Kisa cha Jakaya, Sauli na MUNGU, na mstakabali wa Tanzania Mpya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa cha Jakaya, Sauli na MUNGU, na mstakabali wa Tanzania Mpya.

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Yericko Nyerere, Sep 17, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  [h=1][/h] 16 Sep 2012 kupitia Yericko Nyerere
  Ni takribani miaka 7 sasa tangu taifa la Tanzania limpate kiongozi wake muhimu na aliyekuwa tumaini la watanzania. Ninaamini Tanzania ni taifa lilo chini ya uso wa Mungu na ninaamini tumaini la wengi ni tumaini la Mungu pia.
  Mimi ni mmoja ya wahanga wa uwekezaji wa tumaini letu kwa rais wa awamu ya nne ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, ninakumbuka vema alivyoweza kupora tumaini langu nami bila hiyana wala gubu nikampa kura tena nikikenua meno ya moyo wangu nikiji nasibu kwa turufu ya sandu la kura chini ya upinde wa Rajabu Kiravu. Imani yangu na ya watanzania wengi ilijengeka kwa ccm na Jakaya kutokana na ukweli unaoaminika kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.

  Tukisoma Luka 13:1-2 . Kila mtu na aitii mamlaka iliyokuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; nd ile iliyopo umeamriwa na Mungu; na washindanao watajipatia hukumu.

  Hata kuruani tukufu inasisitiza kuheshimu mamlaka zilizopo, na inatambua kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.

  Ni ukweli usiopingika kuwa mwaka 2005 Jakaya M. Kikwete alikuwa ni chaguo la Mungu, na kwa maksudi ya haki Mungu alimtuma aje atende kazi moja tu maalumu.
  Nasema ni MOJA tu kwakuwa kupitia kinywa chake aliyatamka wazi na kuyapa nguvu za kila nera, hata ulipokuja uvumo wa kusi bado alisimama imara kutuaminisha kile akisemacho,

  Kazi hiyo ilibatizwa jina la MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA. Nani haamini sera na kauli hiyo ya Jakaya? Nani hakumbuki jinsi ubeti huo ulivyokuwa ukipambwa kwa sauti tofautitofauti tena zingine zakughani kwa vina tata chini ya magwiji wa sera msonge za kale zenye asili ya umungu mtu. Hao sio wengine bali ni Kingunge na Malecela.

  Wimbo huu ulirejea mwaka 2010 lakini sasa ukipakwa mafuta zaidi kwa kuongeza maneno ya kilaghai zaidi, Naam nashukuru kipindi hicho nilikuwa tayari nimeerevuka tena kwa mapana yote, hivyo kura yangu haikuliwa na kundi hilo MUFILISI, bali nilijiandikisha jimbo la Ubungo na niliamua kusafiri kilomita kadhaa kutoka Ukonga kwenda kupiga kura jimbo la Ubungo, huko ndiko niliamini kura yangu ya haki itachipuza. Hakika ilichanua chini ya Jemadari John Mnyika.

  Utawala wa Jakaya Kikwete ni utawala pekee unaoweza kuelezwa bila kupaka mafuta kuwa ni utawala MBOVU na DHARIMU ambao haujapata kutokea tangu taifa letu lipate uhuru kutoka kwa waingereza mwaka 1961. Wakati huo nikirejea machapisho ya kale yenye kusimulia tawala kichifu za Tanganyika na Zanzibar bado sijabahatika kufahamu utawala wowote wa kichifu uliosononesha watu wake na kufikia hatua ya kukata tamaa.

  Nimejiridhisha kwa hilo hasa nikiangalia tawala kubwa kubwa za akina Mkwawa, Kinjekitile, Abushiri, Mirambo, Isike nk. Ninaona kabisa kuwa waliwatumikia watu kwa usawa, walipendwa, walilinda raslimali zao, waliheshimika tena kuliko hata Mungu, kwani wengi ilikuwa unawaabudu wao kasha wenyewe watakufikishia maombi yako kwa Miungu wao nawe utabarikiwa.

  Binafsi naamini kabisa kuwa rais wetu mpendwa Jakaya Kikwete kamkosea Mungu. Tena kamkosea sana, amekiuka kile alichomtuma kwa watu wake na badala yake anafanya YAKE.

  Utawala mbovu katika nchi haujaanza leo duniani, kwani wamekuwepo katika simuliza za kale watawala wengi walioiliza mioyo wa wanchi wake, Hii inatupa fursa yakujifunza mengi kama taifa na hakika hakuna taifa ambalo katika historia linaonyesha kuwa liliyarydia makosa yenye kuliza mioyo.

  Kisa hiki hakina tofauti na Mtumishi wa Mungu Sauli aliyetiwa mafuta na Samweli kuwa mfalme wa watu wa Israel, na Mungu akampa kazi MOJA maalumu ya kwenda kuwaangamiza wa Amaleki. Lakini Sauli alikwenda kinyume na Mungu.

  Hebu turejee 1 Samweli 15:1-35
  Katika simulizi hii japo ni ndefu lakini tunaona yakuwa licha ya jeuri na dhihaka ya Sauli, baadae alirejea na kumlilia Mungu na kukiri kuwa alikosea.

  Tatizo ni je watawala wetu wanaweza kukiri mbele za Mungu kuwa wamekosea? Kwanza hawajui kama wamekosea au wanakosea na itakuwa ajabu wamkiri Mungu kuwa wamekosea ilihali hawakiri kwetu sisi binadamu wakawaida wenye macho ya nyama.

  Njia sahihi kwa Watanzania katika kipindi hiki kigumu si kumlaumu rais wala kujilamu bali kutulia mbele za Muumba na kumuomba ashushe hekima na busara kwa rais wetu huku tukijiombea nasi atupe moyo wa ujasili na imani tukijiandaa kwa mageuzi matakatifu yanayoongzwa na Mungu kupitia CHADEMA.
   
 2. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  [h=2][/h]
  16 Sep 2012 kupitia Yericko Nyerere

 3. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni mtawala gani wa dunia ya leo aliyewahi kukiri mbele ya watu wake kuwa kashindwa?

  Pamoja na yote jk nae anamazuri aliyoyafanya, mfano ni huo uhuru wa kutoa maoni unaouonyesha wewe leo, enzi za baba yako Nyerere, mwinyi, na mkapa ungeongea hivi?
   
 4. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo tuendelee kuwa maskini kwa sababu kuna uhuru wa maoni? watu wanavokufa huoni?, njaa hizi wajameni zinatisha
   
Loading...