Kisa cha Almasi za Anastazia ( Anastasia Diamonds)

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
ALMASI ZA ANASTASIA (ANASTASIA DIAMONDS)
anastasia.jpg

Binti Mrembo Anastasi.... Makatili wale hawakuwa na utu kabisa kumtendea vile mrembo kama huyu. inasikitisha sana. je hawakuona kuwa hili lilikuwa ni moja ya mapambo ya dunia hii?

Akiwa amezaliwa june 18 mwaka 1901 anastazia Romanov baba yake alikuwa ni mmoja ya watawala wa Russia. Tsar of Russia kwa jina la Nicholas II. Mama yake akiitwa Alexandra aliyekuwa mjukuu wa Malkia Victoria wa Uingereza Kuu au Great Britain.
Anastazia alikuwa na dada watatu. Olga, Tatiana na maria. Na mdogo wake wakiume akiitwa Alexei.huyu Alexei mdogo wake wa kiume alikuwa na ugonjwa unaoitwa haemophilia huu ni ugonjwa ambao mtu akiwa nao akijikata damu haigandi. Yaani inaendelea kutoka tu kama maji. Kikawaida huwa tukijikata damu inatoka kwa muda halafu inaganda labda iwe tumejikata pakubwa sana. Ila kwa Alexei inamaana hata kama ungemchoma na sindano au kujichubua kidogo tu … basi damu ingetoka kama vile umejaza maji kwenye mfuko wa nailoni halafu ukatoboa… yaani ingetoka mpaka angeishiwa damu mwilini na hatimaye kupelekea kifo chake.
Warusi walikuwa wakifahamu kuwa Alexei ni mgonjwa.

Ukimlinganisha na dada yake Anastasia huyu alikuwa ni tom boy (msichana mwenye tabia za kiume) akipenda sana utani na michezo yenye utani utani hivi.lakini pia alikuwa mtaratibu kipenda kutumia muda wake mwingi na mbwa wake na kaka yake ambaye hakuruhisiwa kutoka nje. Alikuwa akilala na dada yake maria kwenye kitanda kama cha jeshi ambacho huwa kinatumika kambini. Anastazia alikuwa akiweza kuzungumza lugha mbili. Kiingereza na kirusi.


Mama yake anastazia alikuwa akihangaika sana ili kuweza kupata dawa ya kumtibu mtoto wake Alexei. Na huyu alikuwa ndiye mtoto wake pekee wa kiume. Na siku moja akasikia kulikuwa na mtu mtakatifu mmoja akiitwa Rasputin kuwa angeweza kumtibu mtoto wake.
rasputin.jpg

rasputin. Mtakatifu chapombe katika ubora wake.

Aliamua kumtafuta huyu mtakatifu.lakini kinyume na matarajio yake Rasputin hakuwa akienenda kama mtakatifu. mara nyingi alikuwa analewa au alikuwa ni mlevi mbwa.chapombe hafai kabisa. Jambo hili la mama Alexei kuwa na ukaribu na Rasputin likawafikia watu Fulani katika urusi ambao walishangazwa kabisa kusikia kuwa familia ya kifalme /kiutawala inajihusisha na mtu wa aina ya Rasputin. Basi wakaona isiwe kashfa kwa loyal family.wakampoteza Rasputin. Walimwekea sumu kwenye pombe. Wakaona hiyo peke yake haitoshi wakampiga risasi wakamfunga na kumtupa kwenye mto. Huyu jamaa aliuawa mara tatu.

Imagine aliwekewa sumu kifo. Akawapigwa risasi kifo, akafungwa na kutupwa mtoni kifo. Hii yote ilikuwa ni kutokana na hasira walizo kuwa nazo warusi hawa za yeye kujihusisha na royal family wakati akiwa ni mtu mchafu.

Lakini mwaka 1917 kulitokea hali ya sintofahamu huko Urusi, machafuko ya uasi yakazuka huko Petrograd jijini Moscow. Nicholas II alilazimishwa kuachia ngazi. Ajiuzulu ufalme. Maskini.. anastazia na familia yake wakachukuliwa kuwa mateka.wakafungwa.

Wakiwa kifungoni baadaye wakapelekwa Siberia ambako huko gerezani wasichana walikuwa hawaruhusiwi kuwa peke yao.walinzi waliwafuata popote walipoenda hata msalani. Ilikuwa ni ulinzi mkali sana. Na ilipofika julai 16 mwaka 1918 familia nzima iliamshwa asubuhi na mapema.alfajiri, Wakachukuliwa na kupelekwa chumba cha juu kabisa ya jengoni. Wakapangwa katika mstari wakiamini kuwa wanapigwa picha. Maskini hakikuwa wakipigwa picha.walikuwa wakipigwa risasi. Ghafla waliingia watu kadhaa mle ndani na kuanza kumimina risasi. Dada yake anastazia (olga) wazazi wake, daktari wao na watumishi wao wawili hawa walikufa papo hapo...bila hata kuomba maji.

Familia ya Nicholas ilikuwa ina almasi ambazo hizi walikuwa wamezishonea kwenye nguo ya anastazia kuzificha humo. Hivyo zile risasi zilipopigwa zilienda kupiga zile almasi na kudunda. Wale wanajeshi walishangazwa sana na huu muujiza… lakini hawakukoma. Waliendelea kumimina risasi huku zikidunda na kuruka mle chumbani.

Anastasia alikuwa amelala chini akiugulia maumivu. Askari wakaamua kumpiga risasi kichwani. Ilikuwa ni fujo mle ndani chumba kilikuwa kimejaa moshi kutoka kwenye bunduki. Mwishowe Tatiana na maria baada ya kuzishikilia kwa muda roho zao,wakaishiwa nguvu wakazichia ,wakakata roho kwa huzuni sana. Wakijiuliuza wao walikosea nini maskini kuuawa kinyama namna ile kwa kumiminiwa risasi lukuki.

Anastazia alionekana mara ya mwisho akiwa amejikunyata kwa huzuni na maumivu makali ukutani huku akiwa ameshikilia kichwa chake kilichoharbiwa kwa risasi...kilikuwa hakitamaniki.alikishikilia kwa mikono yake yote miwili pengine akijaribu kukikinga.hakuweza,hakuweza.aliuawa kikatilli sana. Alimiminiwa risasi nyingi haikuwa imepata tokea kwa kipindi hicho.chumba kilikuwa kimetapakaa damu...kinanuka damu na moshi.

Na kumekuwa na mkanganyiko katika hili. Maana kuna wanaoamini kuwa anastazia hakufa.
Miili ya ile familia ya kifalme ikachukuliwa na kutupwa kwenye shimo huko msituni. Lile shimo lilikuja kupatikana miaka miwili baadaye miili miwili ikiwa imekosekana. Haifahamiki ilienda wapi na kwa nini mpaka leo. Na pengine hii hupelekea watu wengine waamini kuwa siku ile anastazia hakufa.
HIKI NDICHO KISA CHA ALMASI YA ANASTAZIA

Roho za Familia ile ziweke mahali zinapostahili Amen.
 
Back
Top Bottom