Kisa cha Ally Sykes, Denis Phombeah na Kenneth Kaunda Tanganyika na mkutano wa wapigania uhuru kusini ya sahara 1953

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,249
KISA CHA ALLY SYKES, DENIS PHOMBEAH NA KENNETH KAUNDA TANGANYIKA NA MKUTANO WA WAPIGANIA UHURU KUSINI YA SAHARA 1953

SEHEMU YA KWANZA

Mwaka wa 1953 Harry Nkumbula alikuwa amechaguliwa rais wa African National Congress (ANC) na Kenneth Kaunda aliteuliwa Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kaskazini, Northern Rhodesia sasa Zambia.

Mwezi Agosti Kaunda akawa Katibu Mkuu wa ANC. Haukupita muda Kaunda akaanza kupeleka barua Nairobi, Dar es Salaam na Johannesburg akiitikia rai ya Kenya African Union na chama cha African National Congresss (ANC) cha Afrika ya Kusini kualikwa vyama vya ukombozi kuja Lusaka kwenye mkutano wa vyama vya siasa vya wazalendo kutoka nchi zilizo Kusini mwa Sahara.

Hivi ndivyo ilivyokuwa kuwa ujumbe wa watu watatu wa TAA ukaalikwa na Kenneth Kaunda, kuhudhuria mkutano wa Pan African Congress (ANC) mjini Lusaka. Mwezi wa Novemba, 1953 Ally Sykes alipokea barua kutoka kwa Kaunda akimwalika kuhudhuria mkutano huo.

Wakati ule ANC ilikuwa na manungíuniko kadhaa dhidi ya Waingereza na ilikuwa imeamua katika mapambamo yake kutumia njia za amani ambayo katika barua ambayo Kaunda alimpelekea Ally Sykes aliielezea njia hizo za amani kama hivi, ‘’Hutashirikiana na mtu yoyote katika shauri lolote litakalokuwa na madhara kwa maslahi ya Waafrika.’’

Waafrika nchini Rhodesia Kaskazini walikuwa wanapambana dhidi ya mfumo wa kura tatu ambao baadaye ulitwishwa Tanganyika na Gavana Edward Twining wa 1958.

Baadhi ya malalamiko ambayo Kaunda na ANC iliyoyaona kuwa ni madhara kwa maslahi ya Waafrika ilikuwa uendelezaji wa mashamba na nyumba za Wazungu katika nchi yao.

Lakini suala lililokuwa likiwashughulisha sana watu wengi lilikuwa ni ule msimamo dhidi ya muungano wa nchi yao yaani Northern Rhodesia na Southern Rhodesia.

Kaunda alikuwa akifanya mpango wa kuchukua hatua dhidi ya muungano huo kwa kuwaondosha wafanyakazi wa Kiafrika kutoka kwenye mashamba ya Wazungu na makandarasi wa ujenzi waliokuwa wakifanyakazi za ujenzi wa nyumba za walowezi.

Halikadhalika Kaunda alikuwa akifanya kampeni dhidi ya ubaguzi wa Waafrika.

Kaunda na chama cha ANC kilikuwa kinakusudia kuziunganisha jumuiya zote za Waafrika zilizokuwa zinapinga ukoloni na kuunda Baraza la Waafrika wote kwa ajili ya Afrika iliyo Kusini mwa Sahara ili kuwa na nguvu za umoja wa Waafrika.

Katika kutayarisha mkutano huo mkuu Kaunda alipanga kuvishirikisha Chuo Kikuu cha Makerere Uganda, Achimota Ghana, Fort Hare Afrika ya Kusini na baadhi ya vyuo vikuu nchini Uingereza, India na Marekani.

ANC ilikuwa na mpango wa kuyashughulikia maswala saba katika mkutano huo.

Katika kutayarisha mkutano ule Kaunda alifanya kazi na Rev. Michael Scott na pia alikuwa akitafuta msaada wa Canon Raven wa Maddingley Hall Cambridge na Arthur Lewis, mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Manchester.

Baada ya kupokea mwaliko ule tarehe 12 Novemba, Ally Sykes alimwandikia barua Kaunda akimthibitishia kushiriki kwa chama Tanganyika African Governemt Servant Association (TAGSA) na TAA kwenye mkutano huo.

Denis Phombeah na Bhoke Munanka, katibu wa TAA Jimbo la Ziwa walikuwa walichaguliwa kuwa wawakilishi wa TAA.

Tarehe 1 Desemba, Alexander Tobias aliyekuwa katibu wa TAA alimwandikia barua Kamishina wa Kazi, G, A. Bennet akimuombea ruhusa Ally Sykes ahudhurie mkutano huo wa Lusaka.

Bhoke Munanka alinyimwa pasi ya kusafiria na serikali na kwa hivyo hakuweza kusafiri. Tarehe 10 Desemba, Ally Sykes na Phombeah baada ya kupewa ruhusa na serikali kuhudhuria mkutano huo waliondoka kwa ndege ya aina ya Dakota ya Central African Airways kwenda Lusaka kupitia Salisbury, Southern Rhodesia.

Ally na Phombeah walikuwa ndiyo Waafrika pekee ndani ya ndege hiyo.

Walikuwa wasimame Salisbury na kisha waondoke kwenda Lusaka siku iliyofuata.

Wazalendo hawa wawili wajumbe wa mkutano ule walikuwa wamepanga kufikia Ambassador Hotel, Salisbury, kwa usiku ule na hoteli ilikuwa imethibitisha kuwa imekwisha tayarisha malazi yao.
Image may contain: 2 people, people sitting, text that says 'LIFE'
1596774609312.png

1596774626832.png
1596774638831.png
 
Back
Top Bottom