Kisa cha maisha yangu:- Mchungaji ndie aliyesababisha nighairi kuoa na amenifanya kanisani nikuone mbali

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
5,767
12,982
Unajua kwanini HUWA SIKUBALIANI NA KUOA KABISAAA...

Sababu ni hiii 👇👇

Mwaka 2015 nilikutana na binti wa kichaga Facebook.

Tulianza urafiki na baada ya muda mrefu tukaingia uchumba.
Nilimuahidi kumuoa na kuthibitisha hili nikawa close na familia yake.

Alikua anaishi na dada ake mjini Dsm.

Alikua anakuja sanaa kwangu mpaka akahamia kabisa.

Alikua anafanya Kazi kwenye ofisi moja ambayo ni makao makuu ya dhehebu moja la kanisa kubwa sanaa hapa Tanzania.
Na ni dhehebu ambalo mimi nasali kwalo.

Huyu dada alianza kubadilika ghafla,
Ikawa kila siku akirudi kutoka job anaanza kufuta sms (kabla ya kulala lazima akague simu yake anze kufuta sms)

Nilimpenda sanaa, nikawa namchora tu.
Tabia ikaendelea, akapata mimba.

Kuna siku nilimuhoji mbona unaenda clinic sijawahi sikia ukiniambia nikusindikize, alinijibu "niliona nisikusumbue haina haja"

Wakati wa mimba ikiwa na miezi 3 kuna siku alirudi kachoka balaa.

Alirudi akaoga na kulala direct.

Akasahau kukagua simu yake.

Niliona nimsaidie kukagua.

Nikagundua anakulana na mchungaji wa dhehebu langu.

Huyu mchungaji namjua vizuri, na nilimjua vizurii kipindi hicho yeye ni muimba kwaya (kabla hajaenda kusomea uchungaji) mimi nikiwa nasoma kipaimara.

Kwahiyo nimekua nikiwa namuona na muda mwengine alikua akitufundisha kuimba (kipindi cha sikukuu za watoto kanisani).

Nilisachi nikaona wanavyoo chat na kusifiana juu ya mastaili yao..

Iliniuma sanaa.

Nikarudisha simu na kunyamaza.

Maisha yaliendelea nikijua kabisa mwanamke mwenye mimba yangu na niliyepanga kumuoa anagongana nje na mchungaji.

Miezi ilipita akajifungua.

Nilikua na wasiwasi juu ya mtoto ila nashukuru Mungu mtoto alifanana na mimi.

Alivyojifungua kuna siku tena nikasearch simu yake, nikakuta bado Wana chart na safari hii mchungaji alikuwa akiniponda kichizii..

Alitumia matusi mengi tu..
"Kwanini umezaa na huyo falaa?"
"Unakubali kishoia akupe mimba?"

Na mengine mengiii.

Pia nilichuna.

Siku ya siku ikafika nikamuomba tukapime ukimwi.
Nilifanya hivi baada na mimi kuanza kumchunguza mchungaji na kuambiwa ni kiwembe balaaa.

Anakula sanaa wake za watu kanisani kwake huko.
Akiwa muimba kwaya alimaliza wanawake wa kwaya zoteee.

Majibu yalitoka mwanamke ameathirika na mimi na mtoto ni wazima.

Siku ile ile nilirudi home nikachukua nguo zangu na mwangu nikakimbilia home.

Sijui huko nyuma kilitokea nini, maana nilitupa line zotee na huyo mwanamke hapajui nyumbani ila mimi najua ndugu zake wengi.

Kuna siku nikiwa kazini dada ake alinifata akanililia sanaa "naomba muokoe mdogo angu anakufa kwa mawazo""

Nilikaa chini nikamuhadithia yotee na kumpa print out za chatting ya mdogo ake na mchungaji (nili save screen shots zao zotee).

Nikamjibu asijali, ye aendelee na maisha yake na kifupi anisahau.

Na akijaribu tu kwenda ustawi kudai mtoto basii mimi nitaenda mahakamani kufungua kesi ya udhalilishaji na kutaka kuniambukiza ukimwi kwa makusudi (nina ushahidi wa screen shots).

Dada mtu aliniomba nisifanye hivyo.

Dada mtu aliendelea kuwasiliana na mimi mpaka kuna siku akampa mdogo ake niongee nae.

Alivyomaliza tu nilihisi kama kuna kitu kimenijaa rohoni, nilitupa ile line na kununua mpya.

Na Kazi nikaomba kwengine (Mkoani) hivyo Dar nikahama.

Kwasasa naishi na mwanangu (ana miaka 5).
Ukoo wotee wa mama ake hawajawahi kunitafuta.

Niliwaaambia nyumbani "ole wake mtu atafutwe halafu amwambie niko wapi na nafanya nini""

Nashukuru Mungu life linasonga.

Huu ndio mkasa ulionitokea mwaka 2015 na ukanifanya nighairi kuoa.

Huyu mdada nilimpenda sanaa.
Sikuwahi kupenda kama nilivyompenda.

Nilijitoa hasaa kwake ila alishindwa kuthamini juhudi zotee.
Huwa namuonaga kama muuaji.

Mchungaji huwa namuona sanaa anavyo trend social media.
Huwa najiulizaga "HIVI AKIWA PALE MADHABAHUNI NA KUTAZAMA WAUMINI NA KUONA WALE WANAWAKE ALIOWAVUA NGUO, huwa ANAJISIKIAJE??""

Mbaya zaidi baada ya kupata Kazi niliomba ruhusa ya kwenda kusoma.
Nikawa nasoma chuo fulani hivi ambacho wachungaji wa dhehebu langu nao husomea chuo hicho.

Sasa vile unafiki nilioukuta chuoni,
Vile tulivyokuwa tunagombania mademu na wachungaji.
Vile wachungaji watu wazima (waliokuja chuo kujiendeleza) nilivyokua nawaona wanatembea na watoto wakike wadogo kabisa (form 4 levers - Certificate students)

Niliona kweli wachungaji ni wapuuzi sanaaa.

Yaani mchungaji mtu mzima hasa anagongana na binti mdogo kama mwanae Tena sometimes porini..!!

Kuna mmoja huyu ndio alitia fora....
""Alikuta wanafunzi wanaangalia porn za kibongo zilizovuja huko mitandaoni, akaja kuniomba mimi nimtafutie, kisa najua sanaa computer..!!""

Halafu kesho huyu mchungaji asimame madhabahuni anihubirie "acha uzinzi""

Maisha ya chuo yanifanya niwaone wachungaji waajabu kumbe.
Nilishuhudia visa vingi sanaaa za wachungaji.

Roommate wangu alikua anatoka na mama mchungaji chuoni.
Mama mchungaji alikua anampa conditions atafute guest za mbalii huko (ahame wilaya kabisa).

Siku ya siku nilikutana na yule mama mchungaji DSM akiwa na gari yake yupo na familia (mume + watoto) akanipa hi na kupiga gia..!!!

Nikajiuliza "mama mchungaji, Tena ameolewa halafu ana cheat..!!??""

Kipindi niko mtoto nilikua nikimuona mchungaji madhabahuni nilikua nahisi Mungu kashuka.
Niliwashimu sanaa, kumbe holaaaa..!!

Sasa kali zaidi...
Kuna kipindi kulikua kuna uchaguzi wa kugombea uaskofu.

Nikamtania yule mchungaji aliniomba X agombee..
Alinijibu "Usijaribu kuja kugombea uaskofu, kule ni kurogana tuu na unafiki mtupu". Alinihadithia mengi juu ya mchakato wa kumpata askofu, nikabakia duuuh..!!!

Kwasasa niko Mkoani nafanya yangu na kuhusu kuoa na kupenda SIKUTAKI HATA KUSIKIA.

Nyie endeleeni kuoa na kuwachangia nitachanga ila mimi kuoa HAPANA.

Kwasasa nikitaka maziwa napata then hakuna haja ya kufuga Ng'ombe.

#YNWA
 
Pastors are human being like you,don't relie to their faults, carry your cross, they will carry theirs'.
Aliyegongana jana na dada ake peter leo anakuja kumuhubiria Michael aache uzinzi.
Madhabahuni ni sehemu takatifu bro.

Unajua kwanini Musa aliambiwa avue viatu ndio aingie kwenye kile kijiti cha moto?

#YNWA
 
If you want perfect pastors, tell angels to preach you,if all people are innocent ,why then attending to churches?
Imani YAKO hujengwa na watu.
Ndio maana tunaenda msikitini kupata mawaidha na kanisani kuhubiriwa.

Sasa kwanini watende kinyume na wanayohubiri?

#YNWA
 
Alaaniwe amtegemeae mwanadamu.....kijana shida yako ni moja tu.. you have put all your trust to people. Binadam ambao sio Mungu wala malaika. Hakuna mkamilifu hata hao wachungaj ni binadamu kama ww tu na huanguka dhambini hivyo huhitaji toba na rehema za Mungu mara kwa mara kama bado utaendelea kuweka matumain yako yote kwa binadamu basi utachelewa sanaaa na hakuna faida utapata. Kila binadamu ni dhaifu na shetani karuhusiwa kutujaribu sote ni kuomba rehema ya Mungu tu usiingie dhambini. Hata ww si mkamilifu ukiljjua hilo huwez mshamgaa huyo dada kwa kukucheat maana nae si mkamilifu kama huyo mchungaji. Kama umeamua kuachana nae sawa lakini usitoke povu ooohh hutaoa milele sijui nn maisha ya ndoa yanataka uvumilivu sanaaaa leo huyo kakucheat utaenda kwa mwingine atakucheat tena utaacha wangapi???????
 
Back
Top Bottom