Kisa cha nyumba ya nyasi kijijini chasababisha ndoa kuvunjika

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha 'Stori za Ghost' mtangazaji Ghost Mulee alisimulia kisa kimoja kilichohusisha wapenzi wawili ambao ndoa yao ya miaka mitatu ilisambaratika wakati jamaa alipeleka mkewe nyumbani kwao kwa mara ya kwanza.

Ghost alisimulia jinsi mwanadada alimshinikiza mumewe ampeleke nyumbani kwao upande wa Siaya na hatimaye akakubali na wakaabiri ndege kuelekea kijijini ambako jamaa alizaliwa na kulelewa.

Mwanadada huyo alisikitika sana kuona hali duni ya nyumba ambayo jamaa amejenga pale kijijini ilhali walikuwa wakiishi maisha ya kifahari jijini Nairobi.

"Jamaa amekuwa na mwanadada kwa miaka tatu. Wamekuwa wakiishi maisha ya kifahari na anaendesha gari kubwa.Nyumba yao imetengenezwa vizuri. Ni jamaa ambaye ana mazoea ya kujigamba wanapoenda mahali. Mpenzi wake alimwambia wamekuwa wakiishi Nairobi kwa kipindi kirefu na angependa waende kijijini. Waliingia kwa ndege na wakafika. Kufika kijijini Siaya mwanadada alishtuka sana. Jamaa ananyumba ya nyasi hajajenga. Mwanadada alipoamka asubuhi alimwambia kuwa mapenzi yao yameisha" Ghost alisimulia.

"Mwanzoni mwanadada alidhani ni mzaha lakini alipoamka asubuhi jamaa akamwambia kuwa hapo ndipo nyumbani ila anapanga kujenga. likuwa mara ya kwanza kupelekwa Siaya. Alisema haiwezekani wanaishi maisha ya kifahari Nairobi ilhali kijijini hajajenga. Hapo na hapo akaambia jamaa mapenzi yao yameisha na kila mtu akarudi Nairobi kivyake" Alisimulia Ghost.

Je, katika mahusiano yako hali hii ilishakutokea? Yapi maoni yako?

images (2).jpeg

Hii hali ni kuvumiliana, mwanamke ana nafasi kubwa sana kubadilisha tabia ya mwanaume. Kama huyo Dada angajipanga vizuri hayo makazi yangebadilika ndani ya mwaka, huyo Dada alikuwa na nafasi nzuri ya kumshauri huyo Jamaa namna ya kuboresha makazi ya wazazi wake.

Maisha ni kuvumiliana, kushauriana na kuelekezana pale palipo na kosa na siyo kukimbiana, tutangulize utu kwanza ndio baadae heshima na furaha hufuata.
 
Umechanganua kwa kina kabisa, kukimbia sio suluhisho la matatizo
 
Back
Top Bottom