazeti lile namna zilizyokuwa zinaandikwa kwa 'kutia hasira' Waislam na nikiangalia namna ambavyo bado tunaishi Nchini kwa umoja basi hatatokea Mtu kutugawanya kirahisi. Nazungumzia mwanzo mwa miaka 2000 na mwishoni mwa 99'.

Mzee MS nitapataje nakala za gazeti hilo kila wiki. Wakati ule kila toleo nilikuwa nalinunua. Pia hata matoleo ya nyuma kwenye soft copy.
 
Arushaone

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
14,943

Nashukuru sana mkubwa kwa kumbukizi hii ingawa hukuimaliza yote kwa maoni yangu.

Labda kwa ajili ya muda wako au kwa kuogopa ila kiukweli naona kama una mengi zaidi ya haya ungeweza kuendelea, mfano kama Prof Malima alijitoa CCM akiwa wapi etc etc.

Ahsante sana.

Nakuaminia sana Mzee kwa historia
 
Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,054
2,000
View attachment 1577440

Platozoom,
Hakika yako makosa na nilipofahamishwa nimesahihisha.

Hii ni kumbukumbu kutoka kumbukumbu ya nyuma niliyopata kuandika kwa tukio la Sheikh Mavumbi.

Kwa ajili hii basi aliyehusika ni Sheikh Mavumbi ila yule alikuwa baba yake.

Hili limenogesha zaidi makala hii.

Sikuwa na haraka yoyote na hiyo picha niliiona baadae sana.

Wala sijamdhihaki marehemu.

Kuwa alileta taarifa msikitini ambazo yeye mwenyewe hakuwa na ithibati katika ukweli wake ni kweli.

Kuwa aliletwa msikitini na gari ya polisi ni kweli pia.

Kinachofurahisha kwa Sheikh Mavumbi "mtoto," nilipoona picha ni kuwa yeye kashika bendera ya chama.

Hili linaeleza maneno 1000.

Ikiwa umeumizwa nakutaka radhi ila wasomaji wengi wamefurahishwa na historia hii na maana yake katika jamii hasa baada ya kusahihisha na kueleza kuwa yule alikuwa baba na huyu ni mtoto.

Kuhusu makala ya yule mtu muongo alikuwa kapita kwingi akiaminiwa hadi kufika kwetu na hapo ndipo nilipomuona.

Haikuwa nimeandika habari zake nikijua kuwa ni mtu laghai.
 
Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,054
2,000
Sheikh Mavumbi alishafariki miaka mingi. Fanya utafiti utagubdua kwamba huyu uliyemtaja ni mwanaye.
Malyenge,
Nilifahamishwa kuwa huyu ni Sheikh Mavumbi "Mtoto" na yule alikuwa Sheikh Mavumbi "Baba," na nikafanya masahihisho.

Angalia hapo chini:

[21/09, 19:57]

Kuna mtu kaniandikia anasema Sheikh Mavumbi yule kafariki na nafasi yake BAKWATA kashika mwanae ndiye huyu niliyemtaja hapa.

Nipe ukweli tafadhali.

[21/09, 20:03]

Ni kweli.

Aliye sasa ni Sheikh Mavumbi Mtoto.

Sheikh Mavumbi Baba alishafariki.

Allaah Amrehemu.
 
Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,054
2,000
Nashukuru sana mkubwa kwa kumbukizi hii ingawa hukuimaliza yote kwa maoni yangu.

Labda kwa ajili ya muda wako au kwa kuogopa ila kiukweli naona kama una mengi zaidi ya haya ungeweza kuendelea, mfano kama Prof Malima alijitoa CCM akiwa wapi etc etc.

Ahsante sana.

Nakuaminia sana Mzee kwa historia
Arushaone,
Kweli yako mengi ningeweza kusema lakini sikusema si kwa kuogopa ila kila jambo lina wakati wake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom