Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 5,355
- 11,500
Nimekuwa nikifahamu kwa jinsi ambavyo watu wa bara wanatudharau sana sisi watu wa Pwani. Namfahamu jamaa mmoja tulikuwa naye shule yeye alikuwa hafichi dharau zake.
Akitusema kuwa tunakuwa nyonde nyonde, wavivu, waongo waongo, wanafiki na tusiofaa. Sikuwa napenda tabia ya dharau aliyokuwa akionesha huyo jamaa.
Ila sikudhani kama chuki ile ingefikia hatua ya kumpiga mawe Rais wa Nchi kwa kumwona kuwa ni mswahili swahili. Jamaa waliwaza nini kufikia kumpiga mawe Rais wa nchi?
Wadau nakumbuka kisa hicho ambacho kilisababisha vijana wa eneo hilo wengi kukimbia kijiji chao. Walitafutwa vijana wa kijiji hicho pasipo kujali wahusika na kupigwa sana. Wengi wao hawakuonekana kujutia kosa.
Rais wa nchi anapaswa aheshimiwe hata kinafiki. Tusifikie hatua ya kumpiga mawe, au kumzomea. Leo hii hawa wanaopiga mawe kama wangepata mabomu si wangerusha?
WALE NDUGU NI KWANINI WALIAMUA KUMPIGA MAWE RAIS WA JMT?
Hao wanaozomea mnadhani wakipata risasi hawatamrushia Rais? Tujifunze kuvumiliana. Wazee walisema
"AKUMULIKAYE MCHANA,USIKU ATAKUCHOMA MOTO"