Kisa cha binti mzinifu na kauli za viongozi wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa cha binti mzinifu na kauli za viongozi wa CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mohamedi Mtoi, Mar 27, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Binti mmoja katika kijiji cha asali na maziwa, kijiji ambachokiimeenziwa kwa misingi ya haki na usawa, kijiji kilichokuwa kimejaawazee wa hekima na busara, kijiji ambacho hakikuruhusu hata siku mojakuchezea misingi na maadili alipituka na kutoka nje ya misingi ya ndoakwa kufanya zinaa na mwanaume wa mtu, hii ilikuwa kinyume kabisa nasheria kali za kijiji hicho na adhabu yake ilikuwa ni kunyofolewasehemu za siri kwa wazinifu wote (mwanamke na mwanaume) ili iwe funzokwa wengine ikiwa ni pamoja na kuendeleza utamaduni wa kuwa na jamiiinayohofu kufanya machafu.

  Mbali na sheria kali na matamanio ya kuwa na jamii nyofu, lakinikutokana na hulka ya kibinadamu inayo ambatana na tamaa pamoja naujanja ujanja mwingi unaoweza kugeuza giza kuwa mwanga bintiakajikuta anadondokea kwenye penzi la mmoja wa walinzi wa kiongozimkubwa wa kimila anae heshimika sana hapo kijijini, mlinzi huyoalikuwa na mke na binti hakuwa na mume.

  Wakatongozana na kuanzakucheza mchezo wa vurugu za mahaba kisirisiri.Penzi halijifichi maana hata wahenga walisema, Penzi ni kikohozi, sikuya siku, moja ya wazee mwaadilifu aliye kuwa anaheshimika sana hapokijijini akawafuma wakifanya uchafu karibu na kisima cha kuchoteamaji, Yule mlinzi akakurupuka mbio hakuonekana, msala ukabaki kwabinti maana alikutwa kapandisha baadhi ya nguo mpaka eneo la tumbohuku nyingine zikiwa amezitundika juu ya kichaka.

  Kwa taharuki binti akaanza kuangua kilio huku akikimbia kwa mayowe yakuomba msamaha maana alijua kuwa tayari siku ya kunyofolewa sehemuyake ya siri imefika. Mbio mpaka kwa mama yake, hakumficha akahadithiamwanzo mpaka mwisho. Mama wa binti yule akatabasamu na kumtia bintiyake nguvu huku akimpiga piga mabegani na kumuambia, "Mimi ni mamayako, ndio ninae kufahamu kuliko mtu yoyote, mimi ndio nimekubebamiezi 9 tumboni, hakuna wa kukunyofoa UKE WAKO" mama alijiapiza.

  Akamkumbatia bintiye huku mama yule akifungua ziwa mwanae anyone! Kwamshangao, Binti akamwambia mama yake "mbona mama unanifungulia ziwaninyonye wakati umeniachisha miaka 18 iliyopita?!" Mama akamuambia"Nyonya ziwa haraka mwanangu kengele itagongwa sasa hivi ili watuwakusanyike waone unavyo adhibiwa".

  Haraka binti yule akanyonya ziwa la mama yake, alipo maliza tukunyonya! Mama yake huku akiwa kamshika binti yake sikio akamuambia"NISIKILIZE KWA UMAKINI" kwa mila za hapa, wewe ndio utakuwa wa kwanzakuhojiwa, wakikuuliza kwa nini umezini, kataa! Waambie "Tangu nimeachakunyonya ziwa la mama SIJAWAHI KUZINI".

  Kawaida ya watu wa kijiji hicho kabla ya hukumu huwa wana-nyweshwamaji ya mizimu ambayo hudhuru hapohapo endapo mtu hakusema ukweli.Mara kengele ikagongwa watu wakakusanyika na kunyweshwa maji. Kiongoziakaeleza mashtaka aliyopeelekewa na kuweka wazi dhamira yakukusanyika.

  Binti yule akawa wa kwanza kuulizwa . Pilato.."BintiGamba, leo umefumwa ukizini maeneo ya kisimani, sema ulikuwa unazinina nani na kwa nini uzini'?Binti akafanya kama alivyoambiwa na mama yake tena huku anabubujikwana machozi ya uwongo, akasema "MBONA MNANISINGIZIA? KWANZA TANGUNIMEACHA KUNYONYA ZIWA LA MAMA YANGU SIJAZINI" mizimu ilipo ulizwaikaleta ripoti haraka kuwa ni kweli binti huyo hajazini.

  Watuwakaamriwa watawanyike na kurudi majumbani kwao maana hapakuwa na kesiwala wa kumuadhibu. Mzee aliyetoa ripoti akaonekana muongo akapelekwakeko (Jela) ya waongo.Tuvute pumzi na kurudisha picha ya kisa cha binti mzinifu kwaviongozi wa chama tawala.• JK "…Sijawahi kuwaona Richmond, sijawahi kukutana nao na wala siwajui".•

  Viongozi wa CCM "…Hakuna pesa za EPA zilizoibiwa wapinzani hasa DrSlaa niwazushi wanaichonganisha serikali na wananchi wapuuzeni"• Serikali "…Hakuna kampuni ya Kagoda na wala hakuna fedha zozotezilizo kwapuliwa na kampuni hiyo"• Waziri mkuu bungeni "…mgodi wa makaa ya mawe kiwira ni siri yausalama wa taifa"• CCm kwenye kampeni 2005"..Maisha bora kwa kila mtanzania, kwa aringuvu na kasi mpya"•

  CCm kwenye kampeni 2010 "ahadi zote zitatekelezwa (Kumbuka zikozaidi ya 98) …Tanga itakuwa jiji la viwanda, Kigoma itakuwa Dubai yaAfrika".• CCm wenyewe wakiongozwa na Nape"..Chama kinagamba, tunajivua gamba".• BWM " Vicent hatokei kwenye familia ya Nyerere".• Makinda "Waziri mkuu (Pinda) hajalindanganya bunge kuhusu mauwaji yaArusha, Lema kama unasema waziri kadanganya lete ushahidi".Fikiria mengine, mimi nimefikiri hayo machache mpaka kichwa kinauma.

  Kumbe ndio maana Suma lee yule mwanamuziki wa muziki wa ubongo wenyefleva aliimba kule Mwanza kuwa "Hakunaga kama CCM" Huku yule kaptenialiyetunga nyimbo za kifo cha baba wa taifa kabla hatuja tangaziwakuwa amekufa nae akisema "NAMBARI WANI NI CCM".
   
 2. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Duuuuuu nice one w
   
 3. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  du, kusoma kaziiii hapo
   
 4. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,712
  Likes Received: 8,263
  Trophy Points: 280
  Wat a nice analogy..ingawa haijafanyiwa uhariri lakini imegusa palipotakiwa...we have a choice though, tuendelee kujidanganya na maji ya mizimu au tutmie mbinu mbadala kumjua binti huyu mzinifu...KURA YETU NDIYO ITAKAYOAMUA!!!!
   
 5. Fund

  Fund Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni fikra hasi zilizopo kwa wananchi zikichangiwa na ufinyu waelimu ya Uraia,ila siku itafika ambayo mambo yatakuja kubadirika na nchi itakuwa ni mpya
   
 6. k

  kalakata Member

  #6
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli kaka umeweka mawazo katika nyanja nyingine kabisa!
  But all in all kugundua mzinifu siyo lazima tutumie njia moja sanduku la 2010 ndio njia ambayo pekee itatufanya tumjue mzinifu
   
 7. Mtagwa lindi

  Mtagwa lindi JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 278
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Kweli ccm hakunaga,walisema watajenga daraja mto kilombero hamna lami mikumi maliny hata mita1 hayo maisha bora ni matuc,tunaambiwa tuwe mbaiwai ili tuzd kuumia
   
 8. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Nape, jibu tuhuma kama unaweza! Nimekuomba wewe kwa kuona angalau siku moja moja huwa unaongea ukweli!
   
 9. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Mkuu. Nape alisha kimbia hapa kutokana na falsafa ya kujivua gamba, hawezi kurudi maana maana watu watakumbushia.
   
 10. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  2015 si mbali ndiyo itakaypmhukumu bint mzinifu.
   
 11. Vodka

  Vodka JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 909
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Haa nimeipenda huu uzi,umenigusa sana.Kwakweli hapa amna jipya watanzania inabidi tulifanye zaidi ya kuitafuta elimu na kuwa na nguvu ya pamoja katika maamuzi ili tumuondoe huyu mzinifu madarakani
   
 12. D

  Dr Gustav Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nina matumaini kama wale ambao tumefunguka akiri tutawasaidia wengine ni raisi kuwa na tanzania tunayotaka
   
 13. Ghamoghi

  Ghamoghi JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2017
  Joined: May 15, 2017
  Messages: 562
  Likes Received: 1,258
  Trophy Points: 180
  Aiseeee
   
Loading...