Kisa cha kutimuliwa Job Ndugai Uspika na utawala badala ya kutimuliwa na Wabunge

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,406
7,188
Tangu mama kuingia madarakani kwa bahati mbaya ya kufa kiongozi mpendwa Tanzania magufuli amekuwa hana political base kwa hivyo amejibainisha kama mtetezi wa kupata madaraka wanawake.

Tunaweza kusema baada ya kutofautiana na spika na Spika kujidhalilisha kwa kuomba kinyonge msamaha kwa jambo la kawaida tu mama akamshukia kama mwewe kwa lengo la kumtimua akijua nafasi bila shaka itaenda kwa naibu wake ambaye ni mwanamke😂

Ndugai amekuwa anatumia madaraka yake vibaya kwa kujipendekeza kwa Serikali na kufanya unafiki mara kwa mara hadi kusahau kama bunge ni mhimili huru hauwezi kuamrishwa na serikali kwa maswala ya nguvu zake yaliyobainishwa kikatiba.

Ukikumbuka enzi za Spika Sitta Serikali ilipata shida kila ilipojaribu kumlazimisha bunge lisishughulikie mambo ya ufisadi kama yale ya richmond na kadhalika. Sitta alitumia nafasi yake kuisimamia vema serikali hadi wakati mmoja kufanya waziri mkuu kujiuzulu.

Kwa upande wake ndugai alionyesha kua kibaraka wa Serikali na kufanya mambo ya kinyume na utaratibu kama vile kuweka wabunge wasiyokua na chama bungeni. Ni wale wa viti maaluum wa chadema waliyofoji na kujipeleka bungeni kisha kufukuzwa na chama chao na ndugai akaapa kuwabakiza bungeni licha ya kufukuzwa uawanachama na chama chao.

Mzoea vya kunyonga haweze kula vya kuchinja. Ndio maana ndugai baada ya kutoa maoni yake kuishambulia serikali kwa kukopa ovyo na rais kuonyesha hasira hadharani Ndugai akasahau kama ni uhuru wake kutoa maoni na kwamba cheo cha uspika uteuzi haumhusu Rais bali wabunge. Ndugai akanywea na kupeleka barua ya kujiuzulu kwa katibu wa ccm badala ya katibu wa bunge😂. Huyo ndio Job Ndugai. Hakika hakuwa spika bora.
 
Back
Top Bottom