Kisa cha Idd Amin kuivamia Tanzania

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,798
2,739
Baada ya Idd Amin kumpindua Obote mwaka 1971, aliweza kuhudhuria vikao mbali mbali huko umoja wa mataifa. Siku moja wakakutana katika kikao kimoja cha kwanza kwa Idd Amin kuhudhuria, na kwa kuwa Idd Amin hakujua vizuri lugha ya Kiingereza na kwa kuwa alikaa karibu na Nyerere akamuomba Nyerere amuandikie maneno machache ya kuzungumza pale mbele mara zamu yake ikifika.

Alichokuwa akiweza kuzungumza Idd Amin bila kusoma ni neno "good morning, ladies and gentlemen na neno thank you". Nyerere akamwandikia hotuba fupi akampatia. Yeye Idd Amini akaiweka ile hotuba ndani ya kofia yake ya kijeshi, ili akifika pale mbele ajifanye kuvua kofia na aweze kusoma maandishi aliyoandikiwa na Nyerere bila washiriki wa mkutano kujua.

Kwa bahati mbaya kuna wakati alivua kofia wakati amekaa pale kwa lengo la kujikuna kile kikaratasi kikaanguka kwa nyuma. Zamu yake ilipofika akainuka na kwenda mbele kwa madaha na majigambo kufika pale akavua kofia yake akaanza hotuba kwa maneno yake ya "Ladies and Gentlemen good morning"... kisha akainama ili kusoma hotuba aliyoandikiwa na Nyerere bila kujua alishaangusha akaanza kwa kujitambulisha:

"My name is Idd Amin Dada, the Sovereign Chief of Baganda, Mighty King of Uganda, Saviour of the African continent, the World's Commander-In-Chief, Holder of the Advanced PhD and the Conqueror of the British Empire.

Baada ya majigambo akaendelea na hotuba yake

"Washing instructions: warm water wash/ air dry. Adult & Youth Sizes/ Same Price / Fits Kids Ages 6 to 12. Cap"

Akamalizia "Thank you all.

Baada ya kurudi kuketi Jomo Kenyatta akamwendea kumuuliza kwanini ametia aibu kiasi kile. Baada ya kupata maelezo ya kina kutoka kwa Jomo Kenyatta, tangu siku ile akaingia bifu kali na Nyerere akidhani alimwandikia yale aliyoyasoma kumbe wala. Akapanga kuivamia Tanzania, na ndivyo ilivyokuwa.
 
Kweli Watanzania kwa fix hamuwezekani! Wengine wanasema eti Kawawa kalala chini Ujerumani kisa kashindwa kubonyeza switch ya kufungulia kitanda, mmm makubwa!
 
Wengine waksema et Bibi Titi aliwahi kusema kuwa Mr Speaker, the fire which comes from small bottles which hang from the roof in Kinondoni is not burning, all houses are dark. akiwa na maana kuwa kinondoni hakuna umeme.
 
ahhahaha kazi kweli kwelii Nyerere alikuwa na kazi kubwa maana ni wachache sana walikuwa wanaweza kunyoosha mistari kudhungu wakati ule...........acha tu maana kina Rashidi MK alikuwa kuli tu wa bandarini .......same to AM Karume.....walikuwa wachapa mizigo bandarini.........
 
Enzi hizo kusoma na kuandika tu ilikuwa mbinde, unafanya mchezo na kuongea kiingereza. Nakumbuka bibi yangu alikuwa na maneno yake ya kidhungu nikikumbuka mpaka kesho nacheka peke yangu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom