Kisa cha Panya, Wakulima na Mbegu za Mpunga (Tozo, Wafanyabiashara na Watuamiaji)

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,417
19,441
Hapo sio zamani sana kulikuwa na jamii ya Panya iliyopenda sana kula mbengu za mpunga, hali ilikuwa mbaya sana kwa wakulima, panya wenyewe na hizo mbegu, sababu kutokana na wingi wa panya ilipelekea kupunguza idadi ya mbegu za kupanda hali iliyopelekea wakulima kufa kwa njaa na kupunguza nguvu kazi ya kuvuna mpunga ili kupata mbegu ambazo panya wangeweza kula jambo lililopelekea vifo vya Panya

Panya hawakuwa wajinga baada ya kuona hii hali wakaitisha mkutano na kushauriana wanusuru maisha yao.., Panya mmoja akasema, hawa wakulima sio maadui zetu, bila wakulima sisi wote tutakufa, bora kama tungeweza kupanda na kuvuna wenyewe tungefanya; ila tumikono twetu hutu tudogo hatuwezi, hivyo tufanyeje ili tuokoe maisha yetu?

Baada ya kufikiri sana mjumbe mmoja alikuja na wazo…, “Hivi badala ya kula mpunga, kwanini tusile mchele?, Mbegu moja ya mpunga ikipandwa inazaa mbegu za mpunga maradufu ambazo zinatoa mchele magunia, na sababu mchele haupandwi kwanini sisi tusile kile ambacho mkulima anakula yaani tugawane na mkulima na sio kummlalizia mkulima mbegu ambazo zitamaliza uhai wetu na wa mkulima". Basi wakaamua na ikawa kama walivyokusudia…, ingawa mkulima alikasirika kwa kero za panya kula mchele wake ila aliweza kula, kushiba na kupata nguvu za kupanda mpunga.

Tozo za Miamala, Wafanyabiashara na Watumiaji
Hivyo hivyo kwa Kisa cha panya ndio kisa cha hizi tozo za miamala, wafanyabiashara (makampuni/mawakala) na watumiaji…, Badala ya Serikali kutoza direct kwa kila mtumiaji jambo ambalo linapelekea kupunguza watumiaji, kwanini hata wasiongeze tozo kwenye faida/mapato ya mawakala na makampuni ? Kwa kufanya hivyo watumiaji wataongezeka, makampuni na mawakala wataongeza faida na serikali itakula kwenye faida na sio kwenye mchakato kabla ya faida…

 
Back
Top Bottom