KIsa cha kusikitisha..kweli hii serikali ni feki watu sio wawajibikaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KIsa cha kusikitisha..kweli hii serikali ni feki watu sio wawajibikaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Dec 22, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,419
  Likes Received: 19,726
  Trophy Points: 280
  Mwokoaji Abed Abdalla, alisema said baada ya kukaa katika mti huo zaidi ya saa tatu bila msaada wowote, alikusanya vijana na kutafuta kamba ili waweze kumuokoa.Alisema baada ya kutafuta kamba ndipo aliamua kujitosa kwenda kumuokoa huku wengine wakiwa wameshikilia kamba hiyo, aliyokuwa amejifunga kiunoni ili aweze kumuokoa."Sisi kama wananchi tuliamua kujitolea kumuokoa mwenzetu, na tulipiga simu polisi, zima moto lakini hadi sasa hawajafika hii inaleta taswira gani hatuoni maana ya Serikali,''alisema Abdalla.

  Hata hivyo, wakati Said akijiokoa kwa shida helikopta ya polisi ilipita mara mbili eneo hilo bila msaada wowote mara ndipo wananchi wakaanza kulaumu kwamba badala ya kuokoa majeruhi kazi yao wanapita na kuondoka."Tunasikia kuwa kazi ya helikopta ya polisi ni kuokoa majeruhi, lakini tunashanga wanazunguuka katika eneo hili bila ya msaada wowote, wameonekana mara mbili,"walisema wananchi.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,419
  Likes Received: 19,726
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Ang'ang'ania mkia wa ng'ombe kujiokoa [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 21 December 2011 20:49 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Pamela Chilongola
  SHARIFU Said mkazi wa Tabata Segerea wilayani Ilala, jana alitumia kila aina ya mbinu ikiwamo ya kushikilia mkia wa ng'ombe kwa ajili ya kunusuru maisha yake baada ya kusombwa na maji ya mto Msimbazi kutoka Segerea hadi Matumbi.Kufuatia kuchelewa kwa juhudi za uokoaji, Said alilazimika kutumia kila aina ya mbinu kujiokoa ikiwamo mkia huo wa ng'ombe baada ya kusombwa na maji na kukaa zaidi ya saa tano.

  Akisimulia tukio hilo, Said alisema mvua ilianza kunyesha mnamo saa 11:00 asubuhi mara akaona maji yakiingia ndani ya nyumba yake, ndipo alipoanza kutoa baadhi ya vitu nje.
  Said alisimulia kwamba, alipotoa baadhi ya vyombo alienda kwenye banda la ng'ombe na kukuta maji yameingia ndipo alipoamua kuwaokoa ng'ombe wake kwa kuwatoa ndani ya banda hilo.
  "Nipo ndani mara nikaona maji yanaanza kuingia ndani ndipo nilianza kutoa baadhi ya vitu, wakati natoa mara nikasikia ng'ombe wangu wanalia nikaelekea kwenye banda nikakuta maji yameingia ndipo nikaanza kuwaokoa ng'ombe wangu,"alisema.

  Wakati akiwa anawaokoa ng'ombe wake, alisema mara aliona maji yakiwa mengi kama mto ndipo maji hayo yalipomsomba yeye mwenyewe, ng'ombe na baadhi ya vitu vyake.Said alisema alipelekwa na maji kusikojulikana ghafla yalimtupa eneo ambalo alikuwapo ng'ombe wake ndipo alipoukamata mkia wa ng'ombe.
  "Nilimuomba Mungu anisaidie baadaye nilipoona maji yameshanishinda nilimuachia Mungu yeye ndiye muweza wa kila kitu, kama siku zangu zilikuwa zimewadia au kama zilikuwa bado yeye ndiye anayejua,"alisema na kuongeza:

  "Nikiwa namuomba Mungu mara nikatupwa na maji kwa nguvu karibu na ng'ombe wangu, ndipo nilifanikiwa kumshika katika mkia wake."
  Alisema akiwa yeye na ng'ombe wake, walipita kwenye maeneo ambayo hayatambui wakati huo alikutana na vitu mbalimbali kama magodoro, sofa na ndoo.

  Akiwa amemshikilia ng'ombe mkia, mara alijigonga kwenye mti na kujikuta amemwachia ng'ombe huyo na kutupwa upande wa mti ndipo aliukamata mti huo zaidi ya nusu saa.
  "Nilipokuwa nimeshika ule mti maji yaliongezeka zaidi na kujikuta ninaondoka na ule mti, nilijua hapa ndio mwisho wa maisha yangu,"alisimulia zaidi Said
  Alisema akiwa haelewi anakokwenda akiwa mbali kabla hajafikia daraja la matumbi aliona magari yamepanga foleni barabarani alitamani kunyoosha mkono lakini alishindwa kutokana na wingi wa maji yaliyokuwapo.

  Akiwa anapelekwa na maji eneo la daraja la Matumbi, aliona mti wa muarobaini ndipo alipoweza kuushikilia hadi walipotokea wasamalia wema na kumuokoa.

  Waliomuokoa
  Mwokoaji Abed Abdalla, alisema said baada ya kukaa katika mti huo zaidi ya saa tatu bila msaada wowote, alikusanya vijana na kutafuta kamba ili waweze kumuokoa.Alisema baada ya kutafuta kamba ndipo aliamua kujitosa kwenda kumuokoa huku wengine wakiwa wameshikilia kamba hiyo, aliyokuwa amejifunga kiunoni ili aweze kumuokoa.

  "Sisi kama wananchi tuliamua kujitolea kumuokoa mwenzetu, na tulipiga simu polisi, zima moto lakini hadi sasa hawajafika hii inaleta taswira gani hatuoni maana ya Serikali,''alisema Abdalla.

  Hata hivyo, wakati Said akijiokoa kwa shida helikopta ya polisi ilipita mara mbili eneo hilo bila msaada wowote mara ndipo wananchi wakaanza kulaumu kwamba badala ya kuokoa majeruhi kazi yao wanapita na kuondoka."Tunasikia kuwa kazi ya helikopta ya polisi ni kuokoa majeruhi, lakini tunashanga wanazunguuka katika eneo hili bila ya msaada wowote, wameonekana mara mbili,"walisema wananchi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,205
  Trophy Points: 280
  .....Serikali haina msaada wowote ule, wako radhi kununua bunduki, risasi, marungu, gari za kumwagia Wananchi maji ya pili pili kila wanapojaribu kuandamana kudai utendaji bora lakini hata siku moja haioni umuhimu wa kununua vifaa muhimu vya kuokoa Wananchi wake kwenye mafuriko na majanga mengine mbali mbali ambayo yanawakuta Watanzania.
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Amshukukuru sana Mungu. Je ktk hili kuna imani na serikali yetu tena? Kama ni hapa mjini kulikojaa vifaa vyote vya kijeshi ikiwemo vya uokoaji je walioko huko vijijini si wataangamia wote? Asante Jk kwa yote haya Mungu ndiye atakaye kuwa jibu kwa haya unayotutendea waTz
   
 5. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  aiseee inasikitisha!!
   
 6. L

  Lady G JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 517
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  pole sana muhanga. Inasikitisha kwa kweli
   
 7. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Serikali ni nini? Serikali ni akina nani? Ukiweza kufahamu hili ndio utajua nani wa kumlaumu! Tusizoee tu kutoa lawama zisizo na maana kila siku
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ile chopa haiokei ila inapiga picha tu.
   
 9. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Rejao acha ushabiki fahamu tuko kwenye crisis!

  Ujue kuna watu wamekufa na kupoteza kila kitu chao walichokipata kwa jasho na siyo ruzuku au posho.
  Grow up and show some sympathy for now!

   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Siku zote huwa nakwambia Rejao, zipime kwanza kauli zako kabla ya kutoa hoja. Katika wakati mgumu kama huu ambao watu wanaomboleza, hatupaswi kufanya utani hata kidogo. Kama kila mtu ni serikali basi tuacheni kila mtu afanye maamuzi yake kulingana na anavyoweza. Kwanini polisi hutuambia tukikosea tutakutana na mkono wa serikali? Humaanisha akina nani? Kama si hao polisi, jeshi, mahakama, baraza la mawaziri pamoja na wale wote tuliowapa mamlaka katika nchi yetu? Hivi kama tukisema kila mtanzania ni serikali na alikuwa na jukumu sawa na lile la jeshi la polisi au jeshi la uokozi, tunaliongeleaje suala la usalama wao, ukizingatia kwamba wananchi hawa hawana vitendea kazi? Hivi ingekuwaje kama kila mtu angejaribu kuokoa halafu na yeye akasombwa na maji? Kama nchi tulitakiwa kuwa na trained people wa mambo ya uokozi, wanaodeal na mambo ya maafa. Sasa kwa nchi yetu ni kila kitu ni hovyo hovyo tu.
   
 11. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Hivi Rejao uko serious au unatania? unauliza serikali ni akina nani? m
  ajibu ni wafanyakazi wa serikali si maanishi watumishi wa umma,
  usichanganye chemicals hapo. Kama DSM uokoaji ni shidA, je sisi wa
  huku mikoani itakuwaje?

  hapa ile timu ya maafa kitaifa ni muhimu ikajipanga upya. Helikopta
  za jeshi zinatakiwa kustep in kuokoa watu sio tunasubiri mpaka mbunge
  kutoka mafia aje DSM tena akodi boti kuokoa watu, jeshi (JWTZ have to step in) liko wapi na
  linafanya nini? au ndiyo tuseme hii janga kaachiwa mkuu wa mkoa wa DSM?
   
 12. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ni kweli ile chopa ni ya kupiga picha tu! mmesahau KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI?
   
 13. Shukuru

  Shukuru JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 3, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  We vp? serikali ni ile inayoamrisha jeshi iwapige wale wazee wa EAC wasio na hatia....... ila serikali si ile inayoamrisha wanajeshi wawache watu wafe na mafuriko.
   
 14. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Yangekuwa maandamano ya CDM au ya wanavyuo we polisi faster wangefika na kuanza kupiga marungu.
   
 15. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Rejao Muogope Mungu wako, usione ww hayajakufika ukaropokwa tu. Roho zimepotea na watu wamepoteza kila ki2 chao hlf ww unasema wakulaumiwa ni nani? Sawa basi maafa yashatokea serikali inaashindwa hata kutoa msaada wa haraka kwa wahanga? Tunaangalia Tv hapa wanohojiwa wanasema hawajapelekewa hata chakula na wamefika tangia jana usk kwenye hizo sehem za hifadhi wanasadiwa na wasamaria wema waliopo maeneo ya hapo. Kusema kweli inaskitisha sn.
   
 16. mawazoyangu

  mawazoyangu JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 327
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Wewe rejeo assume ni ndugu zako wamekumbwa na janga hilo ungeongea huo upuuzi hapo Juhudi? Dar ndipo kila kitu kipo, wizara, vitengo vya maafa, majeshi yote, lakini hakuna juhudi zilizoonyeshwa na serikali yetu. Sina imani nayo. Hawakuonyesha jitihada kuokoa watu. Helikopta ilikuwa inazunguka kuwakebehi waathirika, kwa kutumia mafuta yaliyonunuliwa na kodi zetu. TBC nao hawakurusha live maana ingekuwa inaishtaki serikali kwani ni watu waliojitolea ndio wangeonekana wanaokoa watu.
   
 17. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Katika hali ya kustaajabisha na kushangaza kabisa, atakuja hapa mtu mwenye akili za kong'ota na kuwaambia watu kwamba serikali haistahili kulaumiwa.
  Kama helikopta zinapisha angani wakati wa kampeni za uchaguzi, Kamanda Tossi anaweza kuruka na helikopta ya polisi kwenda bonde la mto rufiji kukamata wapika gongo, inakuwaje kwenye majanga kama haya yanayohitaji uharaka wa kuokoa maisha na mali za watu, hatuoni helikopta yoyote!?
  Halafu wajingawajinga wanaanza kumsingizia Mungu, wakati walikuwa na uwezo wa kujiandaa kukabiliana na athari za mvua kwakuwa mamlaka ya hali ya hewa ilishatoa tahadhari mapema.
   
 18. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145

  Hivi huyo Ng'ombe aliyeng'ang'aniwa mkia ni JIKE????
   
 19. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  hivi wewe huwa ni binadamu, jini ama shetani?
   
 20. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  REJAO ndio hao wezi wa rasilimali za nchi asiejali utu na maisha ya binadamu. serikali tunaijua ni kina nani na nni anapaswa kuwajibika kuokoa maisha na mali za wananchi
  nyie mwaendekeza uchama na kujali matumbo yenu huku wananchi wakiangamia
  ndio yale yale ya JK kutoa pole kwa mkuu wa mkoa kwani yy kasombwa na maji?au kwa vile ni mkuu wa mkoa?? pole zitolewe kwa wahanga na sio mkuu wa mkoa NA SIO POLE PEKE YAKE UOKOZI UFANYIKE
  igeni ya mbunge wa Mafia kajitosa kuokoa wananchi bila kujali itikadi au jimbo lake.WENYE AKILI kama za kina REJAO hawana faida humu duniani.
   
Loading...