X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,607
- 1,839
Watani zangu Wamakonde wanatabia ya kuchangamkia majina ya vitu vinavyokuwepo mahali alipo au kufuatana na msimu. Enzi zile ilikuwa sio ajabu kusikia mtoto wa Kimakonde anaitwa 'Chipoku au Baichikeli au Koroboi siku hizi sio ajabu ukasikia Mama Ekchpi(Xp) au Choptiwea au Hadiwea, Mauchi au Chkriin au Kompyuta! Usishangae pia ukasikia kijana wa kimakonde anaitwa Laputopu.
Hata wakati ule wa magari yaliokuwa yakitoka japon(Ujapani) yalipoanza kuingia kwa wingi walikuwepo kina Mama Dachisan, Toyota, Nichani patiroo, Karinya n.k.
Kisa hiki ni cha kweli kabisa. Na kilitoke wakati nikiwa bado Paster. Mmakonde aliyeishi maeneo ya jirani na Kanisa letu alimua kumbatiza mwanawe. Wakati wa zoezi hilo likiendelea ukafika wakati wa kumchagulia jina mwanae, mazungumzo na Padri aliyekuwa akiendesha ubatizo ilikuwa kama hivi:
Padri: Ndugu yetu katika Kristu ungependa kumchagulia jina gani mwanao?
Mmakonde: (Kwa unyenyekevu kabisa na sauti ya upole) Namchagulia jina la "YECHU KRICHTU"!!(Yesu Kristo)
Padri: Hilo sio sahihi chagua lingine!!
MmakondeKwa sauti ya unyenyekevu bado) Nachagua jina la "ACHIKOFU"(Askofu).
Padri: Hilo pia sio sahihi, chagua lingine!!
MmakondeKwa sauti ya upole) Nachagua jina la "Fadha Bikira"

Mmakonde: (Kwa sauti ya kukata tamaa) Basi nachagua jina la "PADIRI NKUU"!!
Padri: Hilo pia sio sahihi chagua lingine au tukuchagulie?
Mmakonde: (Kwa sauti ya kukata tamaa kabisa na ghadhabu kidogo) Chacha nyinyi Wakrichto mna ubaguzi mbona wenjenu Waichilamu watoto wanaita Mwamedi kama ntume wao hawachemi kitu, mimi chitaki tena kumbatiza mwanangu bila ya majina hayo....!!!
Zoezi hilo likabidi liishie hapo ikiwa pamoja na mshangao kwa waalikwa na viongozi wa Dayosisi/Parokia husika