Kisa cha mafisadi na utamaduni wetu.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745
Kama kuna utamaduni basi kilichotokea kuhusiana na vyama vya Upinzani ni kuungana baada ya kuona wamepata siri za mikataba ambayo ni ya uhakika na wakiamini pindipo ikimwagwa kwa wananchi basi wataiezua CCM kama makuti yanayovuja ambayo yanahitaji kubadilishwa kwa haraka kama si hivyo nyumba italoa na kuzamisha kila kilicho ndani.
Jambo la ajabu viongozi wengi wa upinzani ni kutoka katika mizizi au ni mbegu za CCM zaidi ya yote hayo wameshindwa kuifahamu kuwa CCM ni problem proof ingawa kuna wengine utawasikia wakisema CCM tunaijua sisi.
Upinzani hauwezi kuwaondoa CCM hili nililisema kitambo kwenye topiki flani,na ninachozidisha sasa ni huu ufisadi ambao umeonekana umo ndani ya Serikali ya CCM,kitakachofanywa ni kurekebishana tu na kupanguliwa na kupangwa upya hakuna atakae fukuzwa wala kupelekwa mahakamani,mmeona kwenye mali asili tumepangua na kupanga upya.
Wengi wetu ni majeshi hivyo tunafahamiana na nyie mnaopiga makelele kana kwamba mmeona mwizi basi wafukuzaji na wakamataji ni sisi au ni sisi kwa sisi na kama mjuavyo teke la mama kuku haliumizi kifaranga.
CCM itadumu milele yaani mpa mwisho wa dunia msije mkajaribu kutaka kutumia nguvu mjue mtaumbuka na ndio utakuwa ndio mwisho wenu,ila kubalini tuende hivi hivi tu kubanana banana kupigiana mayowe ila pindipo mkijidai mna ubavu basi hakuna mswalie mtume.
 
Back
Top Bottom