Kisa cha Kweli: Pale mtu wa kawaida unaposhindwa kutumia fursa iliyo jitokeza ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Star wa Hollywood

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,299
2,000
Salam ziwafikie wana MMU wote,

Leo nimeona nije kuwacheki wadau wa MMU na kuwapa kisa cha dada mmoja maarufu sana Hollywood anaitwa Sharon Stone.
Upweke noma sana, hakuna shujaa mbele ya upweke au penzi,
Penzi ni pacha wa upweke, huzuni na furaha.
Mapenzi yanapo vamia roho ya mtu lazima atii amri hata awe maarufu au shujaa au mwenye nguvu kiasi gani.

Huyu mrembo Sharon Stone alivamiwa na upweke ndugu wa mapenzi, basi ghafla alijisikia kutafuta mpenzi kwenye mtandao maarufu unaoitwa BUMBLE App, hii ni sehemu ya kutafuta wapenzi (dating app), akafungua account yake kwa jina lake kamili bila kujificha.

Kutokana na urembo, utajiri na umaarufu wake hyu mrembo, watumiaji wa Bumble app hawakuamini kwama kweli mrembo kama huyo anaweza kutafuta mwenza mazingira ya kawaida kama hayo, wakasema isiwe tabu tunamripoti kwa mods, fasta ma-snitch roho mbaya wa kitaa wakatuma malalamiko kibao kwa uongozi wa Bumble app wazuie(block) hiyo app sababu kuna tapeli anatumia utambulisho usio wake.

Majamaa yakasikika yakitema sumu PM kwa mods "Hatumtaki afungiwe tu, asituchoshe na misongo yetu ya mawazo.
Kibaya zaidi anatumia utambulisho wa Star mkubwa wa Hollywood".

Uongozi wa Bumble ukaona isiwe tabu waka-block account ya mwanamama mrembo Sharon Stone.
Mrembo Sharon akastuka kuona roho mbaya ipo hadi huku uzunguni kama uswahilini kwa dada Sky Eclat ?,
Basi ngoja niwalalamikie huko twitter.
Akatuma ujumbe wa kuwaeleza Bumble na kulalamika hivi hiyo site yenu ni ya watu fulani pekee?
Nilikuja kwenye mtandao wenu lakini mmeifunga account yangu".

Bumble fasta wakamrudisha star ili wavune wateja wengi zaidi.

Sasa nikajiuliza mimi na watanganyika wenzangu wale wazee wa kutembelea ganda la ndizi, mteremko, au wazee wa kitonga tuilikuwa wapi hatukutumia hii fursa?

Fikiria tu mastaa wetu hawa fakero wa Bongo movie au Bongo Flava wa kike wakiweka account za namna hiyo wanatafuta mpenzi na wabongo wakijua si huo mtandao utazidiwa na mzigo?

Angalia mfano wa account za Aston Villa zilivyo vamiwa na watanganyika kisa Mbwana Samatta kajiunga na timu yao?!

Mrembo ni kikongwe sasa ana miaka 61 lakini urembo wake utadhani anatoboa 35 hivi.
Nikajiuliza zaidi yule kijana wa kibongo alioa mbibi wa miaka 60 juzi juzi alikwama wapi? Kwanini asingejiwekeza kwa huyu bibi wa Hollywood?

Nikakumbuka mapenzi ni kipenda roho haya angalii sana umri na kipato, anachokipata baharia toka kwa yule bibi sisi wengine wote hatujui, laiti tungepewa anachopewa wengi huenda tungekata roho kwenye ile mechi ya wakubwa.
Jiulize kwanini nyuki dume anaenda kumpanda malkia wao huku akijua mapema kabisa nikimaliza mchezo tu nakufa hapo hapo, na bado jamaa anaenda kujitoa muhanga?
Ujue huo utamu wa naniliu na malkia wako hauna mfano, unaonja mara moja tu maishani mwako, kama ukibaki hai ukawajulisha wenzio kunaweza kutokea ugomvi wa kuuwana familia na kutokomeza familia yote kisa kugombea utamu.


Hii chini ni orodha ya filamu alizo shiriki:

 

kijana wa leo

JF-Expert Member
Nov 28, 2011
2,800
2,000
Kosa la kwanza sio kosa, Bali kurudia kosa, ngoja nimuwahi naweza kujikuta naamia marekani kimasihara sihara hivi hivi....
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,299
2,000
Jamani mbona mzee kabisa ndio unasema anaonekana kama ana miaka 36 huyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanasema Beauty is in the eye of the beholder.
Yaani mtu mmoja anacho ona ni kizuri au kinavutia kinaweza kisionekane hivyo machoni pa watu wengine.
Nakubali kabisa mtazamo wako kwamba anaoneka mzee sio wa 35 hivi.

Mimi nimeona anaonekana kijana zaidi kuliko umri wake, kama vile yupo mid 30s kuelekea 40, kumbe bibi mstaafu.
Enzi zake alitingisha sana hasa kwenye filamu ya Basic Instinct (1992) alionekana kama sex symbol.

Dada mmoja alirusha post akisema kama wewe upo bumble basi sisi tulio salia hakuna matumaini kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom