Kisa cha Mimi kugombea demu na Jini

Wa Lupatu na wa Nairoto

Kuna mmoja watu wengi wametoa ushuhuda ambao jamaa wa Msitu wa nyumbanitu anasimulia
Yule wa Iringa ndio watu wengi wametoa ushuhuda kuwa wanalijua eneo lile, ila kule nje ya nchi wanaopajua ni wachache!
 
  • Thanks
Reactions: T11
Ooh sijawahi kujua hii

Anayefanya ni mod au member yeyote?

Linakuwa na baraka za mods na mwenye uzi mhusika ama ukijisikia tu unaendeleza ilipoishia?
Ameona mambo yasiwe mengi akapokea kijiti, iliwahi kutokea kwenye stori nyingine pia, mwenye uzi wake alianza kuleta madoido jamaa akaamua kuumalizia na mambo yakawa fresh
Kwahiyo acha tu jamaa atuondolee arosto
 
Ilifikia hatua wateja wa hoteli wakimwona wanagongana.Anasema kuna kipindi waitaliano walirushiana bastola kwa sababu yake.

Siku moja akaitwa ofisini na msimamizi mkuu wa hotel.Ni mzee wa heshima zake ambaye wengine walifikiri pengine ana share kwenye ile hotel ya kitalii.Alimweshimu sana.Mzee akaanza kumtongoza.Anasema alimkatalia.Mzee akaendelea kumtongoza mara kwa mara akimpa zawadi mbalimbali kufikia hatua ya kutafuta kiwanja na kumnunulia.
Anasema alikasirika sana siku moja.Akarudi home amesononeka sana maana vibweka vya yule mzee vilimkera.Akalala akaota amepewa penzi tamu sana.Kisha akalalamika kwa lile jamaa.Akaambiwa tulia.
Kesho anafika ofisini yule mzee anamfata kwa kutembea ba magoti akimwomba msamaha na kumwomba aoendoke kwenye hotel yake kuwa atamlipa pesa yeyote anayotaka.Akashangaa sana ni nini kile.
Alipanda tax na kukimbia maana wenzie walikuwa wanamshangaa sana na kumuuliza maswali kibao.
Alipofika home akatafakari sana.Ghafla hodi ikagongwa.Meneja wa hoteli alikuja na begi fulani la ngozi akaambiwa ametumwa ailete.Akaondoka bila mazungumzo.Anasema alipofungua alikutana na US dollars mpya kabisa vibunda kama ishirini.Kwa haraka haraka aliletewa kama kiasi cha millioni mia tatu.

Alishangaa sana.Alipolala mpenzi wake akamwambia hataki tena afanya kazi yale ndio mafao yake.

Baada ya week alipigiwa simu mamake amelazwa mwananyamala.Alipokuwa njian tu mamake alifariki.Alilia sana.Mama kaondoka bila kula matunda yake.Wadogo zake walimwambia mama alikuwa anamswalia sana siku za mwisho kwa sababu aliona ana wakati mgumu.
Akawaza huenda alisababisha kifo cha mama yake.Alihuzunika mno.
Anasema aliporudi Dar hakutaka kurudi zanzibar akiamini yule mlinzi mwisho wake umefika.
Kwa muda kama mwezi aliokaa hakupata shida yeyote.Maisha ya home yalibadilika na kuwa ya kifahari sana.Alikarabati nyumba yao ya Kinondoni B na kumalizia na ya Mbagra.Akamnunulia baba yale Gari la matembezi na kumjengea nyumba nyingine

Mambo yalibadilika alipotaka kukumbushia mapenzi na mpenzi wake wa zamani.Anasema jamaa hakusimamisha kabisa mara zote walizokutana naye.Aliumia sana na akawa na kiu cha hatari.

Alikuja kukutana na Mfanyabiashara fulani kijana ambaye alikuwa na makazi ya kudumu kinondoni ila aliamia arabuni Oman kufanya biashara.Wakapendana ila walipotaka kutest mitambo jamaa hakufanikiwa.Anasema yule kaka alipata matatizo na mikosi mfululizo hata kurudi tena Oman hakuweza.

Hii ilimchanganya sana.Mwaka mzima ukapita pasipo kupata huduma yeyote ya mjegejo.Anasema alikuwa na hasira mno.
Siku moha baba yake mzazi alimwita akamwambia anataka kumuoza kwa kijana mmoja mtoto wa mzito.Anasema akaingiwa udadisi kutaka kufahamu zaidi juu ya habari zile njema.Anasema baba yake alipanga kuwakutanisha kesho yake.
Alilala akiwa na furaha sana.Ila asubuhi ikawa mbaya mno na ya huzuni.Baada ya mzee wake kufariki akiwa anaswali swala ya alfajiri msikitini.

Alilia sana.Wakazika salama.Na baada ya siku mbili kijana alijitokeza kumsalimia.Anasema alimpenda sana kijana mkarimu na mwenye maisha mazuri.
Ila baada ya siku kadhaa walianzisha mahusiaono.Kijana akapata matatizo makubwa sana akapata ajali na kuvunjika kiuno.
Ilkawa mwisho wa habari.

Alijiona mwente mkosi mno.Alilia sana .Alipolala aliota katokewa na yule Mtoto wa amitbachan anamwabiwa yote haya umeyaka.

Alistuka akiwa na maumivu makali ya kichwa kiasi kwamba alishindwa kutoka nje wala kufanya lolote.Ndugu zake walimkimbiza hospitali ila hakuonekana na ugonjwa wowote.
Alilazwa kwa week nzima wakiamini kuwa anaumwa sononi.

Anasema alipata mateso makali mno akilala.Yule kiumbe alikuwa anampigisha push up kama adhabu ya kumsaliti.Aliumwa misuli mno.
Akasema hamna shida bora nitubu kabla hajapoteza damu zingine.

Akaandaa siku akaingia ndani akalia sana huku akisema la azizi nisamehe.
Akasema usiku akamtokea akasema nimekusamehe!
Ntarudi
Embe tueleweshwe kidogo hii stori Nani mhusika wa hii stori. Mbn naona chenga cheng
 
Wadau jambo la kushangaza sana leo asubuhi yule dada amenipigia simu. Ni miaka zaidi ya 8 sikuwahi wasiliana naye.leo amepiga simu asubuhi hii kunisalimia. Anasema amenikumbuka sana. Namuuliza upo wapi hajataka kujibu.

nimeshangaa sababu tulipotezana kitambo sana kwa mawasiliano.mimi namba ninayotumia sikuwahi badilisha kwa zaidi ya miaka 15 yeye alipotea tu hewani akawa hapatikani.leo ndo amenipigia. Sikumtambua mpaka alipokutambulisha. Nmeshindwa elewa imekuaje.
yupo humu JF ameona uzi wako akakukumbuka ila jiandae maana Mzee KHERI yupo nae anakufuatilia atakutatua marinda this time around
 
Moderator mkianza kuruhusu watu wafanye huu uhuni kutakuwa na migogoro mingi sana humu JF. Huu uzi wa huyu aliyeandika hapa. Please tabia hii ikomeshwe otherwise muwe mnashirikiana naye. Nlishatoa taarifa naona mmenyamaza tu.


Baada ya kupewa masharti ya kutokunywa pombe na kufanya mapenzi kabla ya ndoa anasema alishtuka sana!

Maana mrembo huyo alikuwa mpenzi wa Amarula sana tu.Alikuwa anapenda kunywa amarula akiwa kwenye mapumziko yake,hasa nyakati za jioni pia kusikiliza nyimbo za Kicongo.Na alikuwa anapenda sana nyimbo za Koffi Olomide.Wimbo wake kipenzi ulikuwa Kisanola.

Kuhusu sharti la pili nalo ilikuwa mtihani mkubwa sana kwake.Kwa sababu kwa umri wake ule wa miaka 23 alikuwa tayari keshafahamu mapenzi na anaijua raha ya sex.Alikuwa hawezi kukaa mwezi pasi kupanda Boat kwenda Dar kwa mpenzi wake kukaza bolt na alikuwa na matumaini kuwa wangeyajenga na mpenziwe ili arudi Dar weekend kufanya lolote ili wayajenge.
Alilia sana.Ila akaondoka kurudi home,alipiga moyo konde na kujisema kuwa Mungu atamvusha.Sio siri akisimama kujitazama na chain yake ya gold alizidi kuvutia.Alitamani kuivua ila akikumbuka yule mzee alivomla tigo alishindwa.Ghafla akapitiwa na usingizi bila kula wala kuoga.
Anasimulia kuwa alipolala aliona ametokea kwenye sauna moja nzuri sana.Maji ya moto matamu na harufu ya manukato mazuri ilimpa faraja na furaha ya ajabu.Anasema ghafla wakatokea mabinti wawili na matray mawili.Moja lina sabuni ya maji lingine lina taulo safi laini sana hajawahi kuona popote pale duniani.
Kwa matabasamu mazito na bashasha walimtoa kwenye sauna mfano wa mtoto mchanga kwa kumuita jina lake halisi.'Usiogope binti karibu sana', anasema hakustuka sana kwa sababu alishaanza kuzoea viroja.Mmojawao alikuwa na asili ya kichina na mwingine kiarabu.Anasema alipelekwa kwenye bafu akaogeshwa kwa muda mrefu huku wakimsifia kwa urembo wake.Anasema alipigwa na bumbuwazi ghafla baada ya kuletewa sahani iliojaa chakula baada ya kuogeshwa.Nywele zake nzuri natural za kishombe shombe zilipakwa mafuta na kukaushwa kwa mashine anasema kama za salon ila nzuri sana.
Baada ya kula akapelekwa chumba cha masaji.Akalala kifudifudi na kuanza kufanyiwa masaji ambayo hajawahi kupata.Anasema alijisikia raha mnoo.
Ghafla mabinti wakatoweka na 'bwana mkubwa akatokea'.Hili lilikuwa lile jini mlinzi alilopewa na ustaadh.
Anasema alikuwa kafanana sana na mugizaji fulani wa movie za kihindi mtoto wa Bacchani jina alisahau.
Anasema akaona kama mbwai na iwe mbwai akataka kukimbia.Jamaa akamshika bega lwa upendo akawa kama anaishiwa nguvu na kujiskia hali fulani ya usingizi.Akamwambia asiogope hatomdhuru,atamlinda na kumpenda.

Alichohitaji ni uamnifu na usafi.Kuanzia siku hiyo atamtreat kama mmewe halali mpaka pale atakapo olewa.Jamaa alikuwa handsome sana,Kifua cha mazoezi na surwali ya lineni.Marashi yake yalikuwa mazuri sana.Binti akajikuta anamlalia kifuani na kulia kwa kugugumia.Ghalfa akajikuta kalala kitanda cha sita kwa sita akiwa mtupu.Anasema hakuwa na hiyana.Jamaa alimwandaa kisawa sawa akampa mapenzi matamu mnoo.Baada ya mbilinge nzito liliolopelekea mashuka ya satin kuchomoka akapitiwa na usingizi.


Akaamka saa sita mchana.Alistuka sana akaoga haraka haraka na kwenda kazini.Kuhusu kukuta ute,hilo usiulize makofi polisi.Ila alijikuta kavaa pete nzuri ya uchumba yenye kidani cha rangi ya dhambarau.

Kwa mshangao alipofika kazini meneja hakumuuliza kwanini kachelewa zaidi ya kujichekesha tu.Wenzie wote walimshangaa kwa upekee aliokuwa nao siku ile yani alikuwa na mvuto fulani amazing.Mmoja wapo alimtania kuwa siku ile alifanana na Priyanka Chopra kabisa,yule miss world wa India.Anasema alicheka sana.Alijiskia mwepesi mno na mwenye amani.

Rafiki yake aliyempeleka kwa Ostadh alipotaka kujua kinachojiri anasema hakutaka kuzungumzia kabisa.Anasema muda ulimbia mno.
Akarudi home.Akakuta sofa jipya,jiko jipya kila kitu kipya ndani.Alistuka mno nusu azirai.Ghafla simu yake ya kiganjani ikaita.Akaitazama na Neno 'La azizi' lilitokea akasema hakupokea ila simu ikaendelea kuita kama mara 3.Ghafla sms ikaingia.
Alipoifungua ilisema," La azizi ahsante kwa mahaba ya jana.Nimekupa zawadi ndogo sana,utainjoy yaani". Japo mwisho alinalizia kimasihara kama kigogo wa Tweeter anasema alijiskia raha saana.Sababu ndani kulipendeza mno.
Kuanzia hapo ikawa kama kaposwa rasmi.Akifungua wallet anakuta pesa.Akilala tu ni gemu kali matata sana.Akiamka usafi ushafanywa n.k
Baada ya mabadiliko yale makubwa kwenye maisha yake anasema alinawiri sana na kuikubali hali yale.Alipendeza mno kiasi kwamba usumbufu kwa wanaume ukazidi maradufu.

Itaendelea....
 
Ni mpuuzi mmoja anayetafuta umaarufu wa kipuuzi kupitia nyuzi za wenzie.
Tena ukome kuniita Mpuuzi while huna kifua cha ustahimilivu.Uzi kuhamishwa tu umeleta maringo.Alafu usifikiri umaarufu wa mtandaoni ndio kila kitu bro,wala siutafuti na mie nimekushinda ukongwe kama ni swala la umaarufu ningeusaka siku nyingi sana.Acha kudeka deka

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom