Kisa cha kweli - zawadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa cha kweli - zawadi

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Yona F. Maro, Dec 5, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Dec 5, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  DIBAJI
  Ni kawaida kwa watu kuvutiwa zaidi na simulizi za kusisimua zinazohusu maisha ya watu wengine. Ziwe ni simulizi za kweli au za kutunga, uzoefu unaonesha kuwa hadithi hizi zimekuwa zikibadilisha tabia na maisha ya watu kwa namna mbalimbali lakini, ni hadithi chache tu zinazopatikana kwa urahisi. Nyingi zimeandikwa kwa lugha za kigeni hasa Kingereza, Kifaransa na Kigiriki. Na mpaka sasa hakuna hadithi inayoelezea uzoefu wa maisha ya kweli wa kijana wa kitanzania anayeishi na Virusi Vya UKIMWI (VVU) ambalo ni janga kubwa kimaisha linalokabili vijana na jamii yote kwa ujumla.

  Ndugu msomaji ni nadra sana mtu kufanikiwa kubadili misukosuko ya maisha yake kuwa zawadi kwa jamii yake. Ugumu huo unatokana na ukweli kuwa wengi tunahisi si ustaarabu kwa maswala au matatizo yetu binafsi kujulikana na watu wengine. Hata hivyo ipo baadhi ya misukosuko binafsi ya kimaisha ambayo hatupaswi kuwa wachoyo kuisimulia kwani kufanya hivyo ni kuinyima jamii zawadi ya kujifunza, na changamoto za kimaisha, na kuifanya ikose upeo wa kukabiliana na changamoto hizo. Kwa mantiki hiyo, ‘’maisha ya kila mmoja wetu yawe ya raha au karaha, ni zawadi kwa wengine iwapo historia yake itawekwa bayana’’.

  Hilo ndilo linalotokea katika riwaya hii - ’’Zawadi’’. Hiki ni kisa cha kweli na cha kusisimua juu ya maisha ya msichana Zawadi Salum. Binti huyu anazaliwa na kupokewa kama zawadi na wazazi wake, muda si mrefu Zawadi anakosa thamani kwenye familia yake na kugubikwa na matatizo makubwa ya kimaisha. Kwa ujasiri wa hali ya juu binti huyu akiwa na umri mdogo anamudu kupambana na matatizo mbalimbali na kuyageuza maisha yake kuwa zawadi kwa jamii.

  Simulizi hii ni ya moja kwa moja na imegawanyika katika sura sita nazo ni; ’’Ndoto Yangu’’, Usiku wa Uchungu’’, ’’Kufifia kwa Ndoto Yangu’’, ’’Zawadi nikajitoa Zawadi’’, ’’Imani Yangu ikaniweka mtegoni’’, Maisha Yangu, Zawadi kwa Jamii’’.Mgawanyiko huu ndio unaojenga kisa, mkasa na tamati ya simulizi hii, aidha kila sura inaambatana na mafunzo maalum yanayopambanuliwa kwa maandishi ya mlalo na kufunikwa kwa kivuli chepesi.

  Hii ndiyo Zawadi kutoka kwa Zawadi,’’Hakuna zawadi iliyo kuu kuliko zote duniani zaidi ya mtu kukuepusha na hatari dhidi ya uhai wako’’
  Kwa Angell
  Na wote wenye kujithamini

  NDOTO YANGU
  Kama ilivyo kawaida ya viumbe vyote, nami haikuwa dhamira yangu kuzaliwa. Lilikuwa ni kusudio la wazazi wangu na mapenzi ya Mola wangu mimi kuwemo ulimwenguni humu. Hiyo ilikuwa tarehe 12 Machi, 1981, nilipozaliwa nikiwa mtoto wa tano kati ya watoto nane wa familia yetu ambayo kipindi hicho ilikuwa ikiishi Old Shinyanga. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwani alinifanya kuwa kiumbe ndani ya kisiwa cha amani na utulivu na kuwa mtoto ndani ya familia ya maziwa na asali.

  Ndiyo, nilizaliwa kwenye familia iliyokuwa inajiweza kimaisha kutokana na cheo na kipato cha kuridhisha cha baba yangu, kipindi hicho alikuwa ni mmoja wa makapteni wa jeshi mkoani Shinyanga. Hakika, nilikuwa mwana kwa baba na mama kwa malezi mazuri niliyopata mara tu baada ya kuzaliwa, nami nikachochea furaha ya familia yetu, nikatia hamasa penzi la wazazi wangu na kuichangamsha nyumba yetu. Pengine kilichovutia zaidi ni vile nilivyochukua haiba na asili za wazazi wangu, baba msukuma na mama chotara wa kiarabu. Kwa jinsi hii nikatokea kuwa pambo machoni, lulu mioyoni na faraja nafsini mwao, nao wakaniita ZAWADI.

  Miaka mitatu baadaye sote tulihamia Kawe Dar es salaam na huo ndio ukawa mwanzo wa kulijua jiji, raha na karaha zake, jehanamu na pepo ya Tanzania. Haikuwa bahati mbaya kuhamia Dar, ilikuwa ni matokeo ya baba kuhamishwa kikazi kutoka Shinyanga. Hapa maisha yakazidi kupendeza na kwa neema ya wazazi wangu mwaka 1988 nikaanza darasa la kwanza katika shule ya msingi Kawe na kuwa mmoja wa watoto wachache nchini kupelekwa shule mwaka huo. Sikulazimishwa kusoma, shule niliipenda mwenyewe. Ukweli ni kwamba katika miaka ya awali shuleni nilipaona kuwa mahali pazuri pa kujichanganya na kucheza kwa furaha na wenzangu. Baadaye shule ikatokea kuwa sehemu muhimu katika fikra zangu, hii ni baada ya kuhamasishwa kuwa pasipo elimu sitapata kazi na nitakufa maskini. Sikupenda umaskini, nilipenda maisha mazuri na hivyo nikawa na ndoto, ndoto iliyochochewa na jamii iliyonizunguka, ndoto ya kufanya kazi kishujaa na kuvaa kijasiri.

  Naam! Ilikuwa ndoto ya kuwa kama baba yangu – ndoto ya kuwa mwanajeshi. Hapakuwa na kazi nyingine niliyoiona ni bora kwangu zaidi ya kuwa mwanajeshi, nilivutiwa sana na mavazi na ukakamavu wa kijeshi. Niliamini kuwa mwanajeshi ni kila kitu kwa sababu nilikuwa nikipata kila kitu nilichohitaji kutoka kwa baba yangu. Sikuwa na shaka juu ya kuwa mwanajeshi, niliamini kuwa hilo linawezekana kwani baba yangu ndiye alikuwa dira yangu na jamii ya wanajeshi iliyotuzunguka ndiyo iliyokuwa hamasa yangu. Wakati huo nilikuwa mwanajeshi kifikra na kimazingira, na nilihitaji tu muda ufike ili niwe mwanajeshi kamili.

  Ushauri kwa wazazi/jamii
  Mtoto anapoonyesha ya kwamba anataka kufanya nini katika maisha yake ama kwa matamanio au kwa vitendo (kwa mfano kuwa mwalimu, mwanajeshi, uchoraji, uimbaji n.k) ni jukumu la wazazi kumsaidia ili aweze kufikia ndoto/matamanio yake. Wazazi tuwe na tabia ya kuzungumza na watoto/vijana kuhusu matamanio yao ya baadaye. Na kuwashauri ipasavyo.

  Ushauri kwa Vijana
  Vijana wawe na tabia ya kujiwekea malengo na wawe na mikakati ya kujiandalia maisha ya baadaye: kwa mfano kujiwekea lengo la kuwa mwanajeshi, mikakati inayotakiwa ni kujilinda na vishawishi na tabia ambazo zinaweza kuleta madhara (marafiki wnye tabia mbaya, kuwa na tamaa ya pesa na kutamani maisha ya hali ya juu kuliko uwezo wako) ambayo yanaweza kukufanya usfikie ndoto yako.

  USIKU WA UCHUNGU
  Nilipokuwa nikitazama tabasamu na bashasha za baba na mama niliamini kuwa huo ndio utaratibu wa maisha wa siku zote. Kamwe sikufikiri kuwa upendo uliochanua kati yao ungekuja kunyauka na kuathiri mwenendo mzima wa maisha yetu. Laiti watoto wote tungelijua hili, tungekuwa tunawajibika kuchochea na kupalilia pendo la wazazi wetu. Hata hivyo ‘’ thamani na umuhimu wa kitu chochote huwa hakifahamiki mpaka kitu hicho kinapotoweka’’.

  Dalili mbaya za kumomonyoka kwa familia yetu zilianza rasmi mwaka 1990 wakati huo nikiwa darasa la tatu. Mama na baba walikorofishana na kwa hasira mama akarudi Shinyanga. Baada ya mama kuondoka nilipaswa kusitisha masomo na kukosa baadhi ya mitihani kwa sababu tu hakukuwa na mtu mwingine wa kufanya kazi za nyumbani alizokuwa akizifanya mama. Katika umri mdogo wa miaka tisa Zawadi nikafanywa mama wa familia. Kwa bahati nzuri baada ya miezi mitatu mambo yalitengamaa, kheri ikatawala shari na mama akarudi nyumbani kuendelea na maisha ya kifamilia kama ilivyokuwa awali.

  ‘’Mambo yalibadilika’’, Ilikuwa ni mwaka 1992, mwaka wa kukumbukwa katika maisha yangu ndipo nilipoona hasa thamani na umuhimu wa pendo la wazazi wangu. Mwaka huo penzi la wazee wangu lilitoweka tena na familia yetu ikaparaganyika na kubadili kabisa matamanio na matazamio ya maisha yetu. Mama yangu, akiwa mke mdogo kati ya wake watatu wa baba yangu, alitengana tena na baba kwa sababu ambazo sijaweza kuzijua mpaka leo hii, akaenda kuanza maisha yake binafsi na kuniacha nikiishi na baba pamoja na wadogo zangu na kaka zangu wawili wa mama mwingine.

  Mwanzoni sikuwa na mashaka sana, niliamini siku si nyingi mama angerudi nyumbani na kuendelea kuishi nasi tena. Hata hivyo mambo yakawa kinyume na matarajio yangu kwani, yalipita masaa, siku, wiki na hata miezi pasipo mama kurudi nyumbani. Kipindi hicho nilikuwa binti wa miaka 11 ambaye kutokana na malezi niliyokwishayapata niliweza kufanya kazi mbalimbali za nyumbani ikiwa ni pamoja na kupika na kuwaangalia wadogo zangu. Ingawa sikujua kisa cha baba na mama kutengana, niliweza kukumbuka kuwa hilo halikuwa jambo jipya kwa baba yangu. Kabla mimi sijazaliwa, alishakuwa na wake wawili kabla ya kumwoa mama yangu na akatengana nao.

  Katika mwaka huo ndipo nilipopata tabu ya kuishi na ndugu wa mama tofauti na kuathiriwa na ndoa za wake wengi mitaala kwani, chuki za mama zetu zilikuja kusababisha kaka zangu kunibagua mimi na wadogo zangu wa mama mmoja. Zawadi nikawa haramu mbele ya ndugu zangu wa damu! Licha ya kuwaonyesha upendo, kwa kuwapikia na kufanya shughuli zote za nyumbani, kaka zangu walinisimanga kuwa si mtoto wa baba na kunichukulia sawa na mfanyakazi wa ndani tu. Upendo na malezi mazuri ya baba nayo yalififia mara tu baada ya baba kutengana na mama. Shule ikaanza kuwa ngumu, baba hakutujali tena kwa pesa za matumizi wala za vitabu na madaftari. Mbaya zaidi, nyakati fulani baba alituacha bila pesa ya chakula. Maisha yetu yakapinduka, yakaijeruhi ile ndoto yangu na kutokomeza matarajio yangu ya awali.

  Maendeleo yangu kimasomo yakaporomoka, sikuwa tena na mtu wa kunionyesha upendo wala kunihimiza kusoma, achilia mbali wa kuninunulia vifaa vya shule. Njaa na kazi za nyumbani vikanifanya kuwa mtoro, na shuleni pakawa si mahali pema tena kwangu, paligeuka kuwa sehemu ya kebehi na dharau dhidi yangu. Nilianza kutofautiana sana na wanafunzi wenzangu, sikuwa na sare nzuri kama zao na sikuwa na furaha kama wao, – wenzangu walinicheka na kunipuuza. Katika mambo ambayo yalinikera sana katika maisha haya mapya ni tabia ya kaka yangu ambaye alinizidi umri kwa miaka saba, kunidhalilisha kijinsia mara kwa mara kwa kunishika kwa nguvu sehemu za siri. Nilijaribu mara kadhaa kumueleza baba juu ya tabia hiyo lakini hakuniamini. Laiti ningelijua kuwa nini kingefuatia baada ya tabia hii, pengine ningeweza kujizatiti kukiepuka kitendo cha kikatili alichonitendea.

  Ilikuwa ni usiku mmoja mwaka 1992, siku hiyo nilikuwa mimi, mdogo wangu na huyo kaka yangu. Wadogo zangu wawili walikwenda kwa mama na baba hakuwepo nyumbani. Haikuwa kawaida kwa kaka yangu huyu kupika chakula lakini siku hiyo alifanya hivyo, tulikula chakula na baada ya hapo kila mtu akaelekea chumbani kwake kulala. Ilipofika muda wa kama saa saba usiku hivi, nilishituka nilipomwona kaka yangu ameingia chumba tulichokuwa tukilala mimi na mdogo wangu wa kike. Haikunichukua muda kujua jinsi kaka alivyoweza kuingia chumbani kwetu bila hodi, ni dhahiri kuwa aliweza kupitisha mkono wake kwenye wavu mbovu wa dirisha la pembeni ya mlango na kuweza kuufungua kwa kulivuta komeo lake. Ghafla, alinisogelea kitandani na kuniziba mdomo kwa nguvu kisha akanitisha kuwa nikipiga kelele ataniua. Alinivua nguo zote na kunibaka hadi alipomaliza hamu yake yote, yote haya aliyatenda pasipo mdogo wangu kushtuka.

  Na siku hiyo ikawa ya kwanza kuingiliwa kimwili katika maisha yangu kwa kubakwa na ndugu yangu wa damu. Zawadi nikawa nimepoteza usichana wangu, nikawa takataka kwa kutothaminiwa na wazazi wangu hata kufanyiwa kitendo cha kinyama katika umri mdogo wa miaka kumi na moja. Licha ya maumivu makali niliyoyapata, nilivumilia pasipo kumweleza mtu yeyote kwa kuwa nilimwogopa sana kaka na baba alishaonyesha kutojali malalamiko yangu hapo kabla. Nilikosa amani kwa kumhofia kaka na kuugua kimya kimya kutokana na maumivu makali yaliyotokana na ukatili huo. Na usiku huo wa uchungu ndio ulioanza kuandika historia ya uchungu katika hisia zangu.

  Kaka angekuwa hajanizidi sana kiumri asingeweza kunitisha na kunibaka. Yeye alikuwa na miaka kumi na nane na mimi nilikuwa na miaka kumi na moja. Baada ya kubakwa sikujithamini tena, umakini wangu katika kujitunza ukaanza kupungua kwa sababu nilijua nisingeweza kuifuta historia. Familia yetu isingevunjika, baba na mama wangenilea vizuri, wangenilinda na kaka asingepata fursa ya kunibaka. Kama kusingekuwa na chuki ya kifamilia kwa sababu ya baba kuwa na mke zaidi ya mmoja, kaka yangu asingenichukia hata kufikia hatua ya kunibaka.

  Ushauri kwa Wazazi
  • Mara nyingi, ndoa zikiwa imara, familia pia itakuwa imara na watoto watafuata msimamo huo.
  • Ni muhimu wzazi washikamane, wapendane ili kutoa mfano bora kwa familia nzima.
  • Ndoa inapovunjika hasa katika familia ya wake wengi, watoto wote wasikilize na baba na mama wengine waliobaki kuhusu malalamiko ya watoto.
  • Wazazi wawe na tabia ya kuzungumza na watoto wao ili waweze kubaini matatizo kabla hayajajitokeza.

  Ushauri kwa Vijana
  • Wasichana mnapoona kuna dalili za kubakwa (kushikwa sehemu za siri, ****** matiti hata kubusiwa bila ridhaa yako) toa taarifa kwa wazazi/walezi. Wasipowasikiliza au kukupuuza toa taarifa serikali za mitaa na polisi.

  Kwa Vijana wa Kiume
  • Waheshimu dada zao na jamii ya kike inayowazunguka.
  • Waelewe ya kwamba madhara ya kubaka yanaweza kupelekea mbakwaji kupata mimba au UKIMWI au vyote viwili kwa pamoja. Pia anayebaka anaweza pia kuambukizwa UKIMWI kama aliyebakwa alikuwa na tatizo hilo. Pia ki-sheria anayepatikana kisheria na tendo la kubaka anapewa kifungu cha maisha

  ITAENDELEA
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2

Loading...