Kisa cha mbwa wa Manzese na mbwa wa Oysterbay

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,203
157,376
KISA CHA MBWA WA MANZESE NA MBWA WA OYSTERBAY:- Mwalimu Julius Nyerere

“ Ndugu zangu watu wa Dari Salama ebu nisikilizeni; kulikuwa na mbwa wawili, mmoja wa Manzese na mwingine wa Oysterbay. Ikatokea siku moja mbwa wa Manzese akatembea hata akafika Oysterbay.

Kwenye moja ya nyumba za huko Oysterbay akamwona mbwa mwenzake aliye ndani ya geti. Mbwa yule wa Manzese akasogea getini huku akimshangaa mbwa wa Oysterbay.

Mbwa yule wa Oysterbay alinenepeana huku manyoya yake yakiwa yameteremka hadi machoni.

Mbwa wa Oysterbay naye alimshangaa mwenzake wa Manzese. Mbwa yule wa Manzese alionekana kukondeana huku masikio yake yakiwa yameteremka hadi shingoni. Mbwa wa Oysterbay kwa mshangao akamwuliza mwenzake wa Manzese;

“ Hivi nawe ni mbwa kama mimi?!
“Naam, miye ni mbwa kama wewe.”
Alijibu mbwa wa Manzese.
“ Sasa mbona umekondeana hivyo, njoo humu ndani kwa bwana wangu nawe uwe kama mimi.”
Mbwa wa Manzese akajibu;
“ Lakini wewe umefungiwa, mwenzio niko huru!”

Kwa hisani ya NGULI wa JamiiForums
 
Fundisho zuri sana kwa maendeleo ya nchi na jamii ~ be first to reply~
 
Hahhahahaaaa Bujibuji nitasema neno baadae
 
Back
Top Bottom