Kisa cha Nabii Ibrahim na mfanano wa tukio la ajali ya morogoro watu kuungua kwa moto.

Bossless

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
1,381
2,892
Asallam alykum wapendwa ,kwanza nitoe pole kwa ndugu zangu wote waliopatwa kupoteza ndungu zao kwenye ajali ya moto huko morogoro na majeruhi mwenyezimungu awafanyie wapone haraka ili warudi katika majukumu yao ya kila siku.ishallah

Ajali ya jana imenikumbusha kisa cha Nabii Ibrahim (AS) baada ya kusikia kauli ya namba moja akiwaasa watazania waache kudhania kuwa kila alieungua alienda kuiba mafuta ,akasema wengine walikuwa wapita njia,wangine walienda kwa nia ya kuokoa ,wangine walikuwa wanashangaa tu wakajikuta katika majanga bila kutarajia hata Mimi nakubaliana na yeye kwa 100%.

Kisa chenyewe kipo hivi: baada ya Nabii Ibrahim kuongea na mungu kupitia maoni yake ya kitume alimuulize mungu kwanini kila unapoleta makharika,dhoruba kwa vizazi vya nyuma umekuwa ukiwagusa watu wabaya na wasiowabaya yani kharika likija au janga hukumba wazuri na wabaya wote twende. Mungu akamjibu swali lako zuri sanaa ila ntakujibu swali lako baada ya miaka hamsini,Nabii Ibrahim alishangaa sanaa ila akaona ngoja avute subira kama unavyojua watu wa zamani waliishi miaka mingi.
Ikapita Siku ,miezi ,miaka siku ikawadia kwakuwa Nabii Ibrahim na mifugo mingi siku hiyo alitoka malishoni akawa amejipumzisha chini ya mti mungu akamletea usingizi akawa amelala kwa uchovu kisha mungu akawaelekeza sisimizi waende kwenye kichwa cha Nabii Ibrahim kumng'ata na wengine akawa ewaelekeza kuwa wakae pale tu kwenye mti na wengine chini pembeni yake kisha mungu akamuamsha ghafla ,Nabii Ibrahim alivyoamka na kuona sisimizi wanamng'ata akaanza kuua wale sisimizi hakuishia hapo akawageukia wale wa kwenye mti akawaua na wa chini akawakanyakanyaga wakafaa wote.mungu akamuliza ee Nabii Ibrahim kunani hapo mbona unaua sisimizi kwa hasira? Nabii Ibrahim akajibu hawa sisimizi wameninga'ta ndo nimewaua mungu akamuliiza tena vipi hao ambao walikuwa mbali na we kwenye mti na chini wanakuhusu vipi ? Nabii Ibrahim akasema nilikuwa na hasira ndo maana nikaona niwamalize wote tu. Mungu akamkumbusha swali lake lile .akamwambia ninapo kasirika nakuwapa adhabu binadamu sijali aliekuwemo au asiekuwemo kama ulivyofanya we we hapo kwenye sisimizi umeua walikung'ta ana wasiokung'ata.

My take: tujitahidi kuwakumbusha wengine kuhusu kutokufanya yale ayakatazo mola kwani likaja janga halitokuacha litatukumba wote wazuri na wabaya. RIp wrote mliopoteza maisha.
 
Kwahiyo na wale wasio na makosa wakiadhibiwa ni sababu ya hasira za Mungu? ... Mungu naye anafikiri sawa na binadamu??
 
Back
Top Bottom