KISA CHA KWELI: Mwanaume aliependa mlemavu wa macho na kumuoa

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
23,025
2,000
Mimi nilipata tatizo la macho wakati nipo kidato cha tano mwaka 1995 baada ya kupata ajali ya gari na kichwa changu kugonga kioo cha mbele kutokana na kutovaa mkanda na kupelekea vioo kuingia kwenye macho yangu,

Mume wangu nilikutana nae wakati nipo kidato cha nne alikuja kwenye mahafali yetu sababu yeye ni dereva wa gari na alivyoniona alinipenda japo mimi sikumfikiria na alivyosikia nimepata matatizo ya macho akafanya jitihada za kupanga karibu na nyumbani kwetu ili awe ananiona na alifanikiwa na tukaanza kuwa marafiki wa kawaida na ilikuwa mwaka 2000 baada ya muda akasema anataka kunioa nikamuuliza 'Mimi mlemavu wa macho sioni unadhani ndugu, marafiki zako watakuelewa?
Mwaka 2002 mimi nilipata mimba ya mtoto wangu wa kwanza na ikapelekea Baba kunifukuza na kwenda kuishi na mwenzangu (Mume Wangu) na hali haikuwa nzuri pia sababu ya dini Baba yangu alikuwa hataki nibadili dini sababu Mwanaume aliyenipa ujauzito alikuwa Muislam"
Mariam Issa Mindu [HASHTAG]#LeoTena[/HASHTAG]
[HASHTAG]#MapenziMubashara18[/HASHTAG]"Mwaka 2003 mwezi wa pili nikajifungua mtoto wangu wa kwanza, mwaka 2007 Baba yangu alifariki wakaja ndugu zake kunifariji sababu mume wangu alikuwa safarini na mwaka 2008 Baba yake alifariki ikabidi arudi Tanzania ili kuendelea na maisha yetu,
Mwaka 2010 tulikaa na Mume wangu kuwaza tutaishi maisha haya ya bila ndoa mpaka lini na tukaamua kufanya maamuzi ya kwenda kwetu Bukoba kwa Baba yangu mkubwa ili kufanya michakato ya ndoa, kule kijijini walikubali lakini ndugu zangu wa mjini wakagoma hivyo itabidi tutulie na kufika mwaka 2012 mwezi wa 6 tulifunga ndoa na ilifanyika [URL='https://www.instagram.com/explore/tags/leadersclub/'][HASHTAG]#LeadersClub[/HASHTAG]
na tukaanza maisha ya ndoa rasmi na mpaka sasa tuna watoto watatu na kwenye ndoa huu ni mwaka wa sita na kwenye mahusiano huu ni mwaka wetu wa 17." Mariam Issa [HASHTAG]#LeoTena[/HASHTAG][HASHTAG]#MapenziMubashara18[/HASHTAG][/URL]
 

Attachments

McRiyckeel

JF-Expert Member
Jun 21, 2017
570
1,000


Ujue kama wewe unaweza kuona kimwana kwa picha kina churaa alafu ukakutana nacho kimwana kumbe tofauti unaamua kumpotezea lakin mm siwez kumwachaaa
mm nikiona chura tu namchezea af namrudisha kwenye maji...........
 
  • Thanks
Reactions: Lee

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom