Kisa cha kusikitisha hivi kwa nini jeshi la polisi linafanya hivi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa cha kusikitisha hivi kwa nini jeshi la polisi linafanya hivi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by EasyFit, Feb 26, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  JESHI la Polisi nchini limeingia katika kashfa nyingine baada ya kijana Charles Patrick Paulo mkazi wa kijiji cha Mundemu wilayani Bahi mkoani Dodoma kulishushia tuhuma nzito za kupora fedha na kumbambikia kesi ya unyang’anyi.

  Kesi hiyo iliyoendeshwa kasi ilimtupa jela miaka 15 kabla ya kuachiwa huru miezi sita baadaye
  baada ya kushinda rufaa.

  Julai 20 mwaka jana, Paulo alitiwa hatiani na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mundemu
  F. Bulyota kwa shitaka la unyang’anyi kifungu namba 286 K/A Sura 16 na kutupwa jela kwa miaka 15.

  Hukumu hiyo ilianzisha safari mpya ya maisha kwa kijana Paulo ambaye aliachana na maisha ya uraiani akimuacha mchumba wake, Upendo Masila akiwa na ujauzito wa miezi miwili huku
  yeye akipelekwa katika Magereza ya Isanga kuanza kutumikia kifungo chake.

  Lakini kwa vile alijua kuwa hukumu yake imetokana na uonevu wa Polisi, wiki moja baadaye
  kijana Paulo aliwasilisha rufani yake kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma akipinga hukumu hiyo, rufani ambayo ilizaa matunda Januari 26 mwaka huu, pale Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Dodoma, R.M Ngimilanga alipotoa hati ikiamuru
  kijana huyo kuachiwa huru mara moja.

  “Siku ya tarehe 20/07/2011 – Charles S/O Patrick Paulo Mshitakiwa katika jinai 52/2011 alifikishwa/ kutiwa hatiani mbele ya F.

  Bulyota Hakimu Mahakama ya Mwanzo – Mundemu kwa shitaka la unyang’anyi K/F 286 K/A
  Sura 16, jela miaka kumi na mitano (15)... “Hati hii inakuamuru wewe Ofisa wa Gereza kumwachia huru Charles S/O Patrick Paulo.

  Hati hii imetolewa kwa amri yangu na Mhuri wa Mahakama ya Wilaya leo tarehe 26/01/2012,” inasema hati hiyo ya kifungo baada ya rufaa ambayo inamfanya Paulo kurejea uraiani akimkuta mchumba wake Upendo akiwa tayari amejifungua mtoto Februari 2, mwaka huu, mtoto aliyebatizwa jina la Rogers.

  “Mchumba wangu amejifungua lakini sijawahi kumuona mtoto wangu naogopa kwenda
  kijijini Mundemu maana polisi wanasema wanataka kunipoteza kwa kuniua najua wataweza
  kwani walinibambikia kesi ya unyang’anyi nikahukumiwa miaka 15 jela lakini Mungu amenisaidia nimetoka….lazima sasa niwe makini,” anasema kijana Paulo ambaye sasa amegeuka kuwa mkimbizi ndani ya nchi yake mwenyewe akiishi kwa kujificha jijini Dar es Salaam.

  Mkasa wenyewe
  Akizungumza katika ofisi za gazeti hili jijini Dar es Salaam, wiki hii Paulo anasema kisa na mkasa wa sakata lake na Jeshi la Polisi vilianzia katika kijiji cha Kongogo wilayani Bahi alikokwenda kufanya biashara ya mnadani akiuza mitumba na nyama ya ng’ombe.

  Anasema baada ya kumalizika kwa mnada huo uliofanyika Desemba 12, 2010, alikwenda pembeni kidogo ya eneo la mnada kwenye kichaka na kujisaidia haja ndogo.

  Anasema baadaye alitoa fedha zake Sh 470,000 taslimu alizokuwa nazo awali na Sh 150,000
  za mauzo ya mitumba na kuzificha ndani ya bukta ili kuepusha kuibiwa.

  “Mara baada ya kuzificha fedha zangu ndani ya bukta walikuja polisi wawili. Kwanza walinihoji
  kwanini najisaidia vichakani, nikawajibu mara nyingi sehemu za minada huwa tunafanya hivyo
  kutokana na ukosefu wa vyoo.

  Hata hivyo walinipiga piga makofi mgongoni na kunitaka nipotee.

  “Kwanza nilianza kukimbia kwa kwenda vichakani lakini baadaye nikashituka kwamba kule
  hakukuwa na usalama nikaamua kurudi nilipotoka lakini polisi wale walikuwa wakinikimbiza na
  pikipiki. Baadaye niliamua kusimama… walipofika waliniuliza kwanini narudi kule mnadani
  tena, nilitaka kuwajibu walinipiga na kitako cha bunduki nikaanguka na kupoteza fahamu.

  “Nilipopata fahamu nilikuta wamenibeba kwenye pikipiki nikiwa katikati yao huku mkono
  wangu mmoja wakiwa wameufunga pingu ambayo ilikuwa pia imefungwa kwenye bomba la
  pikipiki. Niliwauliza walikuwa wananipeleka wapi…wakasema wanajua wao. Mwendo mfupi
  mbele waliniuliza kama waende na mimi au waniachie… niliomba waniachie, wakaniachia.”

  Alisema baada ya kufika nyumbani (Mundemu) aliamua kwenda hospitali lakini alishindwa
  kutibiwa akiagizwa kwanza kuwa na fomu ya matibabu (PF 3) kutoka Polisi. Anasema baadaye
  alipewa fomu hiyo na kutibiwa.

  “Baada ya matibabu nilianza kufuatilia suala hili. Nilianzia Polisi Mkoa kwa Kamanda wa
  Polisi wa Mkoa (RPC), Ofisa Malalamiko wa Mkoa na hata Polisi Wilaya ya Bahi. Nilifuatilia
  mara nyingi sana lakini nilikuwa napigwa danadana huku na kule… wale polisi baada ya
  kuona nawafuatilia sana walianza vitisho na kuniambia watanibambikia kesi nifungwe nipotee.

  “Baada ya kufuatilia sana baadaye Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Bahi (OCD) aliitisha gwaride la
  utambuzi kwa askari wake wote na nilifanikiwa kuwatambua askari walionipiga na kunipora
  fedha. OCD alianza kufuatilia suala hilo kwa kunitaka nilete mashahidi na nilifanya hivyo
  mara kadhaa bila kupewa haki yangu.”

  Alisema wakati akiendelea kufuatilia suala hilo, ghafla usiku wa Julai 18, kuamkia Julai 19, mwaka huu saa tisa usiku akiwa amelala nyumbani kwake walikuja watu kutoka ofisi ya Ofisa Mtendaji na kudai kuwa nimetajwa kuhusika katika tukio la uhalifu.

  “Asubuhi Julai 29, 2011 nilipandishwa kizimbani nikasomewa mashitaka na nilimuona huyo
  mama anayesema nilimvamia nyumbani kwake usiku huo nikiwa na wenzangu watatu na kupora mali zake na fedha. Cha ajabu sikuona hao wengine ninaoambiwa nilikuwa nao.

  Nilipohoji walisema walikuwa wamenitambua mimi ingawa walisema tulikuwa tumevaa soksi
  usoni.

  “Hakimu alinisomea mashitaka yangu na akamwambia mlalamikaji kuleta mashahidi
  wake. Mimi niliomba nipewe muda nilete mashahidi wangu kwa vile wengi walikuwa
  wamekwenda mnadani lakini kwa bahati mbaya kesho yake Julai 20, 2011 nilihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.

  “Hata hivyo pamoja na kuhukumiwa lakini nilisikitishwa na hatua ya polisi waliokuwa
  wakinipeleka gerezani kwa pikipiki wakiwa na mgambo kunifunga pingu na kunining’iniza
  mtini porini na kuanza kunichapa fimbo wakisema ni kutokana na kunikomesha kwa kujifanya
  mjanja,” alisema Paulo.

  Akizungumzia madai hayo, Ofisa Malalamiko wa Polisi Mkoa wa Dodoma SSP Pancras Mdimi
  alikiri kupokea jalada la Paulo na kusema kuwa limerudishwa Polisi Wilaya ya Bahi ambapo
  kesi yake ilipoanzia.

  Alisema kuwa, baada ya jalada hilo kuletwa likiwa halina hati ya mashtaka na nakala ya hukumu ambapo awali faili hilo liliitishwa baada ya mlalamikaji kuleta malalamiko yake.

  Mdimi alisema kuwa, hata mlalamikaji ambaye kwa sasa yuko Dar es Salaam alipotakiwa
  kuleta mashahidi kuhusiana na malalamiko yake alisema kuwa hawezi kumudu kuleta mashahidi hao kutokana na gharama.

  Hata hivyo alisema kuwa, watashughulikia madai ya mlalamikaji baada ya kupata faili
  kutoka Polisi Wilaya ya Bahi.

  "Mambo mengi yalikuwa hayajakamilika ndiyo maana faili lake halikushughulikiwa kabisa,"
  alisisitiza Mdimi.

  Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Zelothe Stephen alipohojiwa na
  gazeti hili alimtaka Charles afuate utaratibu wakati shauri lake likishughulikiwa.

  "Afuate utaratibu aende pale kesi inapohusika kwa nini anatangatanga wakati shauri lake
  linashughulikiwa?" alihoji Kamanda Zelothe.

  Alisema kuwa, ni vizuri kama mtu huyo angefuata utaratibu kusubiri hatma ya madai yake.

  Hata hivyo kijana huyo ameliambia gazeti hili hawezi kutokana na watuhumiwa katika shauri hilo kuwapo huko na anaogopa safari hii haitakuwa kifungo bali kifo.
   
 2. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  Kwa unji hii yapo mengi sana kama haya lakini habari hatuzpati! ,afadhali na sku hizi vyombo vya habari vipo zamani..... Mmmh
   
 3. Pawaga

  Pawaga JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  makubwa,2taisha cjui
   
 4. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  So sad...aiseeee!!
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,885
  Trophy Points: 280
  du so sad, sasa hao polisi wamechukuliwa hatua gani?? unajua kuua kwa uonevu kama huu kumbe kazi rahisi sana aisee!
   
 6. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Unaweza kuona wazi wale wanaodai afuate utaratibu ni kufunika ili jamaa ashindwe hizo taratibu waonekane hawana hatia. Nchi hii na jeshi la polisi ni rushwa tu hata wajitetee vipi
   
 7. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mkulima wa Kuku...inasikitisha sana...Yaani maisha ya mtu yanaharibiwa kisa shilingi laki 6!!Polisi walikuwa 2...kwa hiyo kila mmoja alikunja laki 3...sasa hii ni hela gani sasa...mpaka iwasukume kufanya unyama huu!!...Ama kweli hizi ni nyakati za mwisho.
   
 8. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  polisi wa tanzania wana matendo zaidi ya al shabab
   
 9. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Huyo jamaa aende kule LHRC kwa kina kiwanga wamsaidie.jeshi linafuga wahuni
   
 10. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,823
  Trophy Points: 280
  Hili ni moja kati ya matukio 1000 yanayofanywa na askari wa jeshi la polisi.
  Iko hivi, kuna jamaa nilipata kusoma naye kitambo na sasa ni polisi kitengo cha FFU.
  Juzi polisi huyu kaniambia kuwa, huwa anakodisha silaha yake kwa majambazi wakati wa lindo usiku (hasa akipangwa bank) na asubuhi hurejeshewa silaha yake na kitita cha laki mbili mpaka tatu kutoka kwa majambazi hayo.
  Hakuishia hapo, polisi huyo alizidi kunidokeza kuwa wanapoishiwa na pesa za matumizi huwa wanachukua silaha wakati wa lindo mida ya jioni na kuvaa makoti makubwa kama raia na kuvamia maduka makubwa ya biashara za jumla wakati wa kufunga na kutishia kwa silaha hizo za jamuhuri na kupora fedha kutoka ktk duka husika.
  Polisi wetu wakiwa huko mafunzoni hufundishwa utii wa uwoga na wanapewa treatment mbaya sana kiasi cha kuwafanya kuwa na roho mbaya na ya kikatili badala ya kuwa waaminifu na watii wa sheria.
  Mafunzo ya ukatili wanayofundishwa askari wetu yanawafanya walinzi hawa wa usalama wa raia na mali zao kugeuka na kuwa majambazi kwa kujaribu kujikwamua kwenye umaskini kwa kutumia ukatili uleule waliofunzwa huko CCP.
  Askari anayelipwa laki mbili unusu kwa kazi ya kulinda bank yenye billions of money lazima awe mwizi.
  Kwa kifupi polisi ndo wezi hapa tanzania.
   
Loading...